Magufuli ataka Watanzania wasichezee amani

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
1,056
Reaction score
1,086
RAIS John Magufuli amewataka Watanzania wasichezee amani kwa kuwa Tanzania ni nchi pekee iliyobakia kuwa kisiwa cha amani.

“Tusichezee amani. Tuidumishe amani yetu kwani kuna watu walijitoa mhanga kupigania amani hiyo na kuifikisha nchi hapa ilipo,” alisema Rais Magufuli mjini hapa jana alipohutubia maelfu ya wakazi wa Dodoma na Watanzania katika sherehe ya Siku ya Mashujaa.

Rais Magufuli aliyeshangiliwa na wananchi waliokuwa wakipunga bendera ndogo za Taifa baada ya kupanda jukwaani, alisema kuwa wakati tunaadhimisha Siku ya Mashujaa tukumbuke wapo watu walikubali roho zao zipotee.

Alitoa mfano wa waliopigania ukombozi wa nchi mbalimbali barani Afrika kama Msumbiji, Namibia, Angola, Comoro na Afrika Kusini. Wengine ni waliopigana vita ya nduli Iddi Amin wa Uganda mwaka 1977, wakati nduli alipovamia Tanzania na wakati wa Mapinduzi kisiwani Zanzibar mwaka 1964.

Aliwataja mashujaa wengine wa Taifa ambao hawawezi kusahaulika kwa mchango wao mkubwa katika ukombozi wa nchi kuwa ni Baba wa Taifa , Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Abeid Amaan Karume wa Zanzibar.

Alisema waasisi hao walijitahidi kuifikisha nchi hapa ilipo.

“Tanzania imekuwa na amani na utulivu kwa sababu wapo watu waliojitoa mhanga kuipigania. Tudumishe amani yetu. Hawa wenzetu waliotangulia, hawakujali dini zao na makabila yao. Walijitahidi kuwaunganisha Watanzania wote,” alisema Rais Magufuli na kuwataka Watanzania wasichezee amani na asitokee wa kuichafua kwani kila mmoja ana wajibu wa kuidumisha. Kwa upande wake, Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi aliwataka Watanzania kulinda umoja na amani ya nchi.

Aliwataka kuendelea kumuombea dua Rais Magufuli ili awe mwepesi katika kutekeleza yote anayodhamiria kwakuwa amepewa dhamana kubwa ya kuongoza Watanzania zaidi ya milioni 40.

“Tuache ushetani, tuache ubilisi, tushughulike na yale yanayotuhusu sisi wenyewe, watoto wetu na vizazi vyetu. Tudumishe utulivu na kupendana. Heri na amani haiji bila kupatikana usawa,” alisema na kuongeza kuwa Rais Magufuli amekuwa kiongozi wa watu, anayepigania watu wanaokosa haki, wanaoonewa na wanaofanyiwa fitna.

Alisema amani ni kitu muhimu sana hivyo Watanzania wafunge masikio wasisikie mabalaa na machafuko yanayotokea katika nchi jirani. Aliongeza kuwa, Mungu katujalia amani hivyo tuidumishe ili asitokee mtu kuiharibu.

“Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Huko nje maguu yanavunjika na yataendelea kuvunjika,” alionya Mwinyi. Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein alisema atashirikiana na Rais Magufuli kuimarisha amani ya Tanzania.

Alisema anafahamu uwezo, nia, ari, jitihada na kasi ya Rais Magufuli ya kuipeleka Tanzania kuwa nchi yenye matumaini na maendeleo makubwa.

Akitoa dua katika maadhimisho hayo kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), Kaimu Shehe wa mkoa wa Dodoma, Ahmed Said, alisema Watanzania wanathamini mchango mkubwa walioutoa mashujaa waliopigania nchi na kwamba mchango wao utaendelea kuthaminiwa.

Alisema umoja na amani havikushuka nchini kama mvua, bali wazee na askari walitoa jasho na kupoteza maisha kwa ajili ya nchi ndio waliosababisha viwepo.

Alisema Watanzania hawawezi kusahau waasisi walioongoza mapambano wakiwemo Mwalimu Julius Nyerere, Shehe Abeid Amaan Karume na Rashidi Kawawa.

