Madhara ya rushwa katika uchaguzi

Madhara ya rushwa katika uchaguzi

Papaa Muu

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2018
Posts
243
Reaction score
292
Ndugu zangu naomba tukumbushane yafuatayo:

Rushwa katika siasa hujenga mfumo wa Uongozi usio wazi na usiowajibika kwa wananchi husika:
----------------------------------
1. Rushwa huondoa uhuru wa mpiga kura.

Hapa mpiga kura hukosa uhuru wa kumchagua yule anayefaa, hivyo hujikuta akimchagua yule aliyemhonga.
Kiongozi aliyepatikana kwa kutumia rushwa hudharau wapiga kura maana huamini kuwa pesa zake ndizo zimemweka madarakani

2. Wagombea wenye vipaji na uwezo wa kuwakilisha hushindwa kushiriki kugombea katika uchaguzi kwa kukosa uwezo wa fedha.

Rushwa hupotoa maneno ya wenye haki na wenye sifa stahiki

3. Rushwa huharibu dhana nzima ya uwakilishaji kwa kuwa wanaochaguliwa hawana ridhaa kamili ya mpiga kura.
Siku zote viongozi wengi wanaopatikana kwa njia ya rushwa uwezo wao wakiuongozi ni mdogo sana.

Hivyo hupelekea wananchi kukosa watetezi stahiki kwa kipindi chote cha Uongozi

4. Viongozi waliochaguliwa kwa njia ya rushwa kamwe hawawezi kusimamia mapambano dhidi ya rushwa.

Hawa Wanakuwa ni viongozi wapenda dhuluma na wasiojali kusimamia haki

5. Rushwa husababisha usimamizi wa shughuli za Maendeleo kukwama Kutokana na vitendo vya ubadhilifu wa rasilimari za umma.

Kiongozi aliyeingia Madarakani kwa kutumia rushwa, lazima atataka kurudisha gharama zote alizotumia kuhonga pindi atakapokuwa madarakani,

hivyo kamwe hawezi kuhangaikia Maendeleo ya wananchi, bali atahangaika kurudisha pesa zake kwa kufanya ubadhilifu.
________________________________
LONGA NA TAKUKURU BURE.
Piga 113
SMS 113
Bonyeza *113#
---------------------------------
Mimi na wewe tuwe mstari wa mbele kabisa kuwapinga wagombea wote watakaotaka kutumia rushwa kupata madaraka.
Toa taarifa zozote sahihi zinazohusu mianya ya rushwa ili uchunguzi uanze haraka iwezekanavyo

Imetolewa na:
Jumuiya ya wanafunzi wanaopambana na kupinga rushwa ,
UDOSOAC ,
S.L.P 259,
DODOMA.
~Kyomo, bahati
Mwenyekiti-Shirikisho

________________________________
RUSHWA HUPOFUSHA MACHO, USIKUBALI KUWA KIPOFU
---------------------------------
 
Rushwa ni adui wa haki kamwe hakuna kitu kibaya na dhambi kubwa kama rushwa kwanza upoteza amani tumuombe Mungu atufungue tuyajue haya na roho ya Mungu iwe ndani ya mioyo yetu
 
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha

Rushwa adui wa haki,tena donda linonuka
Hukosa pa kushitaki,ukapata kusikika
Mtoaji hudhihaki,hauna pa kumshika
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha

Yafika mahakamani,hakimu apinda kesi
Yakakufika shingoni,mambo yakawa meusi
Ukabaki hatiani,waenda somba vifusi
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha

Kifika serikalini,huduma upate pesi
Zama kwanza mfukoni,uzitoe simbilisi
Huduma zawa mwanzoni,ukapata bila wasi
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha

Huko nako mavyuoni,mambo yana ukakasi
Walimu wako mbioni,wanawataka mamisi
Wanavitaka vya ndani,ili wazidishe maksi
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha

Ajabu nao wa dini,wanayafanya maasi
Yafika makanisani,waitaka makasisi
Mashekhe misikitini,mwakosa firidausi
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha

Nchi haina amani,rushwa kawa ni asasi
Atupeleka gizani,tusimoweza kuhisi
Anauwa masikini,awatukuza makwasi
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha

Kina baba amkeni,tukampinge muasi
Na mama zangu twendeni,nanyi mnayo nafasi
Adui tumchapeni,atukome ibilisi
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha

Wasomi nanyi njooni,tuundeni taasisi
Msilete utengani,mkageuka waasi
Mikono tushikaneni,mambo yakawe rahisi
Zuia kataa rushwa,tokomeza elimisha
dee
0675269703
 
Unaweza vuta mpunga na ukapiga kura kwa mgombea uliyemwelewa,hela ukipewa chukua tu usiache ila piga kura mgombea mwenye sifa na unayedhani atawavusha
 
Back
Top Bottom