Magesa Mulongo umewatukana Wakerewe, waombe radhi

kkarumekenge

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
1,708
1,026
Yule aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, anayetamba yupo karibu sana na JK, amewatukana Wakerewe na uongozi wote wa wilaya. Wiki hii Mulongo ambaye amehamishiwa mkoani Mwanza, alikuwa Ukerewe. Akasema hajawahi kuona watu washamba kama Wakerewe na kwamba kama hali ikiendelea hivyo Ukerewe itatawaliwa kijeshi. Hakuishia hapo aliamuru diwani mmoja awekwe ndani.

Kwao Mulongo ni shamba pengine kuliko sehemu yoyote Tanzania. Anatoka Wilaya masikini kuliko zote, Bunda, sehemu iitwayo Karukekera. Shamba kabisa.Haina maji, umeme nk. Shamba kabisa.

Wakerewe walivyo "washamba" walimjibu tu "kishamba"; "umetuchokoza!" Hoja hapa si Wakerewe,bali ni kwanini viongozi wa Tanzania wameanza kutukana watu hasa hawa watokao mkoani Mara? Kwanini siku hizi kiongozi anaweza kutukana watu na kuachwa hivi hivi bila kuchukuliwa hatua?
 
Mulongo alisema ikibidi atazuia hata fedha ya maendeleo kwa ajili ya wilaya ya Ukerewe. Huyu amekengeuka, ingawa sishangai sana kuona viongozi watokao mkoa wa wakitukana watu ambao ndio waajiri wao. Maskini anaona atafia kwenye Ukuu wa mkoa. Ukweli kawakosea adabu Wakerewe, ila kama walivyomjibu, "kawachokoza!"
 
Hata Kwimba alitukana na isitoshe alishundwa ARUSHA je atapaweza jiji la pili tz kama alishindwa jiji la Tatu tz huyu aende kwao karukekere
 
Yule aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, anayetamba yupo karibu sana na JK, amewatukana Wakerewe na uongozi wote wa wilaya. Wiki hii Mulongo ambaye amehamishiwa mkoani Mwanza, alikuwa Ukerewe. Akasema hajawahi kuona watu washamba kama Wakerewe na kwamba kama hali ikiendelea hivyo Ukerewe itatawaliwa kijeshi. Hakuishia hapo aliamuru diwani mmoja awekwe ndani.
Kwao Mulongo ni shamba pengine kuliko sehemu yoyote Tanzania. Anatoka Wilaya maskini kuliko zote, Bunda, sehemu iitwayo Karukekera. Shamba kabisa.Haina maji, umeme nk. Shamba kabisa.
Wakerewe walivyo "washamba" walimjibu tu "kishamba"; "umetuchokoza!" Hoja hapa si Wakerewe,bali ni kwa nini viongozi wa Tanzania wameanza kutukana watu hasa hawa watokao mkoani Mara? Kwa nini siku hizi kiongozi anaweza kutukana watu na kuachwa hivi hivi bila kuchukuliwa hatua?

Wakerewe wakamshitaki kwa binamu zao Wakara wamuloge Mulongo; Wakara si wana uwezo wa kumfanya mtu akajitupa ziwani hivi hivi!!
 
Mbona mzee wa upako kawatukana jana wakristo wote wasioenda kanisani ni mafalla, hamkuliona sasa kuitwa washamba mnatoa mimacho, mwacheni Mulongo afanye kazi.
 
magufuli pia aliwahi kuwatukana wakazi wa kigamboni,"asiyeweza kulipa nauli ya ferry, apige mbizi baharini" teh! teh!
 
Wakerewe wakamshitaki kwa binamu zao Wakara wamuloge Mulongo; Wakara si wana uwezo wa kumfanya mtu akajitupa ziwani hivi hivi!!

We mwache tu, si hapo anaishi karibu na ziwa? wakara watamtengeneza ajipeleke yeye mwenyewe ziwani halafu ghafla atazolewa na mamba! si amewachokoza?
 
Mnapenda maneno ya kinafki kama walivyoviongozi wengi wa kiafrika. Mukiambiwa ukweli mumetukanwa
 
Umekosea kidogo atokako. Anatoka wilaya ya Bunda, tarafa ya Nansimo, kata ya Igundu, kijijji ni Mchigondo.
 
Mie siku hizi nimeacha kuamini mikwara ya members wa JF

Nasubiri nione/nisikie wakerewe mmefanya mambo kwa vitendo

the ball is in your court
 
Huyu jamaa sijui nani anamkingia kifua. Mimi nawashauri Wahe. madiwani wote wa Mkoa wa Mwanza muungane wote mumkatae. Hata kwenye vikao anavyoviitisha musiende na yeye atashika adabu. Kila mtu anahitaji heshima yake hata kama ni mwendawazimu.
 
We mwache tu, si hapo anaishi karibu na ziwa? wakara watamtengeneza ajipeleke yeye mwenyewe ziwani halafu ghafla atazolewa na mamba! si amewachokoza?

Zamani nilikuwa nasikia viongozi walikuwa wanafanyiziwa hadi asubuhi wanaamka wanajikuta uchi huku wakiwa juu ya mti, hiyo medicine siku hizi imewaishia hiyo kanda?
 
Kwa nini alisema hivo. Sababu plz

Kuropoka tu bila sababu. Alidhani ndo CCM itarudisha kiti cha ubunge Ukerewe. Ukweli ni kwamba kwa domo kama hilo, CCM wasahau jimbo la Ukerewe, ni kama alikwenda kugawa jimbo. Wakerewe na Wahaya ni makabila ya ajabu sana kwa msimamo. Kwa vile kawatukana, watampa majibu. Amuulize Getrude Mongella aliyesema huwa akiwakojea (kuwashinda) wanaume. Huko inakodaiwa anatoka ina maana ni Mjita na hawa ndo mafundi wa matusi, mikogo, majisifu na kujikweza nchini.
 
Huyu ni kiongozi....sidhani kama aliropoka tu. Mmejiuliza Aliona nini mpaka akawaita washamba?
 
Back
Top Bottom