johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 94,114
- 164,504
Ni wanyonge wachache ktk kanisa anglikana dayosisi ya Dsm waliopambana kwa takribani miaka mitatu na hatimaye leo wamefanikiwa kumtumbua askofu mokiwa kwa tuhuma mbalimbali ukiwemo ufisadi.Mmojawao hapa magomeni amenieleza kuwa kasi ya Magufuli ktk kuwashughulikia mafisadi ndio "msingi" wa ushindi wao.Amesema ilifika mahala walimwambia askofu wa Jimbo ikiwa atashindwa kulishughulikia tatizo la mokiwa basi wao watalipeleka mahakamani na wanaamini ktk serikali ya Magufuli fisadi hana rangi,chama wala dini.Binafsi nimpongeze Rais kwani sasa hata mamlaka za dini na taasisi zake zinakiri serikali ipo.Hongereni pia waanglikana mliopambana tumeshuhudia "shoka moja" mbuyu chini!Kuweni wamoja sasa muijenge dayosisi yenu