shikulaushinye
JF-Expert Member
- Aug 29, 2014
- 828
- 456
Wakati serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuri inapambana kupunguza Rushwa au kuifuta kabisa kwa style ya kutumbua majibu kuna idara mbili bado hazijasikia kauli ya kutumbua majipu. Kuna jeshi la POLISI na MAHAKAMA. Nafikiri Waziri wa mambo ya ndani na waziri wa sheria na katiba hawajafanya kazi yao ipasavyo kutika kuleta mabadiriko kiutendaji kwaani bado taasisi hizi mbili zinafanya kazi bila woga wa kuchukua rushwa. Nashangaa kuwa mambo haya yanafanyika hadharani tume ya kuzuia na kupambana na rushwa iko wapi?
TUKIO:
Wiki iliyopita jamaa yangu akiwa anatoka kimara aliingia barabara kubwa bila tahadhari ya kutosha kwaani gari lake liligongwa kwa nyuma kidogo na gari lililokuwa maina road likiwa mwendo wa kasi. Baada ya ajari madereva hawa walishindwa kufikia muafaka hivyo kumwita POLISI wa usalama barabarani. Baada ya kupima ajari mchoro ulionyesha jamaa yangu alikuwa na makosa. Alimuomba traffic wayamalize traffic police alimshauri waongee na mwenye gari, basi mweye gari aliomba kulipwa fedha ya matengenezo shilingi 200,000/= na jamaa yangu akakubari kumlipa. Baada ya kumalizana na dereva mwenzake polisi/traffic nae alitaka chake kama 100,000/= jamaa yangu hakuwa na kitu alimbembeleza ampe 50,000/= yaishe lkn traffic alizikataa kuwa ni kidogo. Kwa kumkomoa traffic aliamua kumpeleka mahakani, wakati anaombwa kulipa 100,000/= traffic alimwambia kuwa iwapo wataenda mahakamani ajiandae kutoa hongo si chini ya 350,000/= yaani fine 50,000/= na 300,000/= ya hakimu.
MAHAKAMANI KINONDONI:
Jamaa yangu alichukuliwa na traffic ambaye kwa sasa sitamtaja jina, alipomfikisha mahakani alimkabidhi kwa askari wenzake pale mahakani na akawambia wamweke sero ya mahabusu wakati akisubiri kuitwa kwenye kesi. Akiwa mahabusu alikutana na medereva wenye issue km za kwake wakampa njia ya kumaliza ile kesi. Walimshauri amwambia mtu wake wa karibu amwone karani wa mahakama ambaye atamuunganisha na hakimu. Jamaa yangu alimweleza ndugu yake aliyekuwepo mahakamani kumtolea dhamana, ndugi yake alifanikiwa kuonana na karani wa mahakama dada mmoja ambaye aliongea na Hakimu RWEGAMALILA, hakimu aliomba apewe 300,000/= na fine 50,000/= la sivyo angefungiwa leseni yake, kulipa fine na kifungo. Ili amalize kesi, ndugu alikuwa na 200,000/= alimwomba hakimu Rwegamalila (nae ni dada) awasiadie lakini alikataa kuwa kiasi ni kidogo. walibembeleza baadae akakubari kumaliza kesi kwa 230,000/= na fine ikiwwamo. Baada ya kutoa kiasi hicho jamaa yangu alitolewa sero na kupelekwa kukaa chumba cha hakimu huku akipewa maswali atakayo ulizwa na jinsi ya kuyajibu. Baada ya muda mfupi hakimu aliita jina lake na kuanza kumsomea mashitaka alifanya kama alivyofundishwa na kukubari kosa, baada ya hapo alitiwa hatiani na kutakiwa kulipa fine 30,000/= jamaa yangu akaachiwa huru.
FUNDISHO:
Rais JPM na serikali yake bado wana kazi kubwa kumaliza uonevu uliopo ndani ya jeshi la POLISI na MAHAKAMA, kwaani nikiwa mahamakama niliona vijana wengi kwenda segerea kwa kushindwa kuweka mambo yao sawa kwa hakimu kabla ya kesi. Kwa kifupi ukiwa na pesa hutaguswa na mtu wala huwezi kufungwa, hivyo basi wengi waliopo magereza walifungwa kwa sababu hawakuwa na pesa kuwahonga polisi wa upelelezi na hakimu.
OMBI:
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU isikae ofisini Raia wanakosa haki ifanye kazi zake ili kuendana na dhana ya hapa kazi tu.