Madereva wa daladala Manispaa ya Moshi, Kilimanjaro wamesitisha kutoa huduma ya usafiri

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Madereva wa daladala Manispaa ya Moshi, Kilimanjaro wamesitisha kutoa huduma ya usafiri leo wakidai hawataki kuona bajaji katika maeneo yao.

Daladala zenye mgogoro na bajaji sio zote bali zinazofanya safari kati ya mjini na KCMC.

Chanzo cha mgogoro ni madai ya kwamba Bajaji wanaingia mpaka stendi ndani kitu ambacho daladala hawataki na mpaka sasa hivi bado wapo kwenye mazungumzo kutatua mgogoro huo
 
Lakini kweli bhwana bajaji ni kero kuliko Yaani we katiza mbele yao hata kwa Mguu uone hiyo mitusi halafu wanavyochomekea magari sasa Yaani ni mungu tu anasaidia Lakini ajali nje nje
 
Mimi nilijua wanagoma wenye magari,kumbe madereva?
Halafu wakigoma watakula nini
 
Usafi wa Moshi kumbe wame fall kwenye kuweka utaratibu wa mpangilio mzuri wa vyombo vya usafiri1
 
Unajua daladala walifika mahali wakajisahau, sasa wameona faida ya soko huru. Yaani mtu anawahi hospital na tayari kapakia level seat ila haondoi gari mpaka mshindiliwe, ukisema tuu utatukanwa. Huku koda mchafu mchafu. Sasa wamekuja bajaji wanalalamika. Ase SUMATRA waandikie barua za kuwataka waombe radhi kwa walio tayari kufanya usafirishaji na wanaotaka kugoma futa vibali vyao na waondoeni barabarani. Full stop.

NB
Kwa bajaji axmcheni ujinga wa kupandisha nauli katika kipindi hiki hasa kufika Ushirika wa Neema. Mkiendelea just fanya 500 mtawafanya wananchi wasione shida na huo ujinga wa daladala utaisha na mmoja mmoja atarudi mwenyewe
 
Back
Top Bottom