Madhara ya unene uliopitiliza (obesity)

muzi

JF-Expert Member
Jun 17, 2016
1,038
1,448
Madhara ya unene uliopitiliza (obesity)

1581409495331.png
1581409495331.png


Tatizo hili la unene uliopitiliza kuliko inavyo hitajika kiafya huwa linaletwa na kuongezeka kwa kiwango cha mafuta mwilini.

Njia rahisi na inayokubalika ya kuweza kugundua kama mtu ni mnene kupita kiasi (obese) inafahamika kama kipimo cha Body Mass Index (BMI). Vipimo hivi vya BMI ndio vinaweza kukujulisha kama unene ulionao unastahili kulingana na umri, urefu na uzito wako.

Tatizo la unene uliopitiliza husababishwa na nini?
Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha unene uliopitiliza. Mambo hayo ni pamoja na: Vyakula vya mafuta, Kutofanya mazoezi, Kurithi viashiria vya asili (genes)

Umri - Watu wengi huongezeka uzito au hunenepa kadri umri unavyoongezeka kwa sababu wanakuwa hawajishughulishi sana (less active) na huwa wanapungua maumbile ya miili yao (muscles mass)
Matatizo ya kisaikolojia,

Dawa - Baadhi ya dawa zenye madhara ya kuongeza unene ni kama corticosteroids, blood pressure medications, tricyclic medications na kadhalika.

Kufanya Mapenzi
Unene uliopitiiza hasa kwa wanaume hupoteza ufanisi wa kufanya mapenzi. Unakuta mtu ana tumbo kubwa uume mdogo hata akisimama wima hakionekani sababu ya unene. Lakini pia watu wanene wanachoka haraka sana wakati wa kufanya mapenzi, wengi hukosa pumzi na kuishia kuhema kama mtu aliyekimbia kilometer 10.

Hivyo inapaswa kila mtu kwa sehemu yake awe ana contol diet otherwise nyumba ndogo itakuhusu

Magonjwa yanaoweza kuambatana na tatizo la unene uliopitiliza
  • Kisukari
  • Shinikizo la damu (hypertension)
  • Kiharusi (Stroke)
  • Magonjwa ya moyo
  • Tatizo la kutopumua vizuri wakati mtu yupo usingizini (Sleep apnea)
  • Vijiwe katika mfuko wa nyongo (Gallstones)
  • Kiwango cha juu cha lijamu kwenye damu (cholesterol ikiwemo triglycerides)
  • Ugonjwa wa mifupa kama yabisi (osteoarthritis).
  • Saratani ya matiti
  • Saratani ya tezi dume (prostate cancer)
  • Saratani ya utumbo mpana pamoja na maeneo ya haja kubwa (Colorectal cancer)
  • Matatizo ya mzunguko na mishipa ya damu kama vile kuvimba kwa vena za miguuni (varicose veins). Kwa ushauri
Ijali afya yako
 
Ukisoma kama umeipenda au kukusaidia weka basi like au comment
Asante sana wawejaaa
 
Back
Top Bottom