Magendo inayoendelea Mbweni, Boko na Kunduchi, serikali imejipanga vipi na Corona? Boadaboda ndio wasambazaji bidhaa za Dubai

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
wanaJF,

Kila mara maeneo ya Boko majira ya saa mbili hadi saa tatu, nakutana na bodaboda kama kumi hivi zikikimbia mwendo mbaya wa hatari, zikiwa zimebeba mafuta, batery , sukari, mchele ulioisha muda wake, najiuliza haya magunia, viroba vya sukari hivi wenye corona hawawezi kugusa hii kitu na bodaboda wakasambaza kuanzia mwaloni hadi uswahilini.

Hivi polisi wamejipangaje kukabili bodaboda hawa? katika kitu polisi wamefeli ni kuwaondoa hawa bodaboda wakati wanajua vyanzo vyao kuwa ni BunjuB na Bunju A kuna vijana wataalamu wa kuvusha magendo.

Pia polisi imefeli kukagu mabasi yanayotoka mbweni kwani kuna baadhi huwa bidhaa inafichwa kwenye siti za nyuma.
 
Hata wewe ni serikali! unamsubiria nani aje achukue hatua?
Hivi kwanini wa Tanzania kila kitu mnaona kama wewe huhusiki ila serikali ndo inahusika?

nyie ndo mnajenga nyumba mabondeni afu kutwa kulaumu serikali pale mnapoanza kufa kama kuku na mafurko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Polisi mbona wanajua na wanapambana nao sana kuna siku nilikua Mbweni mida ya mchana tu polisi na hao jamaa walileteana vurugu mpaka mabomu ya machozi yakapigwa, ilikua mwaka jana mwanzoni. Labdi siku hizi iwe wamewaacha wafanye wanavyotaka ila wanajua
 
Mkuu asante Kwa tarifa, ni vyema kutoa tarifa Kwa kila mtu aonapo nchi yake ikiibiwa, sio vizuri kuishia kuponda tu pindi TRA inaposhindwa kufikia malengo yake ya ukusanyaji Kodi

Nchi hii ni yetu sote, tunawajibu wa kuijenga wote, tukishindwa tumeshindwa Sisi sote, hapa namaanisha, hata aje Raisi mzalendo kiasi gani kama Sisi raia hatutaisaidia Serikali yake hataweza na Serikali itashindwa tu
 
Nchi ni yetu sote katika kuijenga,ila katika kuibomoa na kunufaika na ujenzi wetu sote,ni wachache wananufaika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boko mbali sana hapo k--- tu Kuna sehemu watu wanashusha mzigo na wazee wanaimba na wanapewa Chao, Kuna wakati nliwahi chkua video ilikuwa usiku ah nkaona nisijifanye kimbelembele
Cha ajabu Kuna jirani mmja kila akiripoti wazee wakija wanadakishwa mpaka ye mwenyewe kachoka
Kaamua kuwaacha watu wapambane wenyewe

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hata wewe ni serikali! unamsubiria nani aje achukue hatua?
Hivi kwanini wa Tanzania kila kitu mnaona kama wewe huhusiki ila serikali ndo inahusika?

nyie ndo mnajenga nyumba mabondeni afu kutwa kulaumu serikali pale mnapoanza kufa kama kuku na mafurko

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama wewe uhusiki si unyamaze tu? Wanaohusika watimize wajibu wao ndio maana nchi inakuwa na serikali.

Kuna njia nyingi za kutoa taarifa za uovu uliopo kwenye jamii, na hii pia ni moja wapo, huenda naye alikuwa Muhusika na sasa ameamua kuokoka lakini roho inamsuta kuona wengine wanalishwa mchele mmbovu.
 
Huwa polisi wanajua na wanakuwa wamepewa chao kijana tuliza boli
wanaJF,

Kila mara maeneo ya boko majira ya saa mbili hadi saa tatu, nakutana na bodaboda kama kumi hivi zikikimbia mwendo mbaya wa hatari, zikiwa zimebeba mafuta, batery , sukari, mchele ulioisha muda wake, najiuliza haya magunia, viroba vya sukari hivi wenye corona hawawezi kugusa hii kitu na bodaboda wakasambaza kuanzia mwaloni hadi uswahilini.

Back
Top Bottom