Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,069
- 151,316
Ukiacha wapinzani, watu wengine wote maarufu na wenye kupata nafasi katika vyombo vya habari wakiwemo na waandishi wengi wa nchii hii,kazi imekuwa ni moja tu kumsifia Raisi.
Mpaka sasa ni Jenerali Ulimwengu tu miongoni wa watu mashuhuri /maarufu na wenye ushawishi katika jamii ndio aliweza kumkosa Raisi Magufuli hadharani wengine wote ama wako kimya na wakiiongea basi ni kumwaga sifa kedekede kwa mh.
Mtu mwingine alikuwa ni Waziri wa Zamani wa Mambo ya Nje,bwana Bernad Membe ambae wakati fulani alijaribu kukosoa utawala huu wa sasa lakini nae aliishia kushambuliwa tu kama alivyoshambuliwa Jenerali Uimwengu hivi karibuni.
Ni sahihi na ni haki yao kusifu pale mh. anapofanya jambo zuri kama ambavyo hata wapinzani wamekuwa wakifanya.Hata hivyo, ni dhambi kubwa kukaa kimya pale panapostahili kukosolewa na badala yake kusubiri mazuri yatokee ndio mpate nafasi ya kusema na kuona kazi ya kukosoa mwenendo wa serikali ni kazi ya wapinzani tu,wapinzani ambao mara nyingi wanatafsiriwa kama ni watu wa wenye wivu tu.
Mimi nasema wale wote wenye nafasi na ushawishi katika jamii watimize wajibu wao kwa kuishauri serikali na wasipotimiza,muda ndio utasema na wakati huo ukifika si ajabu wakawa wanawakwepa hata waandishi.
Si mnakumbuka zile kauli za chaguo la Mungu?Leo hii kiko wapi?
Ombwe alilotuachia Baba wa Taifa sijui ni nani wa kuliziba maana yeye aliweza kosoa na kushauri bila kumuonea mtu aibu.
Uzuri wote tuko kwenye boti moja na tukizama, tunazama wote.
Tusubiri.