Magufuli, legeza baba, hali ni mbaya!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
16,114
26,006
IMG-20170125-WA0025.jpg

Hali ni mbaya sana, hata wakubwa wanaisoma namba!
 
Hahah kaaaaza hivyo hivyo baba.

Mpk Itv sijui walipiga madili gani eti.hahah
 
Hali ni mbaya sana, hata wakubwa wanaisoma namba!
Mnasema ananyoosha nchi, bado haijanyooka mnasema alegeze.

Nyoosha nyoosha, wadanganyika wamepinda kweli kweli. Nyoosha nchi Magufuli hali inazidi kuwa nzuri, wadanganyika tumefurahi sana.

Uchumi unakuwa kwa mwendokasi, mapangaboi yetu yanapaa kwa mwendokasi, uwanja wa ndege unajengwa kwa mwendokasi, mabasi ynakimbia kwa mwendokasi, njaa imewafikia "wapiga dili" na "wasijitetemesha" kwa mwendokasi.Bei za vyakula zimepungua kwa mwendokasi, kima cha mshahara kimepanda kwa mwendokasi.

Wizara zimehamia Dodoma kwa mwendokasi, Waziri yule anapiga sound kwa mwendokasi, Biashara zimeongezeka kwa mwendokasi, kodi inakusanywa kwa mwendokasi, Makusanyo ya mapato yanapitiliza matarajio kwa kiwango cha Phd kweli kweli..

Tunakopa kwa mwendokasi na deni la taifa linakua kwa mwendokasi, "maisha bora"aka umasikini umeonyoosha vizuri, kila mdanganyika amenyooka au ananyooka vizuri, vitambi vinapungua kwa mwendokasi, tunakunywa juisi kwa pipi kwa mwendokasi, tunajiramba kweli kweli.

Tunaomba misaada kwa mwendokasi... Endelea kutunyoosha, endelea kuinyoosha nchi wala usilegeze, ikiwezekana bana zaidi, bana kweli kweli, bana mpaka inyooke.

Tunakaribia lengo la kuishi kama "malaika"

Wanaosema "hali mbaya" wametumwa na wapiga dili na wafanyabiashara wakwepa kodi? Au wameona dalili za uchumi unaokua kwa mwendo kasi?

Comrade Mwingulu utawafanya nini wanaosema/ wanaotangaza hali mbaya?

Link David Kafulila: Serikali yetu imeanza kukimbizana na T-shirt za njaa
 
Waliambiwa mitaji yao ni ya biashara za juice wakawa wakali.

Ona sasa mshahara wanashindwa kulipa sababu ya madeni.
 
Hajuu bei ya sembe sawa na mchele sababu hajawahi kununua miaka ya karibuni
Kila kitu kwake bure na kodi halipi
 
Naona za kirumi zishawekwa, I,II,III,IV....... Sijui tukifika kwenye namba kubwa kubwa itakuwaje.
 
Acha porojo wewe kwani Magufuli ndiye mdaiwa wa ITV, Nyie kila kitu kinacho enda kombo mnataka kukihusisha na Magufuli.
Mbona una akili ya uchoyo!
Mtoto akiwa na njaa, hata kama baba yake hana kitu mfukoni anamlilia nani, jirani?
 
Back
Top Bottom