Bernard bakari
JF-Expert Member
- Mar 30, 2016
- 407
- 781
Kuna wakati mwanaune huamua kumwoa mwanamke asiyempenda ili tu kukidhi haja fulani iliyopo ndani ya moyo wake. Zipo sababu nyingi zinazompelekea mwanaume kumwoa mwanamke asiyempenda kama vile, kulazimishwa na wazazi, kumkosa mwanamke aliyempenda kwa dhati wenda kwa kuporwa au mwanamke kuamua kumtosa mwanaume, kufiwa na aliyempenda hivyo kuamua tu kuoa haraka ili apate msaada wa kusaidiana naye kulea familia, kutafuta kulelewa na majimama na sababu zinginezo.
Ikitokea mwanaume kaoa mwaname asiyempenda toka ndani ya moyo wake hukumbwa na madhara mengi sana kama vile: kutofurahia tendo la ndoa mara anapokutana na mwenza wake hivyo kukosa raha na utamu wote wa tendo la ndoa hujiona mpweke na mkiwa katika ndoa yake.
Mwanaume aliyemwoa mwanamke ambaye hampendi toka ndani ya moyo wake husababisha ugomvi wa mara kwa mara ndani ya nyumba, hujikuta hata kama mwanamke kafanya kosa dogo la kibinadamu huja juu na kufoka kana kwamba kuna mtu kauawa.
Humfanya mwanaume kutafuta mwanamke mwingine nje ya ndoa ili kukidhi furaha ya moyo wake hivyo huweza kusababisha magonjwa mbalimbali yatokanayo na zinaa kama vile kaswende, kisonono hata ukimwi.
Humfanya mwanaume kutomjali wala mheshimu mke wake hivyo mke huwa hatendewi vyema. Mke hukosa haki zake za msingi kama mke wa ndoa.
Humfanya mwanaume kutomshirikiaha ipasavyo mke wake katika mambo mengi ya maendeleo na ya maamuzi ndani ya nyumba hivyo hufanya maamuzi ndani ya nyumba yawe ya mlengo mmoja kitu ambacho si sahihi katika maisha ya ndoa.
Sisi kama jamii kwa ujumla tusiwe chanzo cha kusababisha mwanaume amwoe mwanamke asiyempenda kwa namna moja au nyingine, NDOA YENYE FURAHA HUMPENDEZA MUNGU NA MALAIKA WAKE PIA.