Tatizo kubwa ni kwamba wenye dhamana ya maamuzi hawana nia ya dhati kukomesha tabia hii ya viboko. Nafikiri wazazi tuchukue hatua ila hata serikali ituunge mkono.
Nakumbuka wakati niko shule ya msingi, kuna mwalimu alikuwa anasifika kwa viboko; siku moja alituchapa darasa zima, mimi niliondoka baada ya kuchapwa nikarudi nyumbani. Mtoto mwingine alienda moja kwa moja akamweleza baba yake. Baba alipoona michirizi ya bakola hizo, alienda kwenye banda akachukua mbuzi mmoja akaondoka naye hadi hapo ofisini kwa mwalimu mkuu.
Alipofika akaingia ofisini na kumshukuru vizuri huyo mwalimu, kisha akamwambia kuwa amemletea zawadi ya mbuzi, hivyo akamwomba atoke nje akabidhiwe.
Kilichotokea pale, ni kwamba ...
Mzazi alimtandika bakola huyo mwalimu akimweleza kuwa awe anamtandika mbuzi badala ya mwanae.
Hadi tunamaliza la saba ... mtoto wa huyo mzazi alikuwa hapigwi.