Maendeleo ni nini

KYANYINIMARAIGA

Senior Member
Joined
Oct 21, 2016
Posts
192
Reaction score
127
Kwa nyakati tofauti nimekuwa nikisikia au kusoma maandishi ambayo yanamuelekeo wa kusema "fulani kaendelea"."Taifa fulani limepiga hatua katika maendeleo" au "maendeleo ni ushirikiano" au wewe "hupo nyuma kimaendeleo" nk.Swali ni je maendeleo ni nini? na nini kipimo cha maendeleo ya mtu binafsi na maendeleo ya Nchi kwa Ujumla.Je ukiwa na ukwasi mzuri ndo maendeleo ? Naomba msaada wa kitaalamu.Matumizi ya takwimu na mifano halisi yatasaidia sana.
 
Maendeleo ni kupiga hatua kutoka nafasi moja kwenda nyingene katika uelekeo chanya. Ni neno la jumla, hivyo maana halisi ya maendeleo inategemea unazungumzia maendeleo ya kitu gani, kama vile maendeleo ya kiuchumi, kiteknolojia, kijamii, kibailojia n.k . Kila aina ya maendeleo itakua na maana yake ambayo ni mahususi kwake tu.
 
ni kweli.Kwa swali hili tujaribu kueleweshana maendeleo ya kiuchumi na kijamii .
 
Maendeleo ni kuwa vile kitu/mtu anapaswa kuwa. Na maendeleo si mafanikio, sababu mafanikio ni kuwa vile kitu/mtu anataka awe. Hivyo basi maendeleo na mafanikio ni vitu viwili tofauti kabisa.

NB:Hiyo ni Falsafa yangu tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…