Magari Yasiyo Toyota

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,421
3,287
Wakuu habarini

Kwanza niwape pole na Majukumu,

Naomba kujua kwa wataalamu wa Magari kuhusu Aina za Magari toka kampuni tofauti na toyota ambazo zipo miaka mingi mfano Volkswagen, Honda, Nissan, Mazda, Ford, Benz, Suzuki nk. Je magari yao ni mabovu, hayaaminiki au hayana spea hapa Tanzania?

Kwanini Toyota pamoja na kuwa gari zao ni za gereji kila siku kwa sababu ya vipuri feki bado zinauza kwa soko la Tanzania.
Je ni kwanini kampuni nyingine hazifurukuti au n mtazamo wa Watanzania tu?

Naomba nipatiwe ufafanuzi.
 
Toyota ni kampuni ya gari rahisi ndio sababu kubwa kupenya nchi nyingi ,Gari za Europe na America ni ngumu sana kuzidi toyota
Mkuu sasa hawa wenye gari mfano volkswagen maana zpo mtaani kwa wingi huwa wanapataje vipur na mafundi maana nijuavyo mafundi nao wako kitoyotatoyota.
 
ni kukariri tuu utakosaje spare ya gari dunia ya sasa..,kuna pick up hizi Ford bantam rocam engine ni vigumu sana sana na vina nguvu na balance na speed...haushi shindi garage kama toyota hilux...na ukatulia na Mercedes 180 au 200, 2013 model confortable ipo mercedes ukiweza kudondosha matairi yote manne yawe juu katika bara bara au nje barabara ukipona unapewa Zawadi hiyo itabingilika mara kadhaa lakini huko bondeni itakaa kama kawaida sijui waliweka nini hawa watu...na ndio yenye kona kali nadhani kuriko gari nyingi sana....
 
Wakuu habarini

Kwanza niwape pole na Majukumu,

Naomba kujua kwa wataalamu wa Magari kuhusu Aina za Magari toka kampuni tofauti na toyota ambazo zipo miaka mingi mfano Volkswagen, Honda, Nissan, Mazda, Ford, Benz, Suzuki nk. Je magari yao ni mabovu, hayaaminiki au hayana spea hapa Tanzania?
Kwanini Toyota pamoja na kuwa gari zao ni za gereji kila siku kwa sababu ya spare parts feki bado zinauza kwa soko la Tanzania.
Je ni kwanini kampuni nyingine hazifurukuti au n mtazamo wa Watanzania tu?
Naomba nipatiwe ufafanuzi.

Kuna sababu nyingi. Kwanza, ni rahisi saana kununua magari ya Asia, hasa Japan kwa sababu yanatengenezwa kwa wingi saana huko, na sheria lazo hasa za bima zinawabana wale wenye magari mazee. Hivyo wanalazimika kuyauza kwa bei ya chini kiasi kwamba watu wengi wa Afrika wanaweza kuyanunua.

Pili, gari za Japan kama Toyota ni ngumu saana, tofauti na unavyofikiria. Gari nyingi unazoziona Tanzania leo zilishasitishwa uzalishaji wake karibu miaka 10 na zaidi. Mfano, Altezza model ya mwisho ilizalishwa mwaka 2005, more than 10 years ago, ila zinaweza kuvumilia kutumika kwenye hali ngumu, na spare parts fake.

Gari za Ulaya ni ngumu pia, hasa gari za Ujerumani mf BMW, Mercedes na Audi na VW. Ni kati ya gari zinazotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu. Tatizo lake ni kwamba ziko very sophisticated (za kisasa zaidi) siku nyingi ukilinganisha na gari tulizozoea, sasa kwa maisha ya mafundi wa kubahatisha na spare parts fake inakua vigumu saana kuzitumia kwa mazingira yetu. Ndio maana unaona watu wanaziogopa.

Vile vile spare parts zinaonekana ni ghalama kidogo sababu wazalishaji wa spare fake ni wanabanwa saana kuziingiza Ulaya na Marekani ambako gari za Ulaya zinatumika zaidi, so mwisho wa siku soko la bidhaa zao linakua dogo kulinganisha na magari ya Japan.

So, hitimisho langu ni kwamba, most Toyotas and other Japanese cars ni very reliable, and less complex to maintain kwenye mazingira magumu kama Africa. European cars are very well made, quite a number of them sio very reliable hasa kwa mazingira magumu kama Afrika, maana gari hizo zina mifumo complex ambayo inabidi ilindwe na kutunzwa vyema.
 
Mi nina LDV CONVOY, ipo poa shida vifaa kupatikana, mwenye kuelewa ama kuuza vifaa hivi pse ni inbox nitakuwa mteja wako, ushauri pia nakaribisha
 
Msaada jaman,gari inayouzwa 1800usd Japan je kwa gharama za bandarin zinaweza kuwa sh.ngapi?
 
Napenda sana benz old model...
Zanipa mzuka
4c71514aad44c5286d69bb3f700e35c0.jpg
 
Iko pouwa ninamilizi toka 2011. Mwanzoni spare zilikuwa shida but kwa sasa hata mbeya unapata. Ni gari nzuri kwa muonekano, inanafasi kumbwa, iko juu na ni all weather unatinga nayo.
Hivi zipo za four wheel?
 
Nadhani watu wanakimbilia Gari za Kijapan kwa sababu wa upatikanaji na urahisi wa spare, mfano unapoenda dukani kununua spare za Kijapani unapata grade A, B mpaka original, lakini kwa gari kama BMW unapata genuine tu tena ziko Expensive kukingana na maisha yetu ya Kitanzania

Pili kwa nchi zilizoendelea, Car dealers wanaweza kukukopesha gari na ukalilipia kwa say miaka miatatu, lakini kwa Tanzania watu wananunua magari kwa cash, au mtu anakopa bank na ndio aende kununua garimiwa cash, sasa hapo lazima ununue gari za bei rahisi na zenye kurekebishika kirahisi
 
Gari za kijapan ukiitunza wala siyo rahisi kuharibika pia (inategemea na aina ya gari). Ila kuna gari za Ulaya kama BMW Xseries hata ukiangalia reviews za watu wa Uaya na marekani wanakwambia ni gari ambazo lazima baada ya muda fulani uonane sana na fundi. Na marekebisho yake ni ghali. Na mjapan pia ana gari amabazo ni ghali na nzuri vilevike kuliko hata za Ulaya. Inategemea tu tunaongea kutoka upande upi hasa. Gari kama rav 4 , Subaru na Suzuki ni maarufu sana hata Ulaya


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kukariri nina bmw 3 series walaaa cna mpango na toyota zao, nikitoka vw tiguan aah mjerumani acha bana
Mkuu nataka kumuomba msamaha wife kwa BMW X3 imekaaje? Wese, vipuri na mafundi?
 
Back
Top Bottom