Mahakama ya Kisutu yawanyima dhamana Harry Kitilya, Sioi Sumari na Shose Sinare

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,502
3,483
77f21e7b-adc2-403e-8d88-9de1605d0ced.jpg

Harry Kitilya akielekea kupanda basi la Magereza
48d98699-e477-40aa-992a-5b94a0087fba.jpg

Bw. Sioi Graham Solomon akielekea kupanda basi la Magereza

Korti ya Kisutu leo, imekataa kuwachia Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya sambamba na Waliokuwa Wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania, Sioi Sumari na Shose Sinare kwa kuwa mashtaka yao hayana dhamana.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), tarehe 1/4/2016 iliwafikisha Mahakamani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Mwenyekiti wa ‘Enterprise Growth Market Advisors Ltd’ (EGMA), Bw. Harry Msamire Kitilya; aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Shose Mori Sinare pamoja na Aliyekuwa Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Sioi Graham Solomon.

Washtakiwa wote walishtakiwa kwa makosa ya:- Kula njama na kujipatia kwa udanganyifu kinyume na kifungu Na. 384 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E. 2002) ; Kughushi kinyume na kifungu Na. 333,335 (a) na 337 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E 2002) ; Utakatishaji wa fedha haramu kinyume na kifungu Na. 12 (a) 13 (a) cha Sheria ya ya Utakatishaji fedha Na. 12 ya Mwaka 2006 ‘Anti- Money Laundering Act’.

Hiki kimbunga kisipoondoka na mtu kitaondoka na bati. Wote wanashutumiwa na matumizi mabaya ya Umma na Ufisadi, wapelekwe mahakamani, sio kuwatumbua kazini halafu wanaachwa Uraiani wakila raha bila kuchukuliwa Sheria yoyote.

Tuiachie Mahakama Ihukumu au isafishe Mtu.
 
HAPA KAZI TU! Unajua palikua pamefikia KIBAKA nikiiba saa Jela miez tisa hawa MAFISIADI wao wanapeta tu mitaani Pu.....vu kabisa.:(:(
 
Back
Top Bottom