Magufuli adai anawindwa

Magufuli adai anawindwa

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713



John-Magufuli.jpg

Waziri John Magufuli


NA JOHN MADUHU, MWANZA

WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ameibuka na kusema kuwa anawindwa na mahasimu wake kwa kumbeza baada ya Mahakama Kuu kuwaachia huru watuhumiwa wa kesi ya kuvua samaki katika Ukanda wa Uchumi wa Tanzania.

Amesema watu hao wanaongozwa na ajenda za siri kisiasa na si wazalendo.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu jana, Dk. Magufuli alisema ameshangazwa na namna suala hilo linavyofanywa kisiasa zaidi, na kudai wapo baadhi ya watu wana malengo maalumu na kesi hiyo.

Alisema operesheni iliyofanyika ya kuwasaka wavuvi haramu waliokuwa wakivua samaki katika Ukanda wa Uchumi wa Tanzania katika Bahari ya Hindi, ilikuwa chini ya ushirikiano wa nchi za kusini mwa Afrika, ikiratibiwa na SADC na kuongozwa na Afrika Kusini.

“Nilipofanikiwa kukamata meli hii na wavuvi wake nilipongezwa, lakini leo nabezwa…, wakati nakamata nilikuwa Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, nilikuwa natimiza wajibu wangu kama msimamizi wa wizara,” alisema.

Alisema baada ya Wachina hao kukamatwa, suala lao lilipelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kisha kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kama taratibu zilivyo na watuhumiwa kufikishwa mahakamani.

“Awali walipofikishwa mahakamani walihukumiwa miaka 23 na mahakama iliagiza meli yao itaifishwe. Sikuwashtaki kama Magufuli, ni Jamhuri ndiyo iliyoshtaki na kushinda.

“Baada ya Wachina hao kuhukumiwa kutokana na kazi nzuri niliyoifanya, ambayo hata ninyi waandishi wa habari hamkunipongeza, ilikuwa kimya, leo hii watu wanaibuka na kuelekeza lawama kwangu baada ya Wachina kuachiwa huru na mahakama, mara Magufuli afukuzwe mara hivi, hizo ni siasa,” alisema.

Alisema kuwa awali Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipopeleka kesi mahakamani Wachina hao walipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 23, lakini hakuonekana mbaya.

Akizungumzia meli ya MV Tawaliq 1, alisema ilitoka chini ya Wizara ya Uvuvi na kuwa katika uangalizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Alisema ikiwa chini ya uangalizi huo, iliibwa vifaa muhimu kabla ya kuzama, lakini hakuna ambaye amewahi kumuuliza Waziri wa Mambo ya Ndani kuhusu suala hilo.

“Mie kwa sasa si Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, nilitimiza wajibu wangu, na sasa hivi niko Wizara ya Ujenzi nikiendelea kuwatumikia Watanzania, malumbano ya kisiasa yasiyo na tija hayana nafasi kwangu, sitaki kuzungumza kwa undani hukumu ya kuachiwa hawa, watafuteni viongozi wa mahakama au ofisi ya AG na si Magufuli,” alisema.

Wiki iliyopita, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwaachia huru Wachina wa ‘samaki wa Magufuli’ na kuamuru Jamhuri iwarejeshee vitu vyao, ikiwamo meli ya Tawaliq 1.

Wachina hao waliachiwa kwa mara ya pili, kwani mara ya kwanza waliachiwa na Mahakama ya Rufaa Machi 28, mwaka huu, kabla ya kukamatwa tena na kushtakiwa upya kwa mashtaka hayo hayo yaliyofutwa.

Washtakiwa hao ni nahodha wa meli, Hsu Chin Tai na wakala wa meli hiyo ya Tawaliq 1, Zhao Hanquing, waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uvuvi haramu katika Ukanda wa Uchumi wa Tanzania.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Prosper Mwangamila, aliwasilisha maombi ya kuifuta kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Isaya Harufani.

“Mheshimiwa hakimu, Jamhuri tunaifahamisha mahakama kwamba hatuna haja ya kuendelea na kesi dhidi ya washtakiwa, maombi yetu tunawasilisha chini ya kifungu cha sheria namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) ya mwaka 2002,” alidai Mwangamila na kuwasilisha.

Wakili wa washtakiwa, Kapteni Ibrahimu Bendera, alikubaliana na maombi hayo na kuiomba mahakama iwarudishie hati zao za kusafiria, meli iliyokamatwa pamoja na samaki waliokuwamo ikiwezekana.

CHANZO:
Mtanzania
 
Duh! Hivi ni lini serikali ya Tanganyika itakuja kushinda kesi yenye maslahi ya taifa? Yaani kila mwizi na fisadi wa fedha na maliasili ya nchi lazima mwisho aibuke staa wa filamu?
 
Suala Kama wizara na system ya Nchi tunatakiwa kujua ni Kosa gani lilipelekea Watu tuliowakuta wakiiba maliasili zetu wametushinda mbele ya sheria...

1...Tatizo kubwa kwenye Nchi yetu ni kuwashirikisha wataalamu na kuchukua utaalamu wao. Wakati hii meli inakamatwa ni kweli ilikuwa kwetu ila Watu walioenda kuendesha hiyo operesheni hawakuwa na ujuzi na sheria na ujuzi wa meli...
kwanini Nasema hivyo....Kosa kubwa baada ya kukamata meli walitegemea captain yuleyule aendeshe meli...... What happen captain akaendesha li meli lake Mpaka kwenye maji ya kimataifa then akapiga simu kwao kureport tukio so system ikarekodi wakati wanatatekwa walikuwa kwenye maji/bahari ya kimataifa na ndio ushaidi Muhimu mahakamani...wakati huo record za nyuma ameshazifuta... Vijana wetu wao wanashangilia na kumtaarifu mhe. Pombe...celebration......where is media..... Tuoshe jina.. Owk...

Wataalam walipofika na kuomba report ya movement ya meli na ni wapi imekamatiwa ....waliishauri serikali wawaachie Hawa wachina because there is technical error.... Hahaaaa nani akubali wakati tunataka kuosha jina....
captain Bendera ni mtaalam aw sheria za majini Tz wizara ilipoomba ushauri ukawaambia ache ni hii kesi hawakumsikiliza.... Wachina wakamchukua huyo huyo mtaalamu wetu akawa wakili wao ....na Majibu ndio Kama hayo Mhe. Pombe...mngemsikiliza Captain Bendera ungeisaidia Nchi yako that is leadership.... Listening ability...

Nawakilisha....
 
Nani amuwinde huyu mkurupukaji?? Kila siku si anashinda kwenye vyombo vya habari akimsifia mwanaume mwenzie? (kikwete) amwambie akamnasue kwenye hii shutuma
 
Ukweli hapa ni kwamba tuliibiwa ila tatizo ni kuto washirikisha wataalamu from day one.
Actually na rushwa pia.
 
Nani amuwinde huyu mkurupukaji?? Kila siku si anashinda kwenye vyombo vya habari akimsifia mwanaume mwenzie? (kikwete) amwambie akamnasue kwenye hii shutuma
Wewe tangu nyumba yenu iungue moto na wewe ukiwepo ukatoka kwa bahati nasibu akili zako zilisharuka ndiyo maana unaandika ubwabwa tu.
 
Ni kipi wachagiaji hamuelewi? Aya ya pili toka mwisho inasema wakili wa serikali kapeleka hati ya kufuta kesi sababu eti serikali haioni sababu ya kuendelea nayo. Na pia mwandishi anasema wakili wa wachina akakubali ila kwa sharti warejeshewe hati za kusafiria na meli. Mahakama ikaridhia na kuhitinisha kesi.Sasa labda tujiulize Magufuli anaingiaje hapo? Cha msingi ni kuhoji DPP na mwanasheria mkuu sababu za kufuta kesi. Hawa ndio wameingiza nchi kwenye kadhia hii. Lakin pia nina hisia kuwa magufuli anaposema kunasababu za kisiasa labda kweli. Maana ni ajabu kesi ulishinda rufaa ikakatwa haijasikilizwa unajitoa!!! Au ndio moja ya condition za kupigwa tafu bajeti??!! au yule mkubwa aliyemuokoa mwanaye kwa mikataba na huu uliingia? Napata tabu kuelewa sababu za msingi za kujitoa kwenye kesi.
 
Nani amuwinde huyu mkurupukaji?? Kila siku si anashinda kwenye vyombo vya habari akimsifia mwanaume mwenzie? (kikwete) amwambie akamnasue kwenye hii shutuma

Katika Kesi hii Magufuri hana kosa maana waliokamatwa ni wezi, kwa maana hiyo alitimiza wajibu wake. Tatizo liko kwenye Sheria, maana Sheria ikitumika vibaya inaondoa haki. Watanzania tujifunze na kuwaheshi viongozi wanaoonyesha uzalendo, tuache kuwabeza.
 
Rafu zimeanza ndani ya chama cha kijani kuelekea uchaguzi mkuu 2015,nani awe rais nani akose
Lkn pia unabii wa askofu kakobe usitupwe nyuma,Mungu anawachafulia lugha kama vile mnara wa babeli.
Nakuunga mkono Magufuli.Mahakama iliyowahukumu kifungo ni ya serikali yako sikivu,na iliyowafutia kifungo ni ile ile
ya serikali yako sikivu,wewe kaza buti tengeneza kivuko magogoni na daraja la kigamboni,watanzania wavuke wachape kazi.
 
hii sinema, magufuli anawatisha sana wanaousaka urais, baada ya kadhia hii wapambe wa wagombea wameona ni kete ya kumfuta magufuli ktk orodha ya wagombea.ndiyo maana wanamwita mkurupukaji na majina mengine yasiyo na staha lkn kimsingi magufuli hajawahi pewa post akaitumia kujitajirisha kama huyo bosi wenu mamvi, la sivyo hapo wizara ya ujenzi ka shfa zingekuwa kibao.
 
