assadsyria3
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 6,903
- 4,051
BAADHI ya wafanyabiashara kwa kushirikiana na sehemu ya viongozi waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameanza kutengeneza mkakati wa kumdhoofisha, Rais John Magufuli, kupitia chama chake.
Katika mkakati huo baadhi ya vigogo wa chama wenye mafungamano ya karibu na wafanyabiashara hasa wanaoshiriki biashara zenye utata na kukwepa kodi, wamepanga kuhakikisha Magufuli hapewi uenyekiti wa chama hicho mapema kama ilivyo mazoea ya chama hicho, badala yake wanataka abaki kuwa Rais hadi mwaka 2017 chama hicho kitakapofanya uchaguzi.
Mtazamo wa vigogo hao ni kwamba mpaka muda huo chama chini ya Mwenyekiti wake wa sasa, Rais (mstaafu) Jakaya Kikwete, wanaweza kuwa na namna ya kudhibiti kasi ya Magufuli ambayo inaelezwa kuwagusa vibaya wanaoaminika kuwa walikuwa wafadhili wa chama hicho.
Wengi wa wafanyabiashara na vigogo hao ambao walikuwa ni wananufaika katika biashara zao kupitia ufadhili wa kuchangia chama na kuwa karibu na viongozi ili ‘kufanya mambo yao yaende vizuri' wanaelezwa kuanza ushawishi kwa Mwenyekiti Kikwete, aendelee na uenyekiti mpaka ufike wakati wa uchaguzi rasmi kwa mujibu wa kalenda ya chama.
"Mpaka wakati huo wanaamini watakuwa wameweka mikakati mingine ya kuweza kukabiliana na kasi hii, kwa sababu sasa hivi ni kama amewashtukiza hawakumtarajia kama angeweza kuwa ‘mbogo' namna hii," kinaeleza chanzo chetu kutoka CCM Makao Makuu.
Chanzo hicho kinaeleza kwamba hofu hiyo pia inatokana na mageuzi makubwa ambayo Magufuli amedhamiria kuyafanya akiwa Mwenyekiti wa chama hicho.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Magufuli anakerwa na mambo kadhaa ndani ya CCM ambayo akishakabidhiwa tu uenyekiti anaweza kuanza nayo nakuleta mabadiliko makubwa.
"Hakuna suala linamkera kama rushwa ndani ya chama hasa katika uchaguzi, akipata uenyekiti Watanzania watashuhudia uchaguzi wa ajabu ndani ya CCM mwaka 2017, pesa hazitakuwa na nafasi," kinaeleza chanzo hicho.
Kwa mujibu wa chanzo chetu hicho, rushwa ndani ya CCM ni jambo linalomkera mno Magufuli, hasa watu wanaponunua uongozi kwa kisingizio cha kuchaguliwa.
"Matumizi ya fedha za rushwa kwenye chaguzi za chama litakuwa jambo hatari kwa mgombea, hatakuwa na mchezo na mtu, na yeye ni mfano halisi, wakati anaomba kuteuliwa na chama, hakuwa na majigambo ya kutumia fedha na kwa hiyo, chini ya uenyekiti wake wana CCM wajiandae kurudi kwenye misingi ya chama hicho," kinasema chanzo hicho.
Jambo jingine ambalo linaweza kukutana na kasi ya Magufuli ni suala la Ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM. Inaelezwa kwamba hatua ya kupanua wigo wa wajumbe wa NEC haijakisaidia sana chama kama ilivyotarajiwa. Ingawa hatua hiyo inatarajiwa kukukutana na upinzani mkubwa, hasa kutoka kwa wajumbe wenyewe wa NEC ya sasa.
"Uko mtazamo miongoni mwa baadhi ya wana CCM kwamba hadhi ya vikao vya NEC imeshuka kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wajumbe. Hakuna uhakika wa vikao kutunza siri kutokana na wingi wa wajumbe na mchanganyiko unaokuwepo," anaeleza mmoja wa makatibu wa CCM kutoka mkoa mmoja wa kanda ya kati, ambaye kwa sababu za wazi aliomba asitajwe jina gazetini.
Wakati baadhi ya wana CCM wakifanya juhudi hizo kumfanya Magufuli asipatiwe uenyekiti mapema, wana CCM wengine wanatamani hali hiyo itokee mapema ili arekebishe mambo kadhaa ili kukinusuru chama chao.
"Chama kilifika mahali kikajisahau, kina rasilimali nyingi lakini kilijiachia kikatekwa na wafanyabiashara, chama kikageuka ombaomba badala ya kutumia rasilimali zake kujitegemea. Magufuli akiingia atajenga utamaduni wa chama kujitegemea na kujiondoa katika utegemezi," anasema Mweka Hazina wa Chama hicho kutoka moja ya mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Hofu ya baadhi ya vigogo hao wa CCM pia inajengwa juu ya kauli zake kuhusu unafiki wa baadhi ya wanachama ambao wanajificha ndani ya chama hicho wakati matendo yao hayashabihiani na itikadi ya chama husika.
