Magufuli's Regime should exercise political tolerance

digba sowey

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
10,173
Reaction score
22,130
Habari wapendwa katika bwana?.
Naomba niende moja kwa moja kwenye hoja ya msingi
Binafsi swala LA kushambuliwa kwa ndugu Tundu Lissu hivi karibuni lilinishitua moyo na nililipokea kwa namna tofauti
Ukweli in kwamba mimi si shabiki wala mfuasi wa CHADEMA lakini bado kitendo hiki sikukipokea kwa furaha
Utawara wa mh JPM mimi naukubali sana tu na bado ninaimani na rais wangu lakini kitendo cha kudhoofisha upinzani kwa namna yoyote ile inabidi kilaaniwe na kila mtanzania bila kujari itikadi zetu, kwani kwa nchi za kiafrika bado hatujafikia kwenye hatua ya utawala bora hata %60+
Hivyo kwa dhana hii bado kuna hitaji kubwa sana la kuendelea na hawa watetezi wa wanyonge ambao mimi nawaita THE VOICE OF THE VOICELESS
Kusema ukweli wapinzan wanekua kama kichocheo kwa kuwasemea watu na pengine hata kuikumbusha serikali mahara ambapo inaenda kinyume
Kwa kuhitimisha napenda kuiomba serikali ya mh JPM kuwa na uvumilivu wa kisiasa kwa kila ntanzania ili wote kwa pamoja tuwe kitu kimoja, lakini pia upinzani nao wawe watu wa kujenga hoja zenye tija kwa taifa letu, kwani sioni tija kunyanganyana matofali wakati tunajenga nyumba moja


Sent using Jamii Forums mobile app
 
how?? the word "tolerance" doesnt exist in his dictionary!
 
He can't.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angeongea DAB angeeleweka
 
Tatizo ni kwamba hawezi kupambana kwa hoja,hivyo njia pekee ni kutumia jeshi la polisi kuzuia hoja kuntu za wapinzani
 
 
Mazuri ya JPM yanafutwa na ukatili. Kauli ambazo kila mara amekuwa akitoa siyo zinazohitajika kutolewa na kiongozi:

1) Alwahi kusema kuwa wanaoandamana kwenda vituo vya polisi walazwe chini (wauawe)
2) Aliwahi kuwaambia makamanda, 'Polisi wanatakiwa kuogopwa. Watu wanaowasumbua hawana hata silaha, kwa nini msiwalaze chini?'
3) Kwenye vita ya madini, anayetukwamisha ni msaliti, adhabu ya msaliti inajulikana, askari mnanielewa

4) Majambazi wenye silaha, muwanyang'anye haraka, nadhani mnanielewa. Wanaowanyang'anya silaha haraka majambazi hawatakiwi kushtakiwa bali kupandishwa vyeo

Ufahamu kuwa huyu ni Amiri Jeshi Mkuu, kauli yake ni amri. Kwa kauli hizo maana yake tayari ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kama alivyowaambia.

Hivi ni jema gani ambalo linazidi ulinzi wa maisha ya watu? Hata kama ungejenga reli za angani, kama watu wanapoteza maisha, zina faida gani? Nchi yetu haipo salama kwa usalama wa maisha ya watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…