Huyu ni waziri wake wa mambo ya ndani na wengine wanasema ni ndugu yake.
Lakini kila kukicha skendo na tuhuma mbali mbali zinazidi kumwandama huyu waziri kuanzia kuchukua mishahara bila kulipwa BOT kwa miaka 6 mpaka hii ya Lugumi enterprises, NIDA na mengineyo.
Kama mlipa kodi najiuliza kwa nini Waziri Kitwanga asikae pembeni mpaka ili kumrahisishia kazi magufuli ambaye spidi yake na kutotopenda logolongo sote tunaikubali? Hivi kama kweli kitwanga anamthamini Magufuli kwa nini asimfanyie wepesi mheshimiwa rais na kukaa pembeni?
na kama Charles Kitwanga hataki kukaa pembeni kwa nini Mhehsimiwa rais anendelea kumbemba waziri ambaye anaongoza wizara nyeti huku amekubikwa na kashfa mbabali mbali?
Kwa jinis ilivyo mheshimiwa rais akubali kuwa kwa sasa Waziri Charles Kitwanga ni liability kwake.