Mwingereza
JF-Expert Member
- Jan 21, 2014
- 1,115
- 2,771
Ni kwa sababu unahangaika na dagaa tena kutumia nguvu nyingi huku huku ukiyaacha Nyangumi yakikukejeli. Ungekuwa kweli Musa wa kizazi hiki, anayewapeleka watanzania waliochoshwa na mfumo wa CCM katika nchi ya ahadi, Usingemuacha Prof. Muhongo Kwenye Baraza la mawaziri hasa ukitafakari kashfa zote zinazomuandama, kuanzia Escrow hadi Mafuta Bandarini.
Ungetaka tukuone mwokozi wa watanzania, Basi January Makamba angejiuzulu mapema sana kutokana na tuhuma za rushwa zinazomkabili. Kadhalika Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga angepisha Uchunguzi kutokana na kashfa nzito ya Lugumi.
Matokeo yake Unapoteza muelekeo kufukuzana mahakamani na kijana asiye na mbele wall yuma kwa kuwa amekuita Bwege. Unapoteza muelekeo kumfukuza Anna Malecela wakati CCM imejaa waua tembo na wafanya bisahara ya kulevya. Mbunge wa Rorya, Lameck Airo amewahi kusema kwamba, nguvu yako ni ya Soda, kweli Nguvu yako soda inakwisha