Maduka yanayouza vifaa vya umeme Mwenge

Maduka yanayouza vifaa vya umeme Mwenge

DaPilly

Senior Member
Joined
Mar 2, 2012
Posts
181
Reaction score
68
Ndugu zangu wana JF,
Napenda kuwatahadhari na maduka yanayouza vifaa vya ujenzi mwenge kwenye round-about inayotokea mwenge sokoni kuelekea ubungo. Maduka haya kibiashara yapo eneo zuri na ni karibu sana na barabara kiasi kwamba mteja anaweza akawa kwenye gari yake kama ana gari na akaagizia kuletewa kifaa anachohitaji kununua. Tahadhari ni kwamba maduka haya mbele kabisa kuna vifaa vingine ni vya vyombo vya ndani (fenicha) ndogo ndogo kama coffee table, lakini mbele ya hayo maduka especially ya ujenzi kuna vijana wanasimama wenye maduka wanawafahamu lakini wnawatazama. Vijana hao ni wezi na endapo utaibiwa wenye kuuza bidhaa hizo wanasema haweahusiki kabisa.

Ninaomba nitoe mfano huu, mdogo wangu kuna siku alinieleza kwamba kuna mama alikuwa anatokea ubungo akawa anapaki gari yake lakini wakati anamaliza kupaki handbag yake hakuiona kwenye gari badala yake akaona kijana amesimama anamtazama. according to mdogo wangu ilibidi huyo mama ambane huyo kijana amwambie begi lake limekwenda wapi wakati anapaki begi alikuwa nalo kwenye gari.

Mfano wa pili ni mimi mwenyewe, jana asubuhi nilikwenda hapo mwenge nilitokea makongo juu, niliingia dukani (gari nilikuwa nimepaki pembeni) ili ninunue vifaa vya umeme, nikaambiwa bei ya vitu ninavyotaka, nikamwambia ninazunguka around nakuja, niliporudi nilikuwa nimeongozana na fundi wangu mkononi fundi wangu alikuwa na bomba za umeme 6 na vifaa vingine vilikuwa kwenye mfuko na pasi used ya umeme. Yule fundi alichomeka hivyo vifaa mbele ya duka hilo kuna sehemu iko wazi na ina vitu kama hanger akachomeka ule mfuko wa rambo na vifaa kidogo vya umeme (vyenye thamani) ya 1500 pamoja na hiyo pasi used.

Tulinunua vifaa vya umeme vya 3500 ndani ya dakika kama 5. Kugeuka mfuko wa rambo wa pasi umekwenda. Nilimgeukia mwenye duka nikamwambia kibiashara hawa watu wezi (baada ya kugundua mfuko umeibiwa) wanakuharibia biashara. PIA baada ya kuibiwa kulikuwa na vijana 3 mbele ya duka hilo wanatazama kama vile kutaka kujua kwenye rambo kuna nini, kwa mimi nilihisi mmoja wao ndio mwizi. Sikupata ushirikiano lakini kwa uelewa wangu wanaouza maduka mwenge eneo la round about inayoelekea ubungo wanawajua wezi. Kwa ushauri wangu kama hawataki kuwataja wezi kwa kuwa wateja wao wanakatishwa tamaa hata kujiapiza wasirudi maduka hayo nadhani ni wakati muafaka sasa kuwaambia wateja wapaki at their own risk. vinginevyo kibishara itamuwia ngumu mteja aliyeibiwa kurudi eneo hilo.

Ninawahasa wateja wanaopenda kufanya manunuzi ya vifaa vya ujenzi maeneo ya mwenge kwenye kona inayoelekea ubungo hilo eneo si salama hivyo waende maeneo yanayoonekana yana usalama zaidi.

KAMA MAELEZO YANGU YATAWAKWAZA WENYE MADUKA NAOMBA MSAMAHA NA NI WAKATI MUAFAKA WA KUFANYIA KAZI VIBAKA WANAOZENGEA KWENYE MADUKA HAYO KWANI NI IMANI YANGU KUWA WANAWAFAHAMU.

ASANTENI
 
kweli kabisa ....hata makondakta wa dalala zetu baadhi wanawatambua wez wa simu ila hawawachukulii hatua zozote... tz tunalindana sana kwenye secta za uhalifu sijui kwa nini? eg mafisadi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom