Mada: Mizania kwenye Uandishi wa Habari; Kukabiliana na shinikizo, ushawishi na Upendeleo

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
693
Reaction score
1,158
IMG_20250626_175917_718.jpg

Katika mazingira yenye ushindani wa kisiasa, kijamii na kibiashara, waandishi wa habari wanakumbwa na changamoto kama shinikizo kutoka kwa wenye mamlaka, upendeleo wa vyombo au wahariri na ushawishi kutoka kwa wafadhili au wamiliki wa vyombo vya habari

Katika yote haya, ukweli na haki ya wananchi kupata taarifa sahihi vinapimwa kila siku. Je, ni taarifa zote zinahitaji mizania? Tunawezaje kuhakikisha kuwa habari haipindishwi kwa maslahi binafsi au ya taasisi fulani?

Kufahamu haya na mengine, usikose kujiunga nasi kwenye Mjadala wa Mizania kwenye uandishi wa habari, tutachambua maeneo muhimu yanayohitaji mizania, namna ya kukabiliana na shinikizo la moja kwa moja au na ulinzi wa uhuru wa habari

Kujiunga bofya https://jamii.app/MizaniaSpaceJune26th

Ni leo Alhamisi Juni 26, 2025 kuanzia Saa 12 jioni hadi 2 Usiku

========================================

MAONI YA WACHANGIAJI WALIOPO KWENYE MJADALA

PETER ELIAS (Mhariri Mwananchi):

Mizania bado ni changamoto katika tasnia ya Habari Nchini hasa katika Vyombo vya Habari vya Mtandaoni, ni mara chache unaweza kukuta kuna Mizania sawa.

Matukio kama yale ya kujibiwa kwa Askofu Gwajima yanaonesha kunakosekana kwa Mizania ya usawa, kwa kuwa kila upande unastahili kupata Haki sawa

Wakati huu wa kuelekea katika Uchaguzi kunakuwa na mashinikizo mengi, hasa kutoka kwa Wanasiasa ambao wanakuwa na nguvu ya Ushawishi, ni vema Wadau wa Habari wakawa makini kwa hili

Moja ya kitu au hali ambayo Vyombo vya Habari vinahitaji kusimamia au kuweka mkazo zaidi, ni suala la Wanasiasa wenye Ushawishi kutumia nguvu waliyonayo ndani ya Vyumba vya Habari kwa lengo la kunufaika wao au kwa maana ya kupata maslahi binafsi.

ELIAS MSUYA (MWANAHABARI):

Vyombo vya Habari vilirekodi mkutano wa Waandishi wa Habari na Askofu Josephat Gwajima, baadaye kukawa na shinikizo kwa Vyombo vya Habari vikitakiwa kuondoa taarifa hiyo.

Siku kadhaa baadaye kukawa na Watu mbalimbali wakiwemo Wanasiasa ambao walimjibu (Gwajima) lakini hakukuwa na shinikizo la kwamba hayo majibu nayo yasiwekwe hewani.

Kuelekea kwenye Uchaguzi ni vema Watu wote wanaohusika kwenye Vyama wakapewa Haki sawa, hii isiwe kwa Vyombo vya Habari Binafsi bali vyote.

ERGON (MDAU):

Vyombo vingi vya Habari vimekuwa vikiendesha shughuli zao vikiwa katika Mazingira ya hofu kutokana na uhalisia wa hali ilivyo

Vyombo vya Habari vimekuwa visemeo vya Wanasiasa na wanashindwa kuwa Wasemaji wa Jamii ya kawaida, ndio maana hata taarifa nyingi zinazotawala kwenye ‘Media’ utaona zinahusu nini ambacho Wanasiasa walikuwa wanakisema au wanatarajia kukisema

EDWARD CHAINA (MDAU):

Kuelekea Uchaguzi Mkuu ni kama tayari baadhi ya Vyombo vya Habari vimeshachagua upande, na hilo linaonekana wazi kutokana na kile ambacho wanakifanya

Inapotokea Chombo au Vyombo vya Habari vinapochagua upande, inamaanisha Wananchi hawatapata taarifa kwa Usawa.

Juzi nilikuwa nasikiliza chombo kimoja cha Habari, kuna mwandishi mmoja alikuwa akimlazimisha mwenzake kukubaliana na Serikali kwa kile ambacho wanakijadili, hiyo inaweza kuchangia ushabiki na kukosekana kwa Maadili ya Mizania katika Chombo husika.

