txyz
Member
- Apr 3, 2014
- 89
- 48
Awali ya yote nitumie fufsa hii kumpongeza Rais Magufuri kwa kazi nzuri anayoifanya ya kurudisha heshima ya urais na kurejesha uadilifu na uwajibikaji ingawa ni wa kulazimisha. Nasema wa kulazimisha kwani asilimia tisini kwa sasa ya watumishi wanafanya kazi kwa kumwogopa rais na si kutoka mioyoni mwao.
Ni wazi kuwa Magufuri kapatikana nje ya utashi wa ccm.Tulishuhudia jinsi wa msoga alivyokuwa kaegemea kwa baadhi ya wagombea na jinsi wafuasi wa mzee wa mvi walivyogomea zoezi la upigaji kura halmashauri kuu hali iliyosababisha mgombea mmoja kuenguliwa ili kubalance.
Pande zote mbili zilizosigishana na kuonesha upinzani mkubwa zilipoenguliwa,ndipo Mh Rais wetu kwa juhudi za mzee wa ukweli na uwazi alipoonekana kuifaa ccm akilinganishwa na wagombea wanawake na kijana wa kunyoa upara.
Bila shaka CCM ililazimika kuangalia nguvu na ushawishi wa ukawa vinginevyo leo tungekuwa tuna president wa ukawa.Na kama upinzani usingekuwa na nguvu,mzee wa mvi asingeenguliwa na ndiye anagekuwa rais.
Nihitimishe kwa kusema wakati tunatembea kifua mbele kwa kuwa na rais mchapakazi, mwadilifu na mcha Mungu.
Tujidai pia kwa kuwa na upinzani uliosababisha tukampata Magufuli na sifa zimrudie Mungu.