Maeneo ya wazi ya Sinza yameanza kuwekwa X tayari kuvunjwa

Chipukizi

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
4,384
6,761
164054eb02f40d48deb15f79ad4c7645.jpg
e0db4d245055c466b2cd4f9c78c8e004.jpg

Huku Sinza ni vilio na taharuki. Serikali inaweka X kwenye maeneo ya wazi ambayo watu wamejenga nyumba za makazi au Biashara.
 
Waamuliwe kubomoa wenyewe na faini juu,....... ili iwe ni fundisho kwa wenye mawazo kama yao!
 
hao ni matapeli tu!
...ilisha kubalika ubomoaji ufanyike mabondeni pekee! ambako ujenzi wake umesababisha joto jingi dar kwa ardhi kukosa pahala pa kupumulia na vegetation iliyokuwepo ilisaidia sana hata kutuletea mvua.
 
Hii kitu ya kubomolewa nyumba bila fidia isikie kwa mwenzako tu inauma mno....Imagine mtu umedunduliza vijisenti ukaenda nunua eneo na tena kwa kufuata taratibu za kijiji, baraza la ardhi la kijiji kwa mwanasheria ukaanza ujenzi hakuna anekuambia imepita miaka 3 leo ndo unakuja ambiwa bomoa hiyo nyumba...Hakuna namna serikali itakwepa lawama hizo ila ndiyo hivyo tena dua la kuku halimpati mwewe.
 
hao ni matapeli tu!
...ilisha kubalika ubomoaji ufanyike mabondeni pekee! ambako ujenzi wake umesababisha joto jingi dar kwa ardhi kukosa pahala pa kupumulia na vegetation iliyokuwepo ilisaidia sana hata kutuletea mvua.
Ha ha ha
 
badala ya serikali kupoteza pesa na kubomoa majengo.ingeyatwaa jayo majengo na kuweka huduma muhimu za jamii kama hospitali,shule na huduma zinginezo.
-ikishindwa imilikishe hayo majengo kwa NHC watu tupange.ama vepeee¡
 
Sheria anasema kutojua sheria siyo kisingizio cha kuacha kuadhibiwa. Kimsingi watu wengi tumedanganywa na watumishi wa serikali ambao siyo waaminifu kwa kutoa offer magumashi. Wapo ambao tulishawishi kwa fedha ili hao watumishi wa serikali wapindishe sheria na kutupatia hivyo viwanja. Bahati mbaya pia wapi waliopewa viwanja hivyo kwa kutojua kwamba wanaibiwa. Lakini ilinapokuja suala la sheria
 
Du,poleni sana watakao athirika na zoezi hili,pia iwe fundisho kwa sisi wengine kuwa sifa ya kweli huwa haujifichi iko siku utaumbuka ikashadhirika, hivyo na watanzania tupende kufuata Sheria, kwasababu tumeziweka wenyewe.
 
Dhana nzima ya kubomoa ili kuzingatia matumizi sahihi ya eneo husika nakubaliana nayo. Ila kuwaacha mamlaka husika waliotoa vibali na kuruhusu ujenzi huo hapo Nadhani Pana tatizo ambalo ndiyo msingi haswa wa kadhia hizi.
Anyway poleni wahanga wa bomoabomoa
 
Rais JPM amesema anapenda sheria,nadhani mahaba hayo ya prezzo na law yanaleta msiba huku,,,chachange,wee mbaura,arex,nawe masawe muje huku kuna dizasta
 
hao ni matapeli tu!
...ilisha kubalika ubomoaji ufanyike mabondeni pekee! ambako ujenzi wake umesababisha joto jingi dar kwa ardhi kukosa pahala pa kupumulia na vegetation iliyokuwepo ilisaidia sana hata kutuletea mvua.
Ina maana waliovamia sehemu za wazi wanaachwa!
 
Hivi viwanja vya kupeana kiholela!

Kwa kweli ni tatizo kubwa sana
 
Back
Top Bottom