SoC03 Maendeleo ya Taifa yanategemea Uwajibikaji pamoja na Utawala Bora

Stories of Change - 2023 Competition
Jun 4, 2023
1
1
Utawala Bora Ni matumizi ya mamlaka husika kwa uwazi, uwajibikaji,ufanisi na ushirikishwaji wa watu katika kufanya maamuzi sahihi katika sekta mbalimbali kama kiuchumi,kijamii nk,kila nchi ambayo inahitaji maendeleo makubwa na yenye tija inahitaji kuwa na viongozi thabiti ambao wanaweza kutengeneza duara la utawala bora na kuwajibika katika nafasi zao kwa pamoja, Kutolea mfano Tanzania ina wizara husika ya utawala Bora ambayo ipo chini ya Mh.Waziri George Simbachawene (MB) akishirikiana na Naibu waziri Wakili Ridhiwani Kikwete (MB),pamoja na uadilifu kwa nchi Kama Tanzania na nchi za Africa katika hii sekta,natoa hoja kuu na muhimu ambazo zitachochea Kwa ukuu uwajibikaji na utawala Bora,

Uteuzi Sahihi wa viongozi, Rais katika nchi husika ana wajibu kikatiba kuteua watu mbalimbali kuwa wasaidizi wake mfano baraza la mawaziri,wakuu wa wilaya na mikoa na viongozi wakuu wa vyombo vya dola,ili kuwepo na uongozi Bora inabidi wateule wa Rais wawe watu wenye weledi na uwezo mkubwa wa uongozi, pia elimu isitumike Kama kigezo kikuu na Cha pekee watu kupata nyazifa katika serikali,Bali vitumike na vigezo vingine Kama historia ya uongozi katika Shule au vyuo walivyosoma, nidhamu na uwajibikaji katika sehemu za Kazi za nyuma kabla ya kuwa mteule mfano Tanzania usalama wa taifa hutumika katika kutafuta wateule, ili kuleta uwajibikaji na utawala Bora inabidi watu wenye uzoefu na uongozi kuchagua viongozi husika na sio watu ambao hawajui chochote kuhusu uongozi au siasa safi na hii itasaidia kuwepo na taarifa kamili ya mteule husika na utendaji wake Kazi

Uwajibishwaji kwa Viongozi wabadhilifu,pia kwa viongozi mbalimbali wawajibishwe endapo watafanya ubadhilifu wa mali za umma kwa namna yoyote mfano kiongozi alikuwa mkuu wa wilaya akihujumu uchumi au kufanya udanganyifu wowote kwa maslahi yake binafsi kikatiba itabidi afunguliwe mashtaka mahakamani na adhabu Kali apewe,hii itachochea uwajibikaji na utawala Bora kwa viongozi wengine maana wataona Ni kosa kubinafsisha Mali za umma,Ila endapo mkuu wa wilaya anakosea tunduru anahamishwa kilosa,hapa hakuna uwajibishwaji wowote uliochukuliwa na heshima ya viongozi haitakuwepi mfano halisi Ni Mh.Sabaya Ole lengai ( Aliekuwa mkuu wa wilaya ya hai) alifikishishwa mahakamani kwa makosa ya uhujumu uchumi Wakati wa uongozi wake ( Taarifa Kutoka Jamii forums)

Serikali kuruhusu maoni Kutoka kwa wananchi wote,moja ya kitu muhimu Ni Serikali kuhakikisha inachukua maoni Kutoka kwa wananchi wanao waongoza bila kubagua Kazi,elimu,nchi nk wananchi Wana uwezo wa kutoa maoni ambayo yatasaidia kukuza na kuchochea uwajibikaji kwa viongozi walio serikalini na waliobeba dhamana kuu ya kuongoza wananchi mfano wabunge,Kumekuwa na dhana mtu akitoa maoni yake kwa Serikali kwa upande wa hasi atawajibishwa vikali,Sasa bila maoni ya wananchi itakuwa ngumu utawala Bora kuwepo maana kutakuwa hamna mfumo mzuri wa kutambua makosa ambayo yanafanywa na viongozi mbalimbali na wa sekta husika

Uwazi na ushirikishwaji wa Habari muhimu kwa wananchi,nchi nyingi Kumekuwa na wimbi la kuwaficha wananchi taarifa mbalimbali muhimu ambazo Ni nyenzo kuu za utawala Bora,ili nchi iweze kwenda vizuri inabidi wananchi washirikishwe katika sehemu za maamuzi muhimu mfano kwa mawazo yangu katika nafasi Kama Mkuu wa NEC-Chombo kinachohusika na uchaguzi inabidi wananchi wapate nafasi kupiga kura na kumchagua mtu wamtakae na kumwamini ili aweze kumptisha Rais mwenye maono mazuri wa nchi husika,kitendo Cha Serikali kuruhusu wananchi kuweza kushiriki katika maamuzi mbalimbali itakua rahisi kuwepo uwazi na uwajibikaji ambao utaunda utawala Bora kuanzia ngazi za juu za Serikali mpaka ngazi ya chini

Mwisho, Nchi nyingi za Africa Kumekuwa na uwajibikaji mdogo na utawala mbovu katika serikali,lakini wakijaribu kufata njia stahiki hapo juu itasaidia kuchochea utawala Bora katika nchi husika mfano Nchi Kama Tanzania inabidi iboreshe mifumo baadhi ambayo itasaidia kuleta mabadiliko makubwa kwa wananchi pia na Serikali na itasaidia wao kujiweka karibu na wananchi/waongozwa
 
Back
Top Bottom