Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha
Rushwa adui wa haki,tena donda linonuka
Hukosa pa kushitaki,ukapata kusikika
Mtoaji hudhihaki,hauna pa kumshika
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha
Yafika mahakamani,hakimu apinda kesi
Yakakufika shingoni,mambo yakawa meusi
Ukabaki hatiani,waenda somba vifusi
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha
Kifika serikalini,huduma upate pesi
Zama kwanza mfukoni,uzitoe simbilisi
Huduma zawa mwanzoni,ukapata bila wasi
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha
Huko nako mavyuoni,mambo yana ukakasi
Walimu wako mbioni,wanawataka mamisi
Wanavitaka vya ndani,ili wazidishe maksi
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha
Ajabu nao wa dini,wanayafanya maasi
Yafika makanisani,waitaka makasisi
Mashekhe misikitini,mwakosa firidausi
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha
Nchi haina amani,rushwa kawa ni asasi
Atupeleka gizani,tusimoweza kuhisi
Anauwa masikini,awatukuza makwasi
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha
Kina baba amkeni,tukampinge muasi
Na mama zangu twendeni,nanyi mnayo nafasi
Adui tumchapeni,atukome ibilisi
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha
Wasomi nanyi njooni,tuundeni taasisi
Msilete utengani,mkageuka waasi
Mikono tushikaneni,mambo yakawe rahisi
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha
dee
0675269703