“Tunamuomba Mungu aendelee kuilinda nchi yetu na kudumisha amani, utulivu na umoja uliopo,” alisema Shehe Said. Pia, Shehe Said aliwataka Watanzania waendelee kumuombea Rais Magufuli awe na moyo wa ujasiri, subira na afya njema ili aweze kuongoza nchi kama ilivyokusudiwa.

Aliomba Mungu awaepushie shari viongozi wanaomsaidia Rais Magufuli kuongoza Serikali. Shehe huyo aliomba Mungu ailinde Tanzania na Watanzania kwa ujumla na pia aubariki Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili uendelee kudumu.

Mchungaji Leonard Mtaita akifanya maombi kwa niaba ya Umoja wa Makanisa ya Kikristo (CCT), alisema waasisi wa Taifa wametoa mchango mkubwa katika kujenga na kudumisha amani.

Aliwataka Watanzania kudumisha upendo na amani kama njia ya kuwaenzi. Mtaita aliwahimiza Watanzania waendelee kumuombea Magufuli aendelee kuwa na afya njema, hekima na busara ili kuwatumikia Watanzania. Alimsifu Rais kwa kuwatumikia kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.

Padri Onesmo Wisi alifanya maombi kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), alisema Watanzania wanafurahia amani ambayo waasisi na askari wetu waliipigania. Aliwahimiza kuwa na umoja ili kulinda amani iliyopo na kujiepusha na uchochezi wa kisiasa, ambao mwisho wake ni vurugu.

Katika maadhimisho hayo, shughuli zilizofanyika ni pamoja na kuweka silaha za asili za mashujaa na maua kwenye mnara, ambapo Rais Magufuli aliweka mkuki na ngao na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange aliweka sime. Kiongozi wa Mabalozi nchini, Balozi Ambrosio Lukoki aliweka shada la maua.

Lukoki ni Balozi wa Angola nchini. Meya wa Dodoma, Jaffar Mwanyemba aliweka upinde na mshale na Mwenyekiti wa Tanzania Legion, Rashid Bakar Ngonji aliweka shoka.

Pia mizinga miwili ilipigwa katika sherehe hizo zilizopambwa na gwaride maalumu. Maelfu ya wakazi wa Dodoma walihudhuria sherehe hizo. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa sherehe za Siku ya Mashujaa kufanyika nje ya Dar es Salaam.

Chanzo Habari Leo

Maoni yangu

Watanzania tumuunge mkono Rais Magufuli kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake katika kuhakikisha amani utulivu vinaendelea kuwepo nchini, tusikubali kutumiwa na yeyote katika kuondoa utulivu tulionao iwe mwanasiasa au wanaotaka kutumia dini kama kigezo cha kuondoa utulivu tulia nao.

Vijana tuna nafasi kubwa ya kulinda nchi yetu, tuache kutumiwa na wanasiasa waroho wa madaraka wanaodhani bila yao kupata madaraka Tanzania haiwezi kupiga hatua na kupata maendeleo, wanaotaka kututumia vijana kama daraja la kufanikisha mambo yao, Watanzania tuache masihara ya kuvikebeshi na kuvifanyia istidhai vyombo vyeti vya ulinzi na usalama kwani vinafanya kazi kubwa ya kuhakikisha hali iliyo ya amani na utulivui inaendelea kuwepo.
 
Hapo ndipo wakati mwingine ninapomshangaa Mkuu wetu wa nchi.

Ni jambo lisilopingika kuwa hakuna asiyejua madhara ya kutoweka amani nchini, lakini ni lazima pia ifahamike kuwa tunda kubwa la amani ni haki.

Na wanaopaswa wa kwanza kutenda haki ni watawala wetu.

Sasa tujiulize je utawala wetu wa awamu ya 5 unajitahidi kutenda haki?

Jibu la swali hilo tunaweza kupata baada ya kutafakari matamshi haya michache yaliyotolewa na Mkuu wetu wa nchi siku za karibuni .

1. Alitamka hadharani kuwa anapiga marufuku shughuli za siasa za vyama vya upinzani hadi mwaka 2020, lakini hapo hapo akitoa ruksa ya chama chake cha CCM kuendelea kufanya shughuli za siasa bila wasiwasi wowote, je huko ni kutenda haki kwa nchi inayoendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi?