KENNETH SIMBAYA (Mkurugenzi Mtendaji UTPC):

Mizania inasaidia kuongeza thamani ya Mwanahabari na Chombo cha Habari ikiwa kutakuwa na usawa na itazingatiwa.

Ukiniuliza mimi, sidhani kama Waandishi wa Habari hawaelewi Mizania kwenye Uandishi wa Habari, swali linakuja, kama wanajua kwanini hawalizingatii hilo?

Tukijibu hilo swali kwanini inakuwa hivyo, Wanahabari tutapata majibu kwanini kuna umuhimu wa kuwa na Mizania.

Kuna hoja ya maslahi ya Wanahabari nayo inachangia suala la Mizania katika Taaluma, wapo ambao hawajalipwa kwa Miaka kadhaa, wanategemea ‘sosi’ ndio awape

Hapo tayari inatengeneza ushawishi kwa yule aliyeandika, hawezi kuandika tofauti na kile ambacho aliyetoa hela hatakipenda.

Unapopata stori ambayo inakuwa ya upande mmoja na ukaitumia, uwezo wako wewe Mwandishi unakuwa unafifishwa

Jamii ikielewa kuwa Chombo chako cha Habari kina mwelekeo fulani inakuwa inashusha thamani ya Biashara yako

Unaporipoti taarifa ya upande mmoja, unawanyima Haki wale wanaotaka kusikia upande wa pili unasema nini

MAXENCE MELO (Mwananchi):

Suala la Mizania bado ni changamoto katika sekta ya Habari, hilo lipo wazi

Unaweza kuzungumzia Habari za Serikali katika Chombo chako na Watu wakakuona bado wewe uliyeandika au kuripoti ni Mtu wa maana na mwenye thamani kubwa, inategemea na Wewe umeitengeneza vipi taarifa yako

Mwanahabari anatakiwa kuelewa yeye anaishi katika Jamii, unachokiandika na kukiripoti ni kile ambacho kinatakiwa kuendana na Jamii husika, usipofanya hivyo ni rahisi Mwananchi kutafuta njia nyingine ya kufikisha ujumbe wake. Ndio maana Watu wengi wanakimbilia kuwasilisha ujumbe wao kupitia njia mbalimbali za Mtandaoni

Sisi JamiiAfrica tumekuwa tukiwapa nafasi Wananchi kueleza hisia zao ikiwemo Kero zao, kufanya hivyo haimaanishi tunaichukia Serikali bali tunaonesha uhalisia wa kile kilichopo kwenye Jamii na ambacho kinahitajika

NEVILLE MEENA (Mjumbe Kamati TEF):

Tunapokwenda kwenye Uchaguzi, Vyombo vyote vya Umma huwa vinatakiwa kuwa chini ya Tume ya Uchaguzi ili vitoe Mizania sawa

Wakati wa Uchaguzi kumekuwa hakuna Mizania ya Usawa kwa Vyombo vya Umma ambavyo vinaendeshwa kwa Kodi za Wananchi, vingi vimekuwa vikiegemea upande mmoja

Suala la kusukumwa kuandika kwa upendeleo ni jambo ambalo lipo kwenye Vyombo vya Habari wala siyo siri, hilo jambo lipo na linatokea, mimi mwenyewe nimekutana na hali hiyo mara tatu katika Vyombo vikubwa hapa Nchini

Wakati wa Uchaguzi nimewahi kukutana na suala la kupata maelekezo kutoka kwa Viongozi wangu kuwa suala hili liende hivi, kulikuwa na maelekezo unatakiwa ufanye hivi kama unaona haifai unaambiwa uchague ubaki au uondoke

Kuna wakati imewahi kutokea Mwenye chombo aliwahi kunishinikiza, nikamshauri kwa Kitaaluma, baadaye akakubali kwa kusema "Haya bana endelea na mambo ya Taaluma yenu", baadaye mmiliki huyo alikuja kukubali kuwa kile ambacho tulimshauri na kukiandika kilikuwa sahihi zaidi

Hao "Content Creators" wao Vyombo vyao havisajili kama ilivyo Vyombo vya Habari, yule anayekupa usajili akikupa maelekezo na akakwambia usifanye hiki, ukifanya anaweza kukufutia usajili

Katika Chombo ninachofanya kazi, tuliwahi kupata barua ya #TCRA ikitutaka kushusha taarifa ambayo licha ya kuwa ilikuwa na Mizania sawa lakini walielekeza hivyo na tukatii kwