Mafuta ya kula nayo bei juu

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,942
428
Utafiti uliofanyika katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam umeonyesha kuwa lita moja ya kiungo hicho cha chakula inauzwa kati ya Sh2,800 hadi Sh3,000 kutoka Sh2,500 ya awali.

Dar es Salaam. Wakati Watanzania wakiendelea kuumia na bei ya juu ya sukari, sasa watalazimika kutoboa zaidi mifuko yao kununua mafuta ya kupikia.

Wafanyabiashara walieleza kuwa wananchi wanashtuka bei hiyo sasa, lakini ilianza kupanda taratibu tangu Machi wakituhumu kuwa hali hiyo imesababishwa na hatua ya Serikali kuzuia mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi.

Serikali imekana madai hayo ikieleza kuwa zuio lolote la bidhaa ni lazima litangazwe wazi.

Mfanyabiashara wa bidhaa za jumla Manzese, Andrea Uiso alisema katoni ya mafuta ya Korie ya lita tatu inauzwa kati ya Sh 49,000 hadi Sh50,000 kutoka kati ya Sh37,000 hadi 42,000 ya awali.

Cosmas Laswai, muuza duka la rejareja Buguruni Rozana alisema sasa wanalazimika kuuza Sh2,800 kwa lita moja baada ya kununua mafuta hayo kwa bei ya jumla ya Sh51,000 ili kufidia hasara.

“Nilipowauliza sababu ni nini wenye maduka ya jumla walinijibu kuwa baadhi ya kampuni wanazochukua bidhaa hii walikuwa wanasafisha visima vyao vya mafuta ndiyo maana kitu kama hiki kimetokea,” alisema Laswai.

Laswai alishauri Serikali kuhakikisha inazuia mfumuko wa bei ili kukabiliana na hali hiyo, kwani wao hawapendi kuuza bidhaa kwa bei ya juu, lakini mazingira yamelazimisha.

Mfanyabiashara wa chips Ilala Bungoni, John Samwel alisema kupanda kwa bidhaa hiyo kumewathiri kibiashara na kwamba hali ikiendelea hivyo watalazimika kupandisha bei ya chips kavu kutoka Sh1,500 hadi Sh2,000 kwa sahani.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage alimwambia mwandishi kwa simu kuwa hajui kama bei ya bidhaa hiyo imepanda, wala Serikali haijapiga marufuku mafuta kutoka nje ya nchi.

“Kwanza sijui kama bidhaa hiyo imepanda. Halafu Serikali ikitaka kupiga marufuku kitu chochote lazima itangaze kwenye vyombo vyake ikiwamo gazeti, hivyo hakuna taarifa kama hizo,” alisisitiza Mwijage.

Mwenyekiti wa Chama cha Wasindikaji wa Mafuta ya Alizeti Tanzania, Ringo Iringo alieleza kushangazwa na upandaji bei wa mafuta hayo ambayo alidai ni yale yanayoingizwa kutoka nje ya nchi.

Alisema mafuta ya alizeti ambayo wanayazalisha hapa nchini yameshuka bei kwa sasa kutoka Sh45,000 hadi Sh41,000 kwa ndoo ya ya lita 20 kutokana na msimu huu kuwa wa mavuno.

Chanzo: Mwananchi
 
Halafu wanakaa na twakimu zao eti mfumuko wa bei umeshuka, mi Leo home tumenunua sukari kg 4 kwa elfu kumi, haya mafuta nayo yashapanda bei, bado ngano na vingine,
 
kazi ya kutumbua majipu si ya raisi bali niya madaktari rais ni taasisi na mikakati mipango na maarifa makubwa ndo maana kuna jopo kubwa linafanya kazi nyuma ya raisi majukumu ya rais sio kusimama hadharani na kuuliza nitumbue nisitumbueee!!!!!
 
Utafiti uliofanyika katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam umeonyesha kuwa lita moja ya kiungo hicho cha chakula inauzwa kati ya Sh2,800 hadi Sh3,000 kutoka Sh2,500 ya awali.

Dar es Salaam. Wakati Watanzania wakiendelea kuumia na bei ya juu ya sukari, sasa watalazimika kutoboa zaidi mifuko yao kununua mafuta ya kupikia.

