Makete Kwetu
JF-Expert Member
- Jan 8, 2012
- 531
- 165

Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma, jana ilifuta kesi ya kupinga matokeo ya ubunge yaliyompa ushindi Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (Chadema) katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, kushoto aliyeongozana naye ni mwalimu Samson Mkotya.
Ushindi wa ubunge wa jimbo la Singida Mashariki alioupata Tundu Lissu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hauna doa baada ya kubarikiwa na mahakama.
Mahakama Kuu kanda Maalum ya Dodoma jana imefuta pingamizi la ushindi wa Lissu lililowekwa mahakamani hapo na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Jonathan Njau.
Jaji Berkel Sehel aliamua kufuta kesi hiyo baada ya mlalamikaji Njau kuiomba mahakama kuiondoa kesi hiyo akieleza kuwa hataki kuendelea nayo.
Katika kesi ya msingi, Njau alikuwa akipinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu na kumpa ushindi Lissu. Aliitaka mahakama kufuta matokeo hayo na kuamuru kura zihesabiwe upya.
Chanzo: Dar24
My take: Huyu jamaa ni mara ya pili anabwagwa na TL kwenye uchaguzi na anakata rufaa, ila safari hii naona kaona ni kupoteza pesa na mda wake kuendelea na kesi na mtu 'dizaini' ya Lissu guru wa sheria. TL huwa haweki wakili, anasimamia show mwenyewe