MAGU AKIUNGANA NA HOJA ZA.............!!!!!!!!!!!

muda wa ukombozi

Senior Member
Jun 28, 2013
129
118
79af7b69b0c66058f1e144d33ca554ed.jpg
Wanasema kwamba ni ngumu sana kuwa ndani ya gari alafu gari hilo likaharibika na msaada pekee wa gari hilo ni kusukumwa, haitawezekana gari hilo kusukumwa na abiria walioko ndani ya gari.

Hapa inamaanisha kwamba lazima wasukumaji watoke nje ya gari ili waweze kusukuma.

Maana yake unaweza ukawa ndani ya serikali iliyooza kwa rushwa, unyonyaji wa wazi kwa wananchi wake, viongozi wa serikali hiyo walafi na waroho na ndio wengi alafu akatokea mtu ndani ya serikali hiyo akaanza kuhoji na kuwaacha uchi wenye tabia za kizandiki namna hiyo?

Sasa mimi natangaza kuwa nipo upande wa Rais wetu DK. JPM, kwenye ili suala la makinikia kabisa, ingawa kifkra sijui kama yupo ndani ya gari lililoaribika au nje, au ndio anajiandaa kushuka kwenye gari hilo au mwili upo ndani alafu akili ipo nje ya gari hilo.

Tokea mwaka 1998 hadi hii leo walioko nje ya gari wanaliona gari bovu likitembea kwa mwendo wa kusuasua, walijaribu kutoa ushauri hili gari liwe Salama ikashindikana, wengine wakafunguliwa na kesi mahakamani kwamba wanapotosha umma, wachochezi, wengine walifukuzwa bungeni kwa utovu wa nidhamu kwa kusema tu gari mlilopanda wenzetu bovu!!!

Ndio, ilikuwa hivyo waliopanda gari hawakutaka bughudha waliendelea kuwa kwenye gari ambalo ni bovu halina spidi kabisa, linatoa moshi mchafu, linabughudhi kwa harufu mbaya kwa wanaotembea kwa mguu na walioko nje ya gari hilo, kibaya zaidi gari halina spidi kabisa.

Ndani ya gari kuna kiyoyozi kikali na manukato sio ya nchi hii, kuna mavyakula ya kila aina na hii inasababisha walioko ndani wasitake safari ile ifike haraka kabisa, mwendo ule wao wanauona mzuri na hata tuliopo nje tunawaona walivyonona wakishuka kuchimba dawa kabla ya kupanda tena.

Sasa kule ndani kimenuka sijui ni nini? Mi najiuliza labda matokeo ya mavyakula na mapochopocho ya ndani gari au ubovu wa gari umezidi?

Kuhusu kunuka Mhhhhh!!!!!!! Sina ushahidi kabisa ila nahisi kuna ubovu dereva kaona maana kashuka dereva mwenyewe na mafundi kawaita waliopo kwenye gari hilo ili walirekebishe, sisi wapita njia, yetu macho tu ingawa tungependa safari hii waitwe mafundi wa nje waje kusaidia labda safari itakuwa inaspidi Kubwa na salama.

Tatizo kubwa hapa ni spidi ya gari na inaonekana wazi mafundi wa ndani wanasuasua kwa maslahi yao binafsi, siku ambayo dereva ataruhusu mafundi wa nje ya gari wamsaidie kutengeneza naamini atafukuza timu yote na abiria wasio na msaada kwenye gari hilo.

"ITAELEWEKA TU"

muda wa ukombozi
 
Back
Top Bottom