Madudu Mengine Elimu

Ni kweli kabisa mkuu B. Sijui ni kwanini wabunge wa upinzani na kuwa kitu kimoja? Hicho ndo kinachotakiwa kwa wabunge na sio kuitetea serkali kama anavyofanya Mwigulu. Safi sana Mbatia.
 
Tulisikia.
Vipi kibwete ; unadhani ni kwanini wabunge wa CCM wanaendelea kuilinda wizara tu licha ya udhaifu wote huu ambao hata Jk kakubali kwamba upo, ila wakati wapinzani wakichachamaa; CCM, Wao wanatetea?
 
Last edited by a moderator:
betlehem Inasikitisha viongozi wengi wa serikali na wabunge wameamua kusimama kwa maslahi ya chama,
kuliko maslahi ya taifa hili,inashangaza mbunge anasimama kutetea madudu ambaya yako wazi na yanaonyesha jinsi kusivyo na uwajibikaji ndani ya serikali.

Any way tatizo kubwa ni kuanzia juu kama rais hajui kwa nini Tanzania ni maskini pamoja na raslimali zote
zilizojaa kwenye hii nchi,unategemea waziri atajua kwa nini elimu ya Tanzania inashuka!!? wote wapo bora liende"
 
Ki ukweli Mbatia anahitaji support kubwa toka kwa wabunge wenzake na hata kwetu kuikoa Elimu yetu! Katika teuzi makini, naona Rais hakukosea kwa Mbatia. Tatizo haliko shule za msingi tu, kwa upande wa sekondary utitili wa vitabu umezidi na hili huwachanganya wanafunzi! "Enyi wabunge wa CCM, muogopeni MUNGU muache unafiki wa kutetea upuuzi unaoonekana hata kwa watoto!! Hivi hawa wabunge, wanafahamu kuwa wanadharauliwa sana kwa upuuzi wanaotetea!! Shame upon them !!
 
Muda si mrefu utawasikia CDM inahusika!:heh:
 
Mh. Mbatia ni jembe basi i wish ningekua rais bila kujali anatoka chama gani ningempa uwaziri wa elimu
 
Tatizo haliko shule za msingi tu, kwa upande wa sekondary utitili wa vitabu umezidi na hili huwachanganya wanafunzi! "Enyi wabunge wa CCM, muogopeni MUNGU muache unafiki wa kutetea upuuzi unaoonekana hata kwa watoto!!
Vitabu vinavyotumika Sekondari; ni vile vya Mh.Nyambari Nyangwine (Mbunge).Inasemekana hivyo ndio vyenye afadhali..
 
hata wizara ya afya kuna madudu hivyohivyo,kuna modules zinazotumika kwa wanafunzi wa taaluma ya afya ngazi ya diploma na cheti ambavyo ni msaada wa mashirika ya kimataifa(I-tech,us PEPFAR) ziko shallow mno,hazina ubora ukilinganisha na umuhimu wa sector husika kwa maendeleo ya jamii
 
Kuna KISWAHILI kusoma na kuandika sehemu ya kwanza-darasa la 1.na M.G.MKINGA ukurasa wa 41,42,43 bomu kabisa.mwanafunzi hawezi kusoma mfano- mf mg ataelewa nini?
 
Dah!... Mmenifumbua macho... Itabidi niwe nafanya review ya vitabu kabla sijawapa wanangu wasome.
 
Mambo mengine yanayoendelea kwenye hii nchi yanatia kichefu chefu!

Mtu unajiuliza viongozi na wataalamu wote wa wizara wapo pale kwa faida gani?! Hupati jibu!
 
Mbatia ni mpinzani wa kweli, co wale wanaosema tufunge mlango tupigane. Big up Mbatia.
 

Kiuhalisia na kama nchi yetu ingekuwa inasimamia haki, maadili na kanuni za utendaji pamoja na uwajibikaji; wizara ya elimu ilitakiwa iwe imeshafutwa na kazi zake kukasimiwa na wizara ama ofisi nyingine ya serikali.

Naweza kuonekana kituko kwa mtizamo wangu lakini ukweli ni kuwa wizara yenyewe imeshindwa kujisimamia na hakuna jinsi yoyote utaweza kutarajia matokeo chanya kutokana na kitu ambacho hakijimudu ama hakiko sahihi. Wizara ya elimu inaweza kuwa mfano wa wizara ambazo haziwezi hata kuhakiki taarifa na matangazo yanayotolewa na wizara hiyo na katika hali hiyo ni dhahiri kuwa hata yale yanayofanywa nje ya wizara hiyo yatakuwa chini ya kiwango kwa kuwa hakuna uhakiki wa kina unaofanywa na wizara husika.

Mfano mzuri ni pale unapofungua tovuti wa wizara ya elimu, hakika aina ya habari na matangazo utakayokutana nayo yanatia hasira kwani naamini makosa yanayofanywa kwenye matangazo hayo ni kielelezo halisi cha kukosa umakini kwa watendaji wake.

TAARIFA MUHIMU ZA USAJIRI WA SHULE NA WALIMU - VIPEPERUSHI

TAARIFA MUHIMU ZA USAJIRI WA SHULE NA WALIMU - VIPEPERUSHI

JARIDA LA ELIMU Toleo la 1/2013 : Januari - Machi 2013

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
JARIDA LA ELIMU
Toleo la 1/2013 : Januari - Machi 2013
Jalida la Elimu - Kiswahili (1.08 MB)
Jalida la Elimu- English (1.07 MB

Chanzo: United Republic Of Tanzania - Ministry of Education and Vocational Training
 
Aisee mimi ndo ningekuwa Rais J M KIKWETE, ningefumba macho tu na kuvaa uzalendo kwa kumteua Bwana James Mbatia kuwa WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI katika nchi hii kuanzia LEO!!

I believe huyu jamaa anaweza kuleta mabadiliko chaya katika eneo hili japo katika mfumo huu huu ulioparanganyikana chini ya CCM!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…