Akiwashukuru wanachama wa CCM mara baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu, Rais Magufuli aliwaambia wana CCM waliokusanyika katika ofisi ndogo za CCM Lumumba, jijini Dar es Salaam kwamba ni bora kuishi na mchawi kuliko mnafiki, huku akimuomba mwenyekiti wa chama hicho, Kikwete, kutowahurumia wanaokihujumu.
"Nisiposema nitakuwa mnafiki, msema kweli ni mpenzi wa Mungu, watubu wajirekebishe. Ni mara kumi kuwa na mpinzani kutoka nje kuliko ndani ya chama, mipango yenu mtaipanga mchana usiku wataitoa nje ni afadhali uwe na mchawi atakuroga ufe kuliko mnafiki ndani," alisema na kuongeza; "Lakini ukweli utabaki kuwa ukweli, wewe (Rais mstaafu Kikwete) ni mwenyekiti, lakini ulikaa na wanafiki ndani ya CCM, ndiyo wametufanya wakati mwingine tufike hapa tulipofika, ndiyo wametufanya tufike hapa tulipo leo.
Kwa hiyo, nakuomba ukitengeneze chama chetu vizuri ukishamgundua mnafiki usikae naye fukuza kesho, nimeona hili nilizungumze lakini unisamehe sana kwa sababu ningebaki nalo moyoni lingenisababishia kiungulia ambacho nimekiona wakati nazunguka nikiwa kwenye kampeni."
Aidha kauli nyingine ya Magufuli ambayo imewatia hofu wanaopenda kujipendekeza kwa viongozi ili kupisha mambo yao ya ovyo, ni ile aliyoitoa kwa wafanyabiashara kwamba hakutaka wamchangie pesa za kampeni kwa kuwa alijua anataka kuja kufanya kazi.
Akizungumzia suala la Rais (mstaafu) Kikwete, kumwachia uenyekiti Rais Magufuli, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, alisema suala hilo ni jambo la kutumia busara kwa kuwa chama kimekuwa na utaratibu wa marais wastaafu kuondoka mapema kabla ya muda wao.
Alisema chama kiliamua kuunganisha kofia hizo mbili za uenyekiti na urais, ili kuondoa uwezekano wa mgongano kati ya Rais na Mwenyekiti wa chama.
"Chama kinatoa mgombea akichaguliwa anakuwa na madaraka ya Rais, lakini pia anatekeleza Ilani ya chama, Mwenyekiti wa chama naye ana madaraka yake mengi kwenye chama. Sasa madaraka yakiwa huku na huku yanaweza kuleta mgongano, japokuwa siyo lazima," alisema Butiku.
Alioongeza kuwa kwa hali ya sasa kati ya Rais Magufuli na Mwenyekiti wa wa CCM, Kikwete, kinachotakiwa ni busara tu kutumika.
"Mwenyekiti wa sasa akiamua kutoka amwachie ni vizuri zaidi, lakini lisipotokea hilo pia linaeleweka, hakuna kanuni inayomlazimisha. Mwenyekiti akiamua kuachia ili iwe rahisi kuondoa mivutano ni bora zaidi," alisema Butiku.
Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salam (UDSM), Dk. Benson Bana alisema suala la Rais kuwa mwenyekiti wa chama au asiwe halina mashiko kwa sababu katika mazingira ya sasa, chama hata kama ni tawala hakishiki hatamu.
Alisema madaraka ya Rais yameainishwa kwenye Katiba na kazi zake zimeainishwa, chama kinatakiwa kumsaidia kuonyesha wapi pana ‘majipu' ili aendelee kuyatumbua wakati akitekeleza ilani ya chama chake.
Alipoulizwa kama watu wasioyatakia mema mabadiliko yanayofanywa na Rais Magufuli kuwa wanaweza kujipenyeza kupitia chama ili kukitumia kudhoofisha juhudi hizo, alisema jambo hilo haliwezekani.
"Vyama vyetu vya siasa havina ubavu huo, anachofanya sasa Rais Magufuli ni kazi ya kukisaidia chama, unamdhibiti vipi na kwa nini umdhibiti mtu anayetumbua majipu namna hii?" alihoji Dk. Bana.
Akizungumzia suala hilo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Msukuma, ameliambia Raia Mwema kuwa, hakuna sababu ya watu kushinikiza au kulazamisha mambo kwa sababu chama kinaongozwa kwa sheria na kanuni zake.
"Kwa busara anaweza kuachia, lakini hatujaona tatizo (kwa Mweyekiti wa chama, Kikwete) kama bado anaona ana nguvu hatuna sababu ya kumlazimisha, kwa sababu sheria wala kanuni hazimlazimishi kupumzika. Vinginevyo tupige kura ya no confidence (kutokuwa na imani) kwa Mwenyekiti jambo ambalo kwa sasa halina sababu," alisema Msukuma.
Akizungumzia hali hiyo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC ya CCM, Nape Nnauye, alisema CCM kinaongozwa kwa sheria, kanuni, utaratibu na utamaduni.
"Ukiangalia historia ya chama hiki, tangu mwanzo utaona jinsi gani chama hiki kinavyojiendesha, kwa hiyo katika hilo hakuna kitu cha ajabu," alisema Nape akizungumzia Mwenyekiti wa chama kumwachia kiti Rais aliyepo madarakani, kabla ya uchaguzi wa chama.
Chanzo: RaiaMwema