Hii habari inaonesha jinsi nchi ilivyo katika hali mbaya. Kila mwenye/wenye nafasi wanajiangalia wao kwanza. Sikutegemea wawakilishi wa wananchi kujadili mambo kwa ubinafsi/umimi wa hali ya juu kama huu. Hebu angalia hii argument yao:
"Huwezi kuamini, leo baadhi yetu tunalalamikia kupanda kwa sukari na gharama za maisha lakini ukweli ulio wazi wabunge wanaishi kama wafalme katika nchi hii...inabidi na sisi tusimame imara tuhakikishe tunaongezewa posho na kupewa mikopo"
Kumbe kinachowaumiza hapa ni WABUNGE kuishi kama wafalme ilhali WAO (MADIWANI) wakiwa hawana kitu na sio wananchi wa hali ya chini. Hii inamaanisha wakipatiwa hicho wanachokihitaji, kelele zote zimekwisha; wananchi mtajua wenyewe. Kuna haja ya KATIBA MPYA ku-address hivi vitu. Suala la mishahara na viwango vyake kwa watumishi mbalimbali, hususan wa wanolipwa kwa kodi za wananchi, ni lazime liwe la kikatiba na sio suala la kuunda tume au kundi fulani kama wabunge kujilipa kifisadi wanavyotaka wao.
Ni lazima Katiba iseme wazi, kwa mfano, kima cha chini cha msahara na posho nyingine haziruhisiwi kutofautiana kwa (zaidi ya) kiwango fulani na kima cha juu kabisa. Na pia kama ilivyo kwa viongozi/rais wastaafu ambao nadhani wanalipwa 80% ya mshahara wa rais aliyeko madarakani wakati huo, kanuni hii, au kadiri Katiba Mpya itakavyoagiza, pia i-apply kwa watumishi wengine na sio kwa wachache kana kwamba wao ni miungu.