Madhara ya mtoto kula mkaa.

BRO SANTANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2015
Posts
1,845
Reaction score
2,249
Wakuu kwema?
Weekend hiyo hapo inakuja.
Naomba ushauri mtoto wangu wa kike ana mwaka mmoja na miezi 2 lkn anapenda sana kula mkaa.
Naomba kujua hasara au faida za kula mkaa kwa mtoto mdogo.
Nawasilisha.
 
Wangu pia anafanya hivyo tangu aanze kuota meno...ila namuacha tu,sidhani kama una madhara...
 
Wangu pia anafanya hivyo tangu aanze kuota meno...ila namuacha tu,sidhani kama una madhara...

Mkaa kama Carbon huwa ni tiba inayotoa sumu iliyoingia mwilini kwa njia ya mdomo. Inasaidia tu kama sumu imenywewa kata ndani ya lisaa limoja.

Nimetoa tu faida ya kula mkaa.
 
Mkaa kama Carbon huwa ni tiba inayotoa sumu iliyoingia mwilini kwa njia ya mdomo. Inasaidia tu kama sumu imenywewa kata ndani ya lisaa limoja.

Nimetoa tu faida ya kula mkaa.
Nashukuru mkuu.
Ngoja nisubiri na hasara zake.
 
Hasara zake ni kifo tuu akizidisha. Jiandae kuzaa mwingine fasta huyo utamkosa soon asipoacha. Mm nilipoteza kwa njia hiyo hiyo.
Daaa mkuu hebu punguza jazba maana unaonekana una pointi za msingi lkn haujatulia.
Toa pointi tujifunze nasisi yasitukute kama ulipata uthibitisho toka kwa daktari kuwa mkaa ndio ulipoteza mwanao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…