2.Ametamka hadharani kwenye kikao cha Mkutano Mkuu wa Chama chake cha CCM kule Dodoma majuzi kuwa JK wakati ule alipokuwa Mwenyekiti na wajumbe wa NEC wakiimba kuwa wana imani na mtu fulani, kama yeye ndiye angekuwa Mwenyekiti, nusu ya wale wajumbe 'wangepotea' Hivi kiongozi kutamka maneno ya aina hiyo hadharani yanayoonyesha kuwa hauko tayari kwa mtu yeyote kutofautiana nawe, hivyo hiyo ni demokrasia kweli? Na je hali kama hiyo ya kutokubali hata kidogo kupingwa kwa jambo lolote hata kama wanaokupinga wana hoja ya msingi, je huko nako ni kudumisha amani?

3 Utawala bora ni lazima uzingatie Power seperation ya mihimili 3 ya dola ambayo ni Executive, Legislature na Judiciary, sasa inapotokea wewe mhimili mmoja Executive 'kutamani' kuikalia kichwani mihimili ile mingine ya Legislature na Judiciary, je huko ni kutenda haki na kudumisha amani?

4. Hivi kuvitegemea vyombo vya dola kumdhibiti yeyote anayekupinga, hata kama huyo anayekupinga havunji sheria ya nchi kwa kuwa Ibara ya 18 ya Katiba ya nchi yetu inatamka wazi kuwa kila mtu yuko huru kutoa maoni yake, je huko nako ni kutenda haki na kudumisha amani?

Ni dhahiri basi kuwa huwezi kutenganisha kutenda HAKI na kudumisha AMANI.

Kwa hiyo kama Mkuu wetu wa nchi amedhamiria kweli kutoka ndani ya moyo wake kudumisha amani ya nchi, analazimika kutenda haki na kutofanya upendeleo na kutokandamiza kundi fulani la wananchi.

Watawala kutegemea vyombo vya dola kuwa ndiyo vitakavyodhibiti wananchi na hivyo kudumisha amani, hiyo amani 'artificial' ya aina hiyo haiwezi kudumu ndani ya nchi,.

Amani pekee inayoweza kudumu ndani ya nchi ni kwa watawala wetu kutenda haki kwa makundi yote ndani ya nchi bila ubaguzi wa aina yoyote.
 
RAIS John Magufuli amewataka Watanzania wasichezee amani kwa kuwa Tanzania ni nchi pekee iliyobakia kuwa kisiwa cha amani.

“Tusichezee amani. Tuidumishe amani yetu kwani kuna watu walijitoa mhanga kupigania amani hiyo na kuifikisha nchi hapa ilipo,” alisema Rais Magufuli mjini hapa jana alipohutubia maelfu ya wakazi wa Dodoma na Watanzania katika sherehe ya Siku ya Mashujaa.

Rais Magufuli aliyeshangiliwa na wananchi waliokuwa wakipunga bendera ndogo za Taifa baada ya kupanda jukwaani, alisema kuwa wakati tunaadhimisha Siku ya Mashujaa tukumbuke wapo watu walikubali roho zao zipotee.

Alitoa mfano wa waliopigania ukombozi wa nchi mbalimbali barani Afrika kama Msumbiji, Namibia, Angola, Comoro na Afrika Kusini. Wengine ni waliopigana vita ya nduli Iddi Amin wa Uganda mwaka 1977, wakati nduli alipovamia Tanzania na wakati wa Mapinduzi kisiwani Zanzibar mwaka 1964.

Aliwataja mashujaa wengine wa Taifa ambao hawawezi kusahaulika kwa mchango wao mkubwa katika ukombozi wa nchi kuwa ni Baba wa Taifa , Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Abeid Amaan Karume wa Zanzibar.

Alisema waasisi hao walijitahidi kuifikisha nchi hapa ilipo.

“Tanzania imekuwa na amani na utulivu kwa sababu wapo watu waliojitoa mhanga kuipigania. Tudumishe amani yetu. Hawa wenzetu waliotangulia, hawakujali dini zao na makabila yao. Walijitahidi kuwaunganisha Watanzania wote,” alisema Rais Magufuli na kuwataka Watanzania wasichezee amani na asitokee wa kuichafua kwani kila mmoja ana wajibu wa kuidumisha. Kwa upande wake, Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi aliwataka Watanzania kulinda umoja na amani ya nchi.

