Mkuu hizi picha za hii barabara mbona kama umeleta nzuri? Kusema ukweli hii barabara ni mbovu tena mbovu haswa, tena usiombe ukapita na gari ndogo utajuta. Mara ya kwanza napita hii njia niliuliza wenyeji ni kwa nini hii barabara ni mbovu hivi inamaana wahusika hawaoni? Nikajibiwa na raia tu ambaye naye sikuweza kumwamini sana eti kuwa hi barabara ni yakimataifa hivyo hizi nchi tatu yaani Rwanda, Tz na Burundi zinategeana.
Ubovu wa miundombinu unachelewesha sana maendeleo na ndio husababisha gharama za maisha kupanda, leo hii kutoka Ngara to Mwanza gari zipo mbili tu na zinaondoka asubuhi, kutoka Ngara mjini kwenda Rusumo unapaswa uzungukie Benaco. Ile njia ya mkato mto umejaa hivyo magari hayapiti maana kivuko hakifanyi kazi.
Gari zinazofanya safari kutoka Ngara mjini na viunga vyake ni kama tax hakuna daladala na watu hujazwa kweli bila kuzingatia usalama. Kwa kuwa gari ni ndogi hivyo nauli huwa kubwa.
Pamoja na yote hayo pia niipongeze TARURA Ngara kwa kweli wanarekebisha sana barabara hasa kwa kiwango cha Lami, Zege na Changarawe.