GreatConqueror
Member
- Mar 27, 2009
- 75
- 5
Wana jamvi leo katika pitapita zangu za kuganga njaa nilijikuta nikiwa BRELA. Katika kupita huku na kule nikamuona Maghufuli akiwa na maafisa wa BRELA akistaajabu mafaili kuhifadhiwa hadi miguuni kwa maofisa wa Brela. Baadaye nikapata taarifa kuwa walimpa kisingizio kuwa hawana jengo na mafaili ni mengi sana. Nampongeza angalau kwa kuhoji ile hali kwani sijawahi kusikia waziri mwenye dhamana ya BRELA (WA VIWANDA NA BIASHARA) katembelea Agency hiyo nyeti serikalini. BRELA mtaendelea kuhifadhi mafaili kama maembe hadi lini? Mbona pesa mnakusanya?
NAWASILISHA!
Sasa Magufuli nae kawa mkubwa sasa, kama kweli anauchungu na nchi yetu anaogopa nini upresidenti! Ajikaze tuu, aanze mchakato na mikakati ya nguvu ndani na nje ya chama mapema (lakini si kama alivyofanya Kikwete kuhonga watu). Tunaweza kupata kiongozi angalau wa maanamaana kiasi.
... kwani sijawahi kusikia waziri mwenye dhamana ya BRELA (WA VIWANDA NA BIASHARA) katembelea Agency hiyo nyeti serikalini.
Hivyo ndivyo nchi yetu ilivyo jamani sio huko BRELA tu ofisi nyingi hiyo ndo habari
Jamani kuna watu wanajituma.
Huyu Kaka yetu Mh. J.P.Maghufuli, kweli anafanya kazi. Kila anakopita anaacha ukumbusho, yaani ana-deliver kuliko wenzie wengi. 50% ya cabinet ingekuwa na watu wa aina yake, sijui tungekuwa wapi sasa.
Jamani kuna watu wanajituma.
Huyu Kaka yetu Mh. J.P.Maghufuli, kweli anafanya kazi. Kila anakopita anaacha ukumbusho, yaani ana-deliver kuliko wenzie wengi. 50% ya cabinet ingekuwa na watu wa aina yake, sijui tungekuwa wapi sasa.
Wewee mamah, Magufuli ana tatizo moja kubwa, anafanya kazi kiukweli kuiwazidi mabosi wake kiasi cha kufikia kuwafunika. Hili ni kosa kubwa sana kwa siasa zetu za bongo. just consider coverage yake kwenye vyombo vya habari wakati wa Benjamini/Fredrick na wakati wa Jakaya /Edward. maana hata baada ya kkuondoshwa miundo mbinu na kupelekwa ardhi wakaona utendaji unazidi kuboreshwa wakaona wamtupe huku aliko sasa. ajabu anazidi kufanya makubwa.
Iko hivi,huyu jamaa ana guest house yake huko Biharamulo alienda BRELA yeye mwenyewe kwaajili ya kusajili Business name ya hiyo biashara yake ndiyo akakutana na hiyo hali na akasema akitoka hapo ataenda kushughulikia TIN number TRA yeye mwenyewe na kufuatilia leseni pia ila ajionea mazingira ya hizo taasisi husika hadi atakapokamilisha anachofuatilia.Sasa kama BRELA iko chini ya Viwanda na Biashara, waziri wa Uvuvi alienda kukagua BRELA kwa msingi gani?
Sasa kama BRELA iko chini ya Viwanda na Biashara, waziri wa Uvuvi alienda kukagua BRELA kwa msingi gani?
Iko hivi,huyu jamaa ana guest house yake huko Biharamulo alienda BRELA yeye mwenyewe kwaajili ya kusajili Business name ya hiyo biashara yake ndiyo akakutana na hiyo hali na akasema akitoka hapo ataenda kushughulikia TIN number TRA yeye mwenyewe na kufuatilia leseni pia ila ajionea mazingira ya hizo taasisi husika hadi atakapokamilisha anachofuatilia.