Aliwataka kuendelea kumuombea dua Rais Magufuli ili awe mwepesi katika kutekeleza yote anayodhamiria kwakuwa amepewa dhamana kubwa ya kuongoza Watanzania zaidi ya milioni 40.

“Tuache ushetani, tuache ubilisi, tushughulike na yale yanayotuhusu sisi wenyewe, watoto wetu na vizazi vyetu. Tudumishe utulivu na kupendana. Heri na amani haiji bila kupatikana usawa,” alisema na kuongeza kuwa Rais Magufuli amekuwa kiongozi wa watu, anayepigania watu wanaokosa haki, wanaoonewa na wanaofanyiwa fitna.

Alisema amani ni kitu muhimu sana hivyo Watanzania wafunge masikio wasisikie mabalaa na machafuko yanayotokea katika nchi jirani. Aliongeza kuwa, Mungu katujalia amani hivyo tuidumishe ili asitokee mtu kuiharibu.

“Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Huko nje maguu yanavunjika na yataendelea kuvunjika,” alionya Mwinyi. Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein alisema atashirikiana na Rais Magufuli kuimarisha amani ya Tanzania.

Alisema anafahamu uwezo, nia, ari, jitihada na kasi ya Rais Magufuli ya kuipeleka Tanzania kuwa nchi yenye matumaini na maendeleo makubwa.

Akitoa dua katika maadhimisho hayo kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), Kaimu Shehe wa mkoa wa Dodoma, Ahmed Said, alisema Watanzania wanathamini mchango mkubwa walioutoa mashujaa waliopigania nchi na kwamba mchango wao utaendelea kuthaminiwa.

Alisema umoja na amani havikushuka nchini kama mvua, bali wazee na askari walitoa jasho na kupoteza maisha kwa ajili ya nchi ndio waliosababisha viwepo.

Alisema Watanzania hawawezi kusahau waasisi walioongoza mapambano wakiwemo Mwalimu Julius Nyerere, Shehe Abeid Amaan Karume na Rashidi Kawawa.

“Tunamuomba Mungu aendelee kuilinda nchi yetu na kudumisha amani, utulivu na umoja uliopo,” alisema Shehe Said. Pia, Shehe Said aliwataka Watanzania waendelee kumuombea Rais Magufuli awe na moyo wa ujasiri, subira na afya njema ili aweze kuongoza nchi kama ilivyokusudiwa.

Aliomba Mungu awaepushie shari viongozi wanaomsaidia Rais Magufuli kuongoza Serikali. Shehe huyo aliomba Mungu ailinde Tanzania na Watanzania kwa ujumla na pia aubariki Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili uendelee kudumu.

Mchungaji Leonard Mtaita akifanya maombi kwa niaba ya Umoja wa Makanisa ya Kikristo (CCT), alisema waasisi wa Taifa wametoa mchango mkubwa katika kujenga na kudumisha amani.

Aliwataka Watanzania kudumisha upendo na amani kama njia ya kuwaenzi. Mtaita aliwahimiza Watanzania waendelee kumuombea Magufuli aendelee kuwa na afya njema, hekima na busara ili kuwatumikia Watanzania. Alimsifu Rais kwa kuwatumikia kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.

Padri Onesmo Wisi alifanya maombi kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), alisema Watanzania wanafurahia amani ambayo waasisi na askari wetu waliipigania. Aliwahimiza kuwa na umoja ili kulinda amani iliyopo na kujiepusha na uchochezi wa kisiasa, ambao mwisho wake ni vurugu.

Katika maadhimisho hayo, shughuli zilizofanyika ni pamoja na kuweka silaha za asili za mashujaa na maua kwenye mnara, ambapo Rais Magufuli aliweka mkuki na ngao na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange aliweka sime. Kiongozi wa Mabalozi nchini, Balozi Ambrosio Lukoki aliweka shada la maua.

Lukoki ni Balozi wa Angola nchini. Meya wa Dodoma, Jaffar Mwanyemba aliweka upinde na mshale na Mwenyekiti wa Tanzania Legion, Rashid Bakar Ngonji aliweka shoka.

