Madawa ya Kulevya: Waziri wa Katiba na Sheria aomba Shikuba akashtakiwe Marekani!

billduke

JF-Expert Member
Mar 19, 2013
860
898
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amewasilisha maombi mahakamani akitaka watanzania watatu akiwemo Ally Hajji maarufu Shikuba wapelekwe nchini Marekani kujibu mashtaka ya kufanya biashara ya dawa za kulevya.

Wakili wa Serikali Mkuu, Edwin Kakolaki aliwasilisha maombi hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha.

Kakolaki aliwataja washtakiwa katika maombi hayo kuwa ni Ally Haji maarufu Chikuba, Iddy Mfuru na Tiko Adam.

Wakili huyo aliomba kuwasilisha ushahidi na vielelezo kisha mahakama itoe uamuzi na amri kwa washtakiwa kusafirishwa.

Hata hivyo ushahidi huo haukuweza kusikilizwa kwa sababu Wakili Majura Magafu, Hudson Ndusyepo na Adinan Chitale kuomba muda wa kuupitia kabla haujasomwa mahakamani.

Hakimu Mkeha alikubali kuwapa muda mpaka kesho asubuhi kwa ajili ya mahakama kusikiliza ushahidi huo, alimuru washtakiwa kurudi rumande.

Chanzo: Mtanzania
 
Bora, waendesha mashtaka wa bongo ni vilaza na huyo drug lord atawatafuta mawakili best available...so ingewezekana akashinda au akapata sentence isiyoendana na makosa
 
Yani kumshtaki Raia wenu mmeshindwa mpaka mumpeleke marekani? Chapo alipelekwa america sababu alingiza dawa za kulevya Tani nyingi mno...sasa huyo shkuba hajafkia hata Tani 2 jamni kwel mnashindwa kuendesha nchi na sheria? kama mna ushahidi why mshindwe kumhukumu hapa??? So ina maansha Mahakama za Tanzania hazina meno
 
Shkuba Sijui kama atapendelea kushtakiwa marekani.....bado wanaona anaweza kucheza na mahakama za bongo hapa

Ova
 
Yani kumshtaki Raia wenu mmeshindwa mpaka mumpeleke marekani? Chapo alipelekwa america sababu alingiza dawa za kulevya Tani nyingi mno...sasa huyo shkuba hajafkia hata Tani 2 jamni kwel mnashindwa kuendesha nchi na sheria? kama mna ushahidi why mshindwe kumhukumu hapa??? So ina maansha Mahakama za Tanzania hazina meno
Ndio kaishatoka huyo ... hakuna kesi tena hapo ...
 
Yani kumshtaki Raia wenu mmeshindwa mpaka mumpeleke marekani? Chapo alipelekwa america sababu alingiza dawa za kulevya Tani nyingi mno...sasa huyo shkuba hajafkia hata Tani 2 jamni kwel mnashindwa kuendesha nchi na sheria? kama mna ushahidi why mshindwe kumhukumu hapa??? So ina maansha Mahakama za Tanzania hazina meno

Mkuu nafikiri kutokana na jamaa alivyo anaweza kuhonga mpaka mahakimu wote..ndo maana wanataka kumpeleka kule.
Maana mpaka USA walikuwa wanamtafuta.
 
Good move ,wameshasoma kuwa ushahidi wetu hautoshi kumtia hatiani inawezekana America wana mashataka yake na anatafutwa kwa hiyo ni heri kumpeleka kule ambapo anasubiriwa kutiwa mkononi tu ili habari yake iishe
 
Kama sijaelewa kitu hapa....
1...je serikali ya marekani imewaomba watuhumiwa hao wakajibu mashitaka waliyogunguliwa usa ?
2....je serikali yetu ya Tanzania ndio imeomba raia wetu wakashitakiwe huko marekani bila kosa walilotenda ndani ya radhi ya usa?
NAOMBA kueleweshwa.....napata husia hawa jamaa wanaweza kwenda USA na kula hata na kurudi tz kama raia wema wa marekani
 
Only in Tanzania, kwahio kumbe walikua sahihi walivyosema kuwa tu import "Rahisi" toka nje ya nchi???
 
Tanzania na michezo ya kuigiza,Nimeisoma hii habari kwa muono wangu,Wakili wa serikali anacheza mchezo wa kuigiza kama waliovyowachezewa akina Lema na watu wengine, Mawakili wa serikali waanainajissi sheria za Tanzania.

Huyu jamaa sio mkubwa hivyo katika madawa ya kulevya kama anavyotanganziwa na Media za Tanzania,Huyu jamaa kweli alikuwa anauza madawa ya kulevya lakini hana sifa kama anazopewa

Hii kesi ya huyu jamaa kwa ufupi wakili wa serikali imemshinda!!!,kama kawaida yao polisi walikurupuka kumkamata huyu jamaa,polisi hawana ushahidi wa kutosha kwa huyu jamaa na ndio maana hii kesi ina miaka mingi bila ya kutolewa hukumu

Anachofanya wakili wa serikali ni kupoteza muda tu,ili huyu jamaa azidi kusota mahabusu,swali muhimu la kujiuliza kwani marekani wameomba huyu jamaa apelekwe huko? inavyojulikana kama nchi ya Marekani inamuhitajia mtu, wao ndio wanaomba kuwa huyo mtu wanamtaka apelekwe akashitakiwe Marekani,lakini kwa kesi hii naona imekwenda kinyume yaani ni Wakili wa serikali anaomba wamerekani wamchukue huyu jamaa,sasa wamarekani watamshitaki huyu jamaa kwa kesi gani

Kwa ufupi nchi ya Marekani hakuna muuza unga wa Heroine aliepelekwa huko,wauza dawa za kulevya wanaoshitakiwa marekani wote ni wale wanaouza Cocaine.

Watanzania ni wazuri wa kutoa maamuzi bila ya kufikiri au kutafuta ukweli uko wapi,mpaka sasa tunachosikia ni habari ya upande mmoja tu,upande wa wakili wa serikali na propaganda zake,bado hatujasikia upande wa mshtakiwa,Wakili wa Shkuba nae angelitumia mbinu wanazotumia wakili wa serikali atumie Media kumtangaza mteja wake ili watanzania nao wasikia upande mwengine wa hii stori

Kwa ufupi msilete movie isiokuwa na maudhui kama mmeshindwa kumshtaki ama mahakama imeshindwa kutoa hukumu mwacheni kama ana kosa mshitakini,sheria lazima zifuatwe sio visasi na mihemko
 
Back
Top Bottom