Utafiti uliofanyika katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam umeonyesha kuwa lita moja ya kiungo hicho cha chakula inauzwa kati ya Sh2,800 hadi Sh3,000 kutoka Sh2,500 ya awali.

Wafanyabiashara walieleza kuwa wananchi wanashtuka bei hiyo sasa, lakini ilianza kupanda taratibu tangu Machi wakituhumu kuwa hali hiyo imesababishwa na hatua ya Serikali kuzuia mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi.

Serikali imekana madai hayo ikieleza kuwa zuio lolote la bidhaa ni lazima litangazwe wazi.

Mfanyabiashara wa bidhaa za jumla Manzese, Andrea Uiso alisema katoni ya mafuta ya Korie ya lita tatu inauzwa kati ya Sh 49,000 hadi Sh50,000 kutoka kati ya Sh37,000 hadi 42,000 ya awali.

Cosmas Laswai, muuza duka la rejareja Buguruni Rozana alisema sasa wanalazimika kuuza Sh2,800 kwa lita moja baada ya kununua mafuta hayo kwa bei ya jumla ya Sh51,000 ili kufidia hasara.

“Nilipowauliza sababu ni nini wenye maduka ya jumla walinijibu kuwa baadhi ya kampuni wanazochukua bidhaa hii walikuwa wanasafisha visima vyao vya mafuta ndiyo maana kitu kama hiki kimetokea,” alisema Laswai.

Laswai alishauri Serikali kuhakikisha inazuia mfumuko wa bei ili kukabiliana na hali hiyo, kwani wao hawapendi kuuza bidhaa kwa bei ya juu, lakini mazingira yamelazimisha.

Mfanyabiashara wa chips Ilala Bungoni, John Samwel alisema kupanda kwa bidhaa hiyo kumewathiri kibiashara na kwamba hali ikiendelea hivyo watalazimika kupandisha bei ya chips kavu kutoka Sh1,500 hadi Sh2,000 kwa sahani.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage alimwambia mwandishi kwa simu kuwa hajui kama bei ya bidhaa hiyo imepanda, wala Serikali haijapiga marufuku mafuta kutoka nje ya nchi.

“Kwanza sijui kama bidhaa hiyo imepanda. Halafu Serikali ikitaka kupiga marufuku kitu chochote lazima itangaze kwenye vyombo vyake ikiwamo gazeti, hivyo hakuna taarifa kama hizo,” alisisitiza Mwijage.

Mwenyekiti wa Chama cha Wasindikaji wa Mafuta ya Alizeti Tanzania, Ringo Iringo alieleza kushangazwa na upandaji bei wa mafuta hayo ambayo alidai ni yale yanayoingizwa kutoka nje ya nchi.

Alisema mafuta ya alizeti ambayo wanayazalisha hapa nchini yameshuka bei kwa sasa kutoka Sh45,000 hadi Sh41,000 kwa ndoo ya ya lita 20 kutokana na msimu huu kuwa wa mavuno.

Chanzo: Mwananchi

Watu tunashindwa kujua. Sanabu ya haya makitu nkuzuiwa kwa bandari bubu zilizo kuwa zina jaza soko na kuongeza supply ya uongo kwa sasa hiyo mianya imezibwa na kubaki wale waagizaji na walipa kodi halali
 
tutamkumbuka sana mkapa..
hakuna aliekula majani wala kusimamishwa na mambo yalikua
POAAAA...
 
Uzi umeanzishwa na watoto wa Ufipa...naona mnatumia mbinu za mjumbe mpya kwenye panel, Sumaye. Goodluck
 
Naona zama za kila kaya kuwa na kadi la kununulia vitu dukani na kupangiwa kiasi cha kununua
 
Kivyovyote vile tufungeni mikanda ,hizo bei zitatulia tu ,kuna watu walizoea kula kiulaini lakini awamu hii namuunga mkono rais wetu tutaheshimiana tu,wananchi tuseme pale tunapoona bidhaa zikipanda kiholela ,tuko tayari kupikia mawese lakini nchi hii irudi kuwa ya watanzania wote sio wachache #viva Magufuli
 
Back
Top Bottom