Pia mizinga miwili ilipigwa katika sherehe hizo zilizopambwa na gwaride maalumu. Maelfu ya wakazi wa Dodoma walihudhuria sherehe hizo. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa sherehe za Siku ya Mashujaa kufanyika nje ya Dar es Salaam.

Chanzo Habari Leo

Maoni yangu

Watanzania tumuunge mkono Rais Magufuli kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake katika kuhakikisha amani utulivu vinaendelea kuwepo nchini, tusikubali kutumiwa na yeyote katika kuondoa utulivu tulionao iwe mwanasiasa au wanaotaka kutumia dini kama kigezo cha kuondoa utulivu tulia nao.

Vijana tuna nafasi kubwa ya kulinda nchi yetu, tuache kutumiwa na wanasiasa waroho wa madaraka wanaodhani bila yao kupata madaraka Tanzania haiwezi kupiga hatua na kupata maendeleo, wanaotaka kututumia vijana kama daraja la kufanikisha mambo yao, Watanzania tuache masihara ya kuvikebeshi na kuvifanyia istidhai vyombo vyeti vya ulinzi na usalama kwani vinafanya kazi kubwa ya kuhakikisha hali iliyo ya amani na utulivui inaendelea kuwepo.
Amani itaweza tu kudunishwa nchini iwapo watawala wetu wataamua kuendesha nchi kwa haki.....

Watawala wetu wanapaswa kufahamu kuwa amani haiwezi kudumishwa kwa matamko ya majukwaani bali kwa dhamira ya dhati ya watawala wetu kutoka ndani ya mioyo yao na matendo yao ya kutenda haki.
 
Magufuli Ndiye anayechezea amani Kwa Kuendeleza Siasa za Kinafiki, Kuziba wengine Kisiasa kwa Hila, for that Mh. Magufuli is as Evil as the Devil and he knows it. Anajua anachofanya Kukataza Mikutano ya Siasa Ni Unafiki Mkubwa Kwa Kuwa anajua CCM itafanya siasa kwa Mgongo wa Serikali. On other Issues Anajitahidi sana Lakini Hili La Hila na Unafiki Katika Kuua Uhuru wa Kisiasa Ni Mnafiki wa Kunuka. Hata angekuwa Baba yangu Mzazi Ningempinga! Hata wangekuwa UKAWA ndio wangeachwa Washinde Urais Wakafanya Uhuni Huu unaofanywa sasa kwa Maana Kuwa wakawafanyia Unyama huu CCM Pia Ningewapinga. Na Pia Mh. Magufuli alipokuwa Mbunge na Waziri alikuwa akipita Bila Kupigwa ila Kuna wakati alikiri alipata mtu aliyetaka Kumpinga, "Akaja tukaelewana akajitoa" Mwisho wa Kumnukuu, Je walielewanaje, so Magufuli sio Fisadi wa Pesa (Very clean on that) Ila Kwa Kutaka na kuinda Madaraka Kwa Njia ya Mkato na hila, Hapo hana Tofauti na Akina Mobutu Seseseko KUKU Nbendu WaZabanga.
 
Mimi nina wasiwasi sana kama Kweli Raisi Magufuli na chama chake cha CCM wanaitakia amani nch yetu. Wamezigeuza siasa za Tanzania kama ni uwanja wa mapambano, wakitumia kila namna kuhakikisha wanawakandamiza watu wa vyama vya upinzani. Wamefanikiwa sana katika kujenga mindset ndani ya Watanzania kwamba vyama vya upinzani ni maadui wa Tanzania, wasio na nia njema na Tanzania na wanaopasaswa kutukanwa, kupigwa, kudharirishwa, kufungwa na "kutwangwa" kwa kila namna. Sasa hivi hatuoni siasa tena nchini bali magenge ya uhuni tu kama ya wauza madawa ya kulevya yanayoshindania kutawala mitaa ya mji, gansterism.

Kwa hiyo kabla Raisi hajatuhutubia kuhusu kudumisha amani nchi, yeye na watu wake CCM wanapaswa kujiuliza ni jambo gani hasa katika nchi mbalimbali linalotowesha amani. Kisha wajitafakari ikiwa michezo ya kisiasa wanayofanya dhidi ya vyama vya upinzani ni kichocheo cha kuendeleza amani au kuitowesha.
 
Back
Top Bottom