Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Baraza la kwanza kabisa la mawaziri lilikuwa na sura za kisomi, Wanasiasa kama Job Lusinde, Said Fundikira, Amil Jamal, Paul Bomani, Oscar Kambona, Tewa Said Tewa na Nsilo Swai, walikuwa ni wasomi, lakini kwa ujumla Tanganyika ya 1961/ 62 ilikuwa na wasomi wachache sana. Na kwa miaka mingi ya awamu ya Nyerere idadi ya wasomi ilikuwa ni ndogo sana. Hivyo upinzani wa kweli kwa maana ya changamoto kwa Mwalimu Nyerere hazikuwa ni nyingi. Ilikuwa rahisi kwa msomi mmoja mmoja kuweza kutafutiwa njia za kurudishwa kwenye mstari.
Lakini nchi inayoongozwa na John Magufuli ni tofauti kabisa na ile iliyoongozwa na Mwalimu Nyerere. Wasomi ni wengi sana, wanao uhuru mkubwa wa kutumia elimu zao. Watu wanazitambua haki zao na wanajua waende wapi ili waweze kusikika. Kwa kulitazama baraza la mawaziri la awamu ya tano kumejaa PHD na Masters, hicho pekee ni kipimo cha ugumu wa kazi ya rais Magufuli kwa sasa. Nadhani JPM ana kazi ngumu kuliko watangulizi wake, kwani serikali yake haidaiwi siasa, inadaiwa maendeleo, inadaiwa nidhamu kubwa ya kazi. Inadaiwa uwezo mkubwa wa kumobilize resources zote ziwe ni za ardhini, ziwe ni za vichwani mwa watu.
Pole sana Rais JPM unaongoza nchi yenye wasomi wenye uwezo wa kujenga hoja na wakaeleweka. Hauongozi nchi kama ile ya 1961/62, unawaongoza wajukuu na watoto wa wale wazee walioliunda baraza la kwanza la mawaziri. Ni mtihani mzito ulio mbele yako, lakini naamini Mungu anapoongoza kitu hakuna binadamu mwenye uwezo wa kuliharibu.