Mafua ya asubuhi

Uncle Araali

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
944
1,257
Wakuu,

Nimekuwa na changamoto ya kupiga chafya na kuwa na mafua makali kila asubuhi. Nimetumia dawa zote za mafua lakini hazitibu bali zinapoza tu tatizo.

Naomba kujuzwa chanzo cha mzio huo na namna ninavyoweza kupona tatizo hilo.

Natanguliza shukrani.
 
Wakuu,
Nimekuwa na changamoto ya kupiga chafya na kuwa na mafua makali kila asubuhi.Nimetumia dawa zote za mafua lakini hazitibu bali zinapoza tu tatizo. Naomba kujuzwa chanzo cha mzio huo na namna ninavyoweza kupona tatizo hilo. Natanguliza shukrani.
nami nangoja jawabu nina ndugu yangu anapitia hali hio pia
 
Fua mashuka na blanketi mkuu.

Ila seriously kama unalala umefunga madirisha tegemea yote. Usisahau kuyasafisha pia, badilisha mapazia. Kama ni wanaume wanaweza kukaa na mapazia miaka mitano halijui kufuliwa. Na kama unalalaga na nguo mbichi ndani nayo imo. Au kama Ac yako ina fungus ndani inaweza kuwa chanzo pia. Pelekea mafundi waisafishe.

Niliwahi kulala hotel moja capri point nadhani chumba nlichopewa hakikutumia siku nyingi aisee ile Ac ilininyoosha kwanza nilipata sore throat, nilikaa siku tatu tu lakini nilirudi nyumbani na mafua ya wiki mbili nikaambiwa chanzo ni AC. Pendelea sana kulala dirisha wazi yaani na nyavu ili lipitishe hewa. Carbon dioxide iweze kutoka na oxygen iingie fresh
 
Fua mashuka na blanketi mkuu.

Ila seriously kama unalala umefunga madirisha tegemea yote. Usisahau kuyasafisha pia, badilisha mapazia. Kama ni wanaume wanaweza kukaa na mapazia miaka mitano halijui kufuliwa
samahani, what if yote umeyafanya and still bado hali ni ile ile kuna njie nyingine yoyote ndugu? nasema hivyo sababu ulichosema yeye anakifanya pia
 
samahani, what if yote umeyafanya and still bado hali ni ile ile kuna njie nyingine yoyote ndugu? nasema hivyo sababu ulichosema yeye anakifanya pia
Kula kitunguu swaumu. Inaweza ikawa ni virus.

Ikishindikana nenda hospital
 
Inaweza kuwa vinyama vimeota puani ( nasal polyps) . Ni vzr uonane na Daktari wa pua (ENT specialist ) akufanyie uchunguzi zaidi km tatizo ni hilo unaweza kufanyiwa upasuaji mdogo wa kuvikata hivyo vinyama
 
Wakuu,

Nimekuwa na changamoto ya kupiga chafya na kuwa na mafua makali kila asubuhi. Nimetumia dawa zote za mafua lakini hazitibu bali zinapoza tu tatizo.

Naomba kujuzwa chanzo cha mzio huo na namna ninavyoweza kupona tatizo hilo.

Natanguliza shukrani.
Nimetumia sana centrizen lkn wapi, hii hali inakera, kwangu hata nikinywa kitu cha baridi chafy zinaanza na sikua hivo awali
 
Unatafuna hata punje mbili. Hakikisha ile allicin inaingia mdomoni. Kiwe fresh. Vumilia harufu. Unaweza hata kutafuna na tangawizi.
Shukran ntajaribu kitunguu swaum, vipi kwa mie ambae hata nikitia kitu cha baridi mdomoni lazima nipate mafua na chafya za kutosha
 
Back
Top Bottom