Madawa ya kulevya

HABAKUKK

Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
6
Reaction score
2
Nimemsikiliza vizuri Dr Harrison Mwakembe, ni mtu mkweli anaonekana machoni
Ila nimeshangaa tunakwenda wapi??wafanyabiashara wa madawa ya kolevya
wanapesa ndefu sana,ukifwatilia nchi mbalimbali utaona vituko mimi namwomba
sana asikurupuke na najua hatakurupuka maana kupoteza maisha ni dakika moja,,
nimeona baadhi ya mada watu wanamshitumu,hiyo siyo kazi rahisi ndugu,zanguni,
marehemu william Saitoti??wakati anapambana na madawa ya kolevya alisema
mawazo yangu ni mungu anajua,,na akapotelea angani ni biashara inafanywa na watu
wakubwa sana,DR,Mwakembe anasema aliwahi kufa akafufuka,,historia ya Dr Mwakembe
inaniogopesha sana maana naona maneno yake hayana tofauti na marehemu Saitoti
kitendo cha kuweza kutaja afsa usalama wa taifa na polisi ni ujasiri mkubwa ,,,hilo ni
jibu kuwa hawa wafanya biashara siyomchezo kuweza kununua usalama wa taifa?
Ni mwanzo mzuri na ni kazi ngumu,,ila cha muhimu achunguze mizizi yake ni minene
kiasi gani, ataweza kuiong'oa kusema kweli mwanaume hupaswi kuogopa maana kufa lazima tufe,,
 
:A S-key: kifo tumeumbiwa binadamu, kikubwa ni jamii kumuunga mkono waziri na kujitolea kumlinda na kumpa taarifa za mara kwa mara, nina shaka na ulinzi unaoombewa kwa serikali wakati ndani yake kuna ambao hawapendi kuona waziri akifanikiwa kwani wataumbuka wengi, kwahiyo tuwe makini na ulinzi wake usiwe ndiyo chanzo cha yeye kudhulika, LAKINI UKIMWUA WEWE UTAISHI MILELE?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…