Pentavalent: Chanjo ya Kifaduro, Dondakoo, Homa ya Ini na Magonjwa ya Homa ya Uti wa Mgongo na Kichomi yanayo sababishwa na Haemophilus influenzae

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
572
2,550
KIFADURO
Kifaduro ni ugonjwa unaoambukiza, husababishwa na vimelea vya bakteria wanaoitwa Bordetella pertussis. Huenezwa kwa njia ya hewa na huwapata hasa watoto wenye umri wa chini ya mwaka mmoja.

9D0410F2-E368-4AA3-B0FF-D9816CF3F4DE.jpeg


Ugonjwa huu huathiri mfumo wa upumuaji wa mtoto. Huambatana na dalili za homa, mafua au kuziba kwa pua, kikohozi kikali kinachotoa sauti kama ya filimbi (au kubweka), kutapika na kubana kwa kifua.

Athari za kifaduro ni kusababisha mtoto apatwe na kichomi, Utapiamlo, Uvimbe katika ubongo na hatimaye kifo.

=====

DONDAKOO

Dondakoo ni ugonjwa unaowapata watoto wadogo. Ugonjwa huu husababishwa na vimelea ambavyo hujulikana kama “Corynebacterium diphtheriae” ambavyo hushambulia sehemu za koo na huenezwa kwa njia ya hewa, mate au majimaji yanayotoka kwenye sehemu za maambukizo.

Ugonjwa wa dondakoo unaojionyesha kwa dalili zifuatazo: -
  • Kukosa hamu ya kula na kushindwa kula
  • Vidonda kooni
  • Kutoa kamasi iliyochanganyika na damu
  • Utando kwenye koo ambao humzuia mtoto kumeza na hata kupumua
  • Maumivu makali ya shingo
  • Shingo pia huweza kuvimba sana na kupewa jina la ‘shingo ya nyati’.

Athari za ugonjwa wa Dondakoo ni kumfanya mtoto ashindwe kumeza na kupumua, kupooza sehemu za paji la uso hadi shingoni pamoja na Kifo.

======

MAGONJWA YA HOMA YA UTI WA MGONGO NA KICHOMI YANAYOSABABISHWA NA HAEMOPHILUS INFLUENZAE (Hib)

Homa ya uti wa mgongo na kichomi husababishwa na vimelea vya aina mbalimbali.

Moja ya vimelea hivyo ni bakteria aina ya “Haemophilus influenzae” ambao hupatikana katika makundi sita (a, b, c, d, e na f), magonjwa ya homa ya uti wa mgongo na kichomi husababishwa na Kundi b (Hib).

Magonjwa haya yameenea duniani kote na kwa kiwango kikubwa katika nchi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania.

Huathiri zaidi watoto wenye umri dhini ya miaka mitano ambapo Hib husababisha zaidi ya asilimia 95 ya visa vyote vinavyo wapata watoto.

Bakteria aina ya Hib huambukizwa kwa njia ya matone ya mate yenye uambukizo kutoka kwa mtoto anayekohoa au kupiga chafya.

Hib pia huenea kwa kubadilishana vitu vya kuchezea kama vile midoli na vitu vingine vilivyowekwa mdomoni.

Bakteria aina ya Hib wanaweza kuathiri kiungo au mfumo wowote mwilini.
Hivyo, dalili zinategemea ni kiungo gani au ni mfumo gani ulioathirika.

Baadhi ya dalili hizo ni-
  • Homa kali
  • Degedege
  • Kukakamaa kwa shingo
  • Kupungua kwa kiwango cha ufahamu
  • Kuathirika kwa mfumo wa fahamu kama vile kutosikia vizuri, upofu pamoja na mtindio wa ubongo na hatimaye kifo
Dalili hizi hutokea pia kwa homa ya uti wa mgongo inayosabishwa na
bakteria aina nyingine.

========

Magonjwa haya kwa pamoja huzuiwa kwa chanjo moja jumuishi yenye mchanganyiko wa chanjo za kuzuia Dondakoo, Pepopunda, Homa ya ini, Homa ya uti wa mgongo na kichomi yaani DTP-HepB-Hib ambayo kwa sasa hujulikana kama Pentavalent.

Hutolewa mara tatu kwa mtoto kwenye umri wa wiki 6, wiki 10 na wiki 14.

Ni lazima mtoto apate chanjo hii mara tatu kwa mpishano wa wiki nne kila moja ili apate kinga kamili.

Chanzo: Mpango wa Taifa wa Chanjo Tanzania
 
Kifaduro ni ugonjwa unaoambukiza na kusababishwa na vimelea vya bakteria wanaoitwa Bordetella pertusis. Ugonjwa huu huenezwa kwa njia ya hewa na huwapata hasa watoto wenye umri wa chini ya mwaka mmoja.

View attachment 2370335

Ugonjwa huu huathiri mfumo wa upumuaji wa mtoto. Huambatana na dalili za mafua au kuziba kwa pua, kikohozi kikali kinachotoa sauti kama ya filimbi (au kubweka), kutapika na kubana kwa kifua.

Athari za kifaduro ni kusababisha mtoto apatwe na kichomi, Utapiamlo, Uvimbe katika ubongo na hatimaye kifo.

Kifaduro huzuiwa kwa chanjo yenye mchanganyiko wa chanjo za kuzuia dondakoo, Pepopunda, Homa ya ini, Homa ya uti wa mgongo na kichomi yaani DTP-HepB-Hib ambayo kwa sasa hujulikana kama Pentavalent ambayo hutolewa mara tatu anapofikia umri wa wiki 6, wiki 10 na wiki 14.

Ni lazima mtoto apate chanjo ya kuzuia Kifaduro mara tatu kwa mpishano wa wiki nne kila moja ili apate kinga kamili.
Shukrani sana kwa taarifa na kwa elimu nzuri kuhusiana na chanjo.

#MaendeleoHayanaChama
 
  • Thanks
Reactions: MCN
Hii imetengenezwa Mwatasi kwa bibi kindore? Au inatoka cyamiozi Kule Mleba kwa bwana kajugusi? Ebu tuelezane kama imetengenezwa Madale kwa Mama dangote?

Kuna wimbi kubwa la watu wanao chanja pepopunda , ukiwauliza waliwahi kuona mgonjwa wa pepopunda? Wanajibu hapana, Cha ajabu hawako tayali kuchanjwa Johnson Johnson Wala Pfizer.

Wanasema ni za mabeberu je hii imetengenezwa buzirayombwe?
 
  • Thanks
Reactions: MCN

Similar Discussions

Back
Top Bottom