Mafua vs homa kali

Mrs Gudman

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2015
Posts
613
Reaction score
1,300
Naombanei mnishauri kuhusu hii hali
Iko hivi Nina mtoto wa miaka minne ,ila anapata mafua mara kwa mara na Kila mafua yakimshika yanaambatana na joto Kali sana kati ya nyuzi joto 38 hadi 40 hivyo dawaza kushusha homa kama paracetamol hazisaidii nalazimika kuchoma sindano ya Diclofenac Kila mara apatapo mafua,
Nimezunguka hospital nyingi za Dodoma kama Benjamin Mkapa,Ntyuka ,Milembe General na nyinginezo nyingi bila mafanikio.

Pale Benjamin nilienda kwa Dr wa masikio pua na Koo akamcheki akasema Hana shida ya nyama za pua ni Allergy hiyo,Ntyuka napo niliambiwa hivyo hivyo.

Nimempima magonjwa yote jamani sijaona tatizo ,na Kila akipata mafua napima tena na tena ila anaonekana Hana ugonjwa wowote.

Akili yangu imefika mwisho naombeni ushauri wenu ,wa nini nifanye ,au hata daktari anayeweza kunisaidia,kama Kuna mtu aliwahi kukutana na changa moto hii pia anaweza kunisadia.

Mafua yanaambatana na kukoroma
 

Pole kwa kuuguza.
Kwa ufahamu wangu pamoja na reference, mafua ya allergy hayaleti homa labda tu kama kuna complication/kuandamana na kitu kingine.

1: Kama ni mafua tu yanaleta homa, likely yanaletwa na virusi.

2: Ni vyema kueleza kama mtoto alifanyiwa vipimo vingine na majibu yalikuwaje?

3: Kuna historia ya mzio/allergy kwenye familia? Pumu?

4: Kwa watoto, sabuni na mafuta zenye harufu kali, karanga, blueband, unga wa mbegu za maboga na vitu vyenye rangi zisizo asili kama pipi, popocorn na ubuyu wenye flavor, vumbi, vyakula vya baridi/ice cream, juice za viwandani na maziwa huwa ni chanzo cha vikohozi na mafua yasiyoisha.

NB: Bado kuna haja ya mtoto kuangaliwa vyema na daktari bingwa wa watoto ili kupata mwafaka wa kinachojili. Kwa kiasi cha homa, kuna kitu nyuma yake.
 
1. UTI
2. Allergy
3. Infections mchanganyiko zinazohitaji pia matibabu mchanganyiko kwa pamoja


NB:
1. Mimi sio daktari bali nina uzoefu wa malezi ya watoto wadogo
2. Homa kali endelevu sio nzuri kwa mtoto mdogo, pambana utatue issues za kiafya alizonazo mapema. Onana na daktari bingwa wa watoto - ikibidi nenda Dar ambapo consultation ni rahisi kwenye clinic zao binafsi, unalipa gharama unamuona.
 
Asante ,mfano hospital gani
 
Mtoto alifanyiwa vipimo vingi sana na hakuonekana na ugonjwa wowote
 
Allergy Kwa ndugu sijawahi kusikia
 
Fanya uangalizi juu ya ulaji wa vyakula vya mazao ya wanyama au ndege kama ndio chanzo cha allergy kwake mfano nyama, maziwa nk. Pia angalia juu ya uwepo wa vumbi nyumbani ikiwemo mazulia, mashuka nk
 
Asanteni kwa mawazo yenu, mara ya mwisho kuumwa mafua homa ilipanda kama kawaida nilienda kwenye maabara ya hapo kitaa
Na hapo ndo uponyaji w mtoto niliupatia

Yule medical attendant alinishauri nimpe dawa ya tonses ile pen v, nikabishabisha ila baadae nikakubali namshukuru Mungu ni miezi takriban mitano ajawahi chemka ile homa tena

Mpaka mwenyewe nasikia kunenepa [emoji7][emoji7][emoji7][emoji7]God is good and his so faithful, analeta majibu kwA njia nyepesi, wataalamu wote walishindwa nikaja saidiwa na mtu ambaye hata elimu kubwa hana
 
Fanya uangalizi juu ya ulaji wa vyakula vya mazao ya wanyama au ndege kama ndio chanzo cha allergy kwake mfano nyama, maziwa nk. Pia angalia juu ya uwepo wa vumbi nyumbani ikiwemo mazulia, mashuka nk
Asante amepona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…