Kazi ipo mwaka huu na mwaka kesho, ccm mpaka kumpata mgombea urais mtakuwa mmetoana meno, magufuli ni mchapa kazi sana na alitimiza wajibu wake sasa sijui alie faya lobbying kwa ag,dpp na rais mpaka kesi imefutwa anakusudia nini? Hii haitoshi kumchafua magufuli na kwa taarifa yenu ccm hakuna mgombea atakae ng'ara kama magufuli.wengne teona ni wanafik, opportunist na wasi weza kufanya maamz. Mkitakakuju leteni mgombea ovyomtakiona ch a moto
 
Kwa ujinga huu lazima awindwe nchi yenyewe masikini alafu yeye ndo anaongoza kuzidi kuiingiza nchi kwenye lindi la umasikini kwa sababu ya mahaba yake ya kisiasa.sasa mahakama imezidi kumvua nguo hadharani ,hii ni mara ya pili kwa mwaka huu baada ya ile ya kuvunja manyumba za watu brbr ya Morogoro,Kwa utumbo huu hapa chini nadhani muungwana ukivukwa na nguo chutama badala kuendelea kusimama wima kujidhalilisha zaidi.

Alisema operesheni iliyofanyika ya kuwasaka wavuvi haramu waliokuwa wakivua samaki katika Ukanda wa Uchumi wa Tanzania katika Bahari ya Hindi, ilikuwa chini ya ushirikiano wa nchi za kusini mwa Afrika, ikiratibiwa na SADC na kuongozwa na Afrika Kusini.
"Nilipofanikiwa kukamata meli hii na wavuvi wake nilipongezwa, lakini leo nabezwa…, wakati nakamata nilikuwa Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, nilikuwa natimiza wajibu wangu kama msimamizi wa wizara," alisema

1-Kama iliratibiwa na Afrika ya Kusini mbona hawakuitwa kutoa ushahidi?
2-Waliokupongeza bwana Mapadlok walikuwa mataahira/mateja wenzio ambao huongozwa na mahaba ya kisiasa.
3-Wenne akili zao wamekuja kukupa facts bado hutaki kuelewa unawaita maadui kisiasa.poor!

4-Hizo fedha zilizopotea zingesaidia waTz wenye shida basics ila CCM hawaoni ubaya kwani ndo lengo lao tuzidi kuwa wajinga tuwachague.Hongera kwa hilo mapadlock.
 
hii sinema, magufuli anawatisha sana wanaousaka urais, baada ya kadhia hii wapambe wa wagombea wameona ni kete ya kumfuta magufuli ktk orodha ya wagombea.ndiyo maana wanamwita mkurupukaji na majina mengine yasiyo na staha lkn kimsingi magufuli hajawahi pewa post akaitumia kujitajirisha kama huyo bosi wenu mamvi, la sivyo hapo wizara ya ujenzi ka shfa zingekuwa kibao.
ile nyumba ya ubungo aliyompa hawara yake hiyo si matumizi mabaya ya madaraka?Au na wewe unajitia upofu au anapoingiza taifa ktk hasara kubwa kama hii tumwiteje!Kama nae anataka kugombea urais akafie mbali pamoja na wewe mpambe wake as both of you are the best loosers!
 
ile nyumba ya ubungo aliyompa hawara yake hiyo si matumizi mabaya ya madaraka?Au na wewe unajitia upofu au anapoingiza taifa ktk hasara kubwa kama hii tumwiteje!Kama nae anataka kugombea urais akafie mbali pamoja na wewe mpambe wake as both of you are the best loosers!
siwezi mtetea sana magufuli kuhusu nyumba ya ubungo lkn baraza la mawaziri lilishaamua nyumba ziuzwe, mtu anfanya kazi serkalini kwa nini asiuziwe, hata hivyo punguza munkali magufuli hajasema kama anagombea usku mwema.
 
Tunataka kujua kiasi cha fedha kilichotumika kuwakamata hawa wavuvi haramu,
Pili kiasi cha fedha kilichotumika kuendesha kesi yao hadi mwishowe wakaonekana hawana hatia, tatu kiasi cha fedha watakachodai kama fidia ya meli yao, samaki zao, muda waliopoteza nk (rough figure) Halafu fedha hizo zigawanye kwa watanzania million 45 tuangalie kila mmoja anadaiwa kiasi gani? na fedha hizo zingetosha kuwalipa waalimu wa primary na secondary wangapi kwa muda gani?

Theni tujadili kama watanzania...kama nikumtosa magufuli tumtose tuu asianze kulialia hapa.
 
Back
Top Bottom