Magufuli tumbua jipu mahakama ya Mbeya

Ubungoubungo

JF-Expert Member
Jul 28, 2008
2,502
741
wakati wa kuhutubia mahakama na kutoa hela nyingi kuboresha mahakama, magufuli alimtaka othman chande atumbue mahakimu wala rushwa na wasio na maadili. suala hili halijafanya kazi katika mahakama, hasa mahakimu mkazi na wilaya. pale mbeya kuna hakimu mmoja anaitwa MTEITE, ni hakimu mkuu wa mkoa wa mbeya.

  1. mtu huyu amekuwa akilalamikiwa sana na wananchi kwamba anakula rushwa na kuharibu kesi ambazo wananchi wameonewa.
  2. imethibitika kuwa anavuta bangi. hakimu mzima anavuta bangi na kila mtu anayemfahamu anaelewa hilo.
  3. uwezo wake kichwani kuelewa sheria ni mdogo, haelewi sheria. wanasheria wanaoappear kwake wamelalamika sana.
  4. juzi kulikuwa na mhasibu mmoja wanasema aliiba pesa Teofilo Kisanji, wanafunzi wakileta ada yeye anapeleka kwenye account yake, na vielelezo vyote TEKU wanasema vimepelekwa mahakamani na kesi iko wazi, yeye akapewa milioni 40,000,000 akamwachia mwizi bila sababu yeyote ya msingi. kwa wale wambao walishafanya kazi na TEKU au wana uhusiano walau mdogo na TEKU, jaribu kufuatilia hili jambo, liko wazi na limesambaa mbeya nzima. mwizi ameachiwa wazi wazi bila hata sababu za msingi kwasababu tu amechukua milioni arobaini. mwizi mwenyewe ameiba milioni 600ml ada za wanafunzi.
kwa niaba ya wapenda haki, tunaomba magufuli ondoa huyu kiumbe, tunazidi kukusanya ushahidi tutauleta hapa wa mambo mengine mengi anayoyafanya ati anataka kupata hela ya kustaafia kwasababu ameshakuwa mzee. mahakimu hawa wanapoteza haki za wananchi, TEKU wameibiwa ushahidi wote umeletwa lakini yeye amechukua rushwa na kumwachia mshitakiwa waziwazi pasipo sababu ya msingi. tunatafuta hukumu tutaileta hapa kwasababu kesi imeshaisha ndio tutaijadili vizuri.
 
jaribu kufikiria, umeibiwa pesa nyingi, unapeleka kesi mahakamani, unategemea kesi iishe mtuhumiwa apewe hukumu na pengine upate compensation au uchukue hukumu yake ukafungue kesi ya madai, halafu hakumu anapokea rushwa nono na kuua kesi anamwachia mshitakiwa, wewe haki yako inapotea hivihivi. mahakama zimekuwa zikilalamikwa sana kila siku lakini hakuna hata hatua yeyote inayochukuliwa kufukuza mahakimu wala rushwa ili kuwe na haki. watu watakimbilia wapi sasa kama mahakama ndio iko namna hiyo?

mbona kenya walifukuza mahakimu karibia kumi kwa rushwa? kuna watu wameshamchukua kwenye clips akipokea rushwa na tutaleta hapa clip hizo za ushahidi, yeye alifikiri ni watoa rushwa kumbe walitumwa kwake kummaliza. movie hii ni ndefu sana subirini.

na haiwezekani hakimu anayevuta bangi akategemewa kutoa haki mahakamani, anaingia mahakamani baada ya kuvuta bangi, bila ya kuvuta bangi hawezi kuendesha kesi. na hata akiongea haongei kama mtu aliyesomea sheria, anaongea kama teja la bangi, kwa wale waliokwisha muona watawaambieni. anavuta bangi, hakimu anavuta bangiiii. polisi mko wapi?
 
huyo hakimu ndiye incharge? Teofilo kisanji ilikuwaje hadi wakaibiwa au huyo mhasibu ndio alikuwa anasaidiana kutapeli bodi ya mikopo kama vyuo vingine walivyofanya? serikali ijaribu kuchunguza hivi vyuo , na sio hicho tu na vyuo vingine, wahasibu wanalipwa hela ndogo sana lakini ni mamilionea huku nje hela hazijulikani wamezipataje.
 
haya malalamiko kama ni ya kweli, yafaa kuchunguzwa, ila tusichukulie kama ndio kweli tukamhukumu bila kuchunguza. ila ukweli ni kwamba, mahakimu wanakula rushwa sana na wanatakiwa kutiwa adabu.
 
Back
Top Bottom