Magufuli is Doing Good For This Nation, Tumuassess kwa Positive Attitude, Kwa Mazuri Tumpongeze, Tumuunge Mkono Kumsupport, lakini kwa Mabaya Tumkosoe

Pascal Mayalla but why ?
Sitaki kuamini umetumwa Naomba tuangalie upande mwingine wa shillingi
By the way sioni kikubwaaaaaa sana alichofanya ni machache sana labda nidhamu makazini kuilinda passport yetu (wapopo wameitumia sana kuvuna matunda) otherwise yaliyobaki mengi yalianzishwa na Mkwere

Pascal ni Wananchi wangapi wamekuwa maskini kupindukia hawana milo mitatu wameshindwa kuwapeleka watoto shule Leo kuna mtu anajiamulia kufanya anavyotaka na pesa ya walipa kodi. Kujenga uwanja kufungua hifadhi sijui mbuga ya wanyama etc
Dodoma barabara mbovu etc hakuna cha kuwafanya watu wainvest pale uwanja wa ndege mbovu halafu akawalazimisha watu wahamie Dodoma yeye yupo bado mujini
Inauma sana kuona wazazi wetu wanashindwa kununua hata panadol

Punguzeni hizi shangwe kuna watu wengi wanaumia
Mmesikia ya ICC yalianza hivi hivi

Kama hukoseleki hushauriki mlitaka watu wafanye nini
Kikubwa mkumbuke hii nchi ni ya WaTz wote
Afadhali mazuri yangekuwa mengi kuliko mapungufu lakini ni kinyume ndio maana WaTz hawana furaha ni wachache wenye kuneemeka ndio wenye furaha ipo siku mtazikumbuka hizi nyakati na wakati but it will be too late

Sina chama niko left right n center

Mungu yupo mjue!
 
Ili kutetea bandiko lake Jamaa anadai eti kwa kuwa amewafahamu watoto wa viongozi, wake zao au viongozi wenyewe basi eti angetaka cheo ingekuwa rahisi hahaha huyu jamaa hajui kuwa kuna wenye thamani kwa watu hao kuliko yeye na huenda hao wenye kujulikana/kuthaminiwa zaidi kuliko yeye ndo waliolamba shavu au waliopigiwa chapuo walambe shavu!

Kwa mfano bwana Mayala, kwani unadhani Riziwani anakujua wewe peke yako?, au wewe ndiye best of the bests kwake?

Usijipe umuhimu ambao pengine unaodhani wanakuona muhimu kumbe hawakuoni muhimu kivile kama unavyojidhania。


KUKAA KARIBU NA VINGUNGUTI HAKUKUFANYI KUWA MTAALAMU WA KUCHINJA!

Acha kusifia visivyosifika
 
Ovyo kabisa

Mkubwa mimi sikubaliano na mawazo yako, lakini sioni ya ovyo. Unajua hapa JF inabidi tukubaliane kuwa ni watu wenye mawazo tofauti. Si kila wakati mawazo ya wengi ni sahihi, na mawazo ya wachache sio sahihi.

Kwa jinsi ninavyoona ni kuwa mimi natumia darubini (Telescope) kuingalia Tanzania na maendeleo yake, na wengine wanaoona kama mawazo yangu sio sahihi, naona kama wanatumia hadubini (Microscope) kuiangalia Tanzani. Kwa hiyo inawezekana kabisa kuwa we have different focal points. So it is very possible that one of us is right, i can not say it is me, and you can not say it is you.
 

Mkuu bado hatuna mechanism ya kumuwajibisha kiongozi, awe mbunge au Rais, kufanya tuwe middle income. Kuna kitu kilikuwa kinaitwa vision 2025 angalia yaliyoandikwa mle ndani na tuko wapi sasa. No where. At least tupate umeme, tupate reli maji barabara, kuliko kupata sifuri.
It is a bit interesting mtu anapigania katiba ambayo imejaa maslahi ya wanasiasa, na kuangalia siasa tu. Elimu, afya, usalama, maji, biashara...hakuna vinagusiwa kijuujuu tu. Believe me kama akija rais ambaye ni mbinafsi anafikiri yeye, tumbe lake na familia yake .. hata kabtiba iwe nzuri kiasi gani tutaendelea kufuta vumbi tu.
 
Kesha kusahau ndugu yangu labda ukitaka pitia kwa DAB akupe njia ya kumfikia
 
Paskali,

Hivi Jambazi akivamia familia tajiri akaua wanafamilia wote kisha akatokomea na fedha na vitu vya thamani na kisha akatumia fedha hizo kutoa sadaka, kusaidia mayatima na wajane, je hiyo misaada pamoja na sadaka zitamfanya kua mtu mwema??? Rejea hujuma na ukatili unaoendelea nchini kwa kipindi hiki, kupigwa risasi kwa Tundu Lissu, kupotezwa Azory Gwanda, kuminywa demokrasia, wabunge kuvuliwa ubunge wao kwa matakwa ya mtu mmoja na mengineyo yenye sura kama hayo. Kwa kweli hata akija kunijengea binafsi uwanja wa mpira wa kimataifa kijijini kwangu na kuhamishia hifadhi ya serengeti wilayani kwangu, bado huyo mtu kwangu hana nia njema!
 
Endelea na kazi zako za kusifu na kuabudu mkuu Pascal Mayalla , usikubali tukupangie mapambio ya kupiga😅
 

Mkuu unajua nadhangaa sana kwanini baadhi yetu tunaona umaskini sasa, na tunapretend kuumia sana na umaskini sasa kuliko zamani. There is no way mtu akaniambia kuwa watanzania we are worse off today than we were five years ago.

Ni kosa sana kusema mambo yamekuwa magumu. As far as i can remember sijawahi kusikia hata siku moja mtu akisema sasa maisha rahisi, this is the song we have been singing toke enzi za mwalimu.

Kuna baadhi ya mambo tunayafanya kama nchi. Hata hayo uliyosema yalianza enzi za Mkwere, infact yalianza enzi za Mkapa, kuna plan ya taifa tunayotakiwa kuifuata regardless anakuja rais gani. Lakini ukiangalia sana style ya utawala wa mkwere, ni kama alikuwa ana-enjoy urais, sio kama alikuwa bize kufanya kazi kwa ajili ya nchi.

Nakuunga mkono sana kwa kuangalia hali ya nchi yetu bila kuwa kwenye kivuli cha vyama. Maana kuna mdudu mmoja ameingia hapa JF, inakuwa kama ni uwanja wa mapambano kati ya makundi-maslahi ndani ya CCM. Kwa hiyo ni kama watu wanataka kutuaminisha wana JF kuwa mawazo ya kumpinga JPM ndio sahihi, na kukosoa wapinzani wake sio sahihi.

Hii nchi bila kuitikisa kwanza haitapiga hatua hata kidogo. What can be more good than vituo zaidi ya 200 vya afya? Serikali ya awamu ya 5 imejenga vituo vingi vya afya kuliko Mwalimu Nyerere, Mwinyi, Mkapa na JK combined. Kuna ubaya gani kusifia hili? Tukubali umeme wa REA ulianza wakati wa JK, angalia kasi yake kwa sasa, angalia maana ya Stiglers kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Tanzania, angalia issue ya maji kwa Tanzania kwa sasa kumekuwa na matumaini.

Ni kweli maisha yamekuwa magumu zaidi kwa kuwa hela za dawa za kulevya zimepungua mtaani, hela za ufisadi zimepungua mtaani, kuishi kwa kutegemea kupiga mizinga kumekuwa kugumu. NI kweli hela chafu zilikuwa zinasaidia kuendelesha baadhi ya biashara mitaani. Tukubali kuwa baadhi ya wenzetu wanakufa kutokana na uhaba wa dawa za kulevya. Haya ni matokeo ya hatukutegemea. So we have to face the reality.
 
Teh teh teh 😂😂teh 🤣🤣🤣🤣 we mzee una mikwara aisee ....
 

The government snitch of all time!

You’ve turned state!

No street cred at all!
 
Kwa mfano ninakuwa mwanafunzi halafu nakutana na pepa natakiwa kuchagua swali la kujibu kati ya kuelezea 1.kwa nini Magufuli sio kiongozi mzuri? au 2. Kwa nini Magufuli ni kiongozi mzuri? ...Namba moja kwangu lingekuwa rahisi sana kwasababu hoja zipo nyingi sana ..lakini la pili ningehofia kufeli kwa sababu ningehitaji kudanganya sana kulijibu kwa urefu...
 
Ni ndefu sana.Weka summary
 
Kuna watu kipindi hiki cha Magu tumepata haki zetu ambazo huko nyuma ingekuwa ndoto kuzipata.
Leo hii hakuna mtu anaweza kuniambia "unanijua mimi ni nani?" au "kashitaki kokote unakokujua"
Ofcourse kuna makosa ya kibinadamu lakini kiukweli nchi kwa sasa imepata KIONGOZI.
Hao wanaoshindwa kununua panadol mwanzo walikuwa wanazipataje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…