Machungu hayo kwa mujibu wa Rais Magufuli, yataanza kuonekana wakati wa utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya kwanza kwa Awamu ya Tano, ambayo fedha za maendeleo zimeongezeka kutoka asilimia 27 za bajeti iliyopita, hadi kufikia asilimia 40.
Rais Magufuli alisema katika bajeti hiyo inayotarajiwa kupelekwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, litakaloanza vikao vyake Dodoma wiki ijayo, machungu hayo yataanza kuonekana kwani fedha za chai, semina na safari, zimekatwa na kujaziwa katika fedha za maendeleo.
Wananchi wamechoka kutuona sisi viongozi tunafaidi matunda ya Uhuru wa nchi tangu Uhuru na wao wakiwa wasindikizaji halafu wao tunawaomba kura na wakishatupigia tunawasahau,” alisema na kuongeza kuwa anataka wananchi watoke kwenye machungu na sasa wawe ‘watamu’ kwa maendeleo.
Magufuli alisema lazima viongozi wabadilike na kurudi kwa wananchi wa maisha ya chini na hiyo itakuwa sadaka kwa kuwapa madaraka kwani wananchi wanyonge wameteseka siku nyingi.
Dk Magufuli alisema wananchi wote bila kujali vyama vya siasa, wanalilia maendeleo na maendeleo hayana chama, kwani wananchi wamechoka ‘machama chama’, wanataka kwenda mbele, hivyo hakuna sababu ya kubaki nyuma na kubishana kwa mambo ya chama chama, wakati uchaguzi umepita na aliyeshinda ni yeye ambaye ni CCM.
JE VIONGOZI WA CCM NA UKAWA HASA WALIOEA MADARAKA KAMA NJIA YA KUPATA ULAJI WATAFURAHIA HII KITU??NAAMINI HAWAFURAHI NDO MAANA KILA SIKU NIKUMULAZIMISHA AENDE KUTEMBEA ULAYA HATA KAMA HANA AGENDA