Magufuli chukua tahadhali kubwa

Magufuli chukua tahadhali kubwa

boyayoparuparu

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
343
Reaction score
82
Sasa hivi hakuna biashara ya watumwa,kinachoendelea duniani ni utumwa wa kiuchumi,tunawatumikia mabwanyenye kupitia fedha,ukitaka fedha yao moja uwe na za kwetu gunia moja,hawakubali hata kidogo wakiona nchi flani fedha yake ikaikaribia thamani ya dola,endapo nchi hiyo inataka kuikaribia fedha yao zitafanyika mbinu mbali mbali ili fedha yao ishuke thamani na utumwa wa kiuchumi uendelee.

Kinachotokea Syria,kilicho mtokea Gaddafi,Saddam nk ni moja ya mbinu zilizotumika kuhakikisha utumwa wa kiuchumi unaendelea.

Katika nchi zetu hapa tuna mifano katika nchi yetu Tanzania, Burundi, Rwanda.Burundi na Rwanda mara nyingi kunakuwa na vita za wenyewe kwa wenyewe mara tu fedha zao zinapoikaribia dola,bahati mbaya hata wasomi hawana muda wa kutafuta chanzo cha vita hizo badala yake wanaimba wimbo ulioanzishwa na vyombo vya Magharibi.

Tanzania tulipokuwa na uchumi imara tulipiganishwa na nchi ya Uganda,wakati Kikwete anashika nchi,alijaribu kutoa yale mabilioni yaliyokuwa yanaitwa ya Kikwete lakini akawa Rais wa kwanza kukutana na rais Obama,mara tu baada ya Obama kuapishwa na baada ya hapo hatukusikia tena akitoa mabilioni yale wakati alikuwa amekwishaahidi kuyatoa kila mwaka.

Sasa napenda kumwambia Magufuli, ajue kuwa anachokisema na kuahidi kukifanya ajue kuwa anahitaji tahadhari kubwa sana,kwenye kila kitu hasa kwa maisha yake,yeyote anayebisha aniambie kwanza sababu ya marais wa Iraq,Libya,Venezuela nk ni kwanini waliuawa!!

Syria ni kwanini anawindwa kama mbwa,rais yeyote anajenga urafiki, uswahiba,anayesifiwa na mabeberu,takwimu za kiuchumi zinasalia kuwa namba tu,hazina uhusiano na hali halisi kwa maisha ya mwananchi wa hali ya chini.

TUNASOMESHWA MANAMBA TU.
 
Tunaamini kuwa Magufuli ni chaguo la Mungu....atamlinda na kumtetea, relax
 
Haya ni mawazo ya Nkuruzinza. Mbona kule Singapore, Malesia nk wanafanya vyema lkn hawajauliwa? Kwa hiyo yale anayoyafanya Nkuruzinza ni nchi za Magharibi ndo zimemwambia asitoke madarakani? Bila shaka hatayale
 
Haya ni mawazo ya Nkuruzinza. Mbona kule Singapore, Malesia nk wanafanya vyema lkn hawajauliwa? Kwa hiyo yale anayoyafanya Nkuruzinza ni nchi za Magharibi ndo zimemwambia asitoke madarakani? Bila shaka hata yale ya Zanzibar yanasababishwa na wazungu, eti?? Hizo nchi ulizozitaja chanzo cha matatizo yao ni kung'ang'ania madaraka km wanavyofanya ccm kule Zanzibar.
 
Isaya nehemia si kila kitu lazima uchangie,kama hujui kaa kimya,nenda kasome sera za amerika wapo wazi kabisa kwamba hawatajishughulisha na jambo lisilo na maslahi kwao,kama hakuna mkono wa mabeberu nkulunziza angekuwa hayupo asinge kuwa rais,zile fujo zina saidia sana kukuza thamani ya dola na kuangusha faranga ya burundi,tunapoona viongozi wa nchi za magharibi wakitembelea nchi flani afrika ujue wanafuata maslahi yao sio upendo wa kawaida tu,hiyo asia unayoisema ina nini?
 
Haya ni mawazo ya Nkuruzinza. Mbona kule Singapore, Malesia nk wanafanya vyema lkn hawajauliwa? Kwa hiyo yale anayoyafanya Nkuruzinza ni nchi za Magharibi ndo zimemwambia asitoke madarakani? Bila shaka hata yale ya Zanzibar yanasababishwa na wazungu, eti?? Hizo nchi ulizozitaja chanzo cha matatizo yao ni kung'ang'ania madaraka km wanavyofanya ccm kule Zanzibar.
Hawa ndio watanzania wanaojiita wameenda shule wakaelimika! Kaazi kweli kweli,huyu nae anafikiri ushauri weke nao utaxingatiwa eti! Hivi sababu ya Nkurunzinza kubaki madarakani eti nae Marekani inamwonea wivu! Kwi kwi kwi!
 
Boyayu una hoja lakini jukuipanga vizuri, wachache wataiona au kukuelewa.
 
Petrol,asante kwa kujua kama nina hoja kupanga inawezekana ni uwezo wangu mdogo,nahitaji maombi
 
mleta mada muwongo na mvivu au anataka kutuaminisha mawazo yake ,


The current OMR/TZS exchange rate is 5640.31. (Last updated on November 22, 2015 09:00:02 UTC).
It means you will get TZS 5640.3065 for 1 OMR or OMR 0.0177 for 100 TZS.

Mbona hawapigani
 
Mh, mawazo mengine ni hatari.....mleta hoja nimejitahidi kukusoma na kwa kukuelewa unataka kutuambia MAREKANI wanafurahia vita uovu wa Nkurunzinza ili dola ya US ibaki kuwa juu, bila shaka pia una maanisha wanatamani tuendelee kuwa na ufisadi,mipango mibovu ili hela yetu isiinuke thamani.......hii imekuwa ngumu kumeza.
 
Sina tatizo na mawazo yenu wote tuendelee kuamini tunavyo amini,bahati mbaya sijui umri wa ninajadiliana nao,wakati mwl nyerere akiwa rais wa nchi hii aliwahi kutuambia sio kwa bahati mbaya kuwa anashinikizwa kushusha thamani ya tsh huo nao si ufuatiliaji wa mabeberu? Kuna mambo mengi ya kuwaeleza nanyi jaribuni kufuatilia mambo mtabaini mengi,tusiende shule ili tumtumikie mzungu na matumbo yetu bila kuishughulisha akili na kuondokana na utumwa wa kifra,mtueleze sasa nikisa gani kulicho pelekea Gadafi akauwawa na kwanini mabeberu ndio walikusanya nguvu na kumuuwa? Walicho ahidiwa walybia wamekipata?uchumi wao uko kwenye hali gani?tunaweza kuwa na rais mzuri duniani zaidi ya Gadafi?
 
Back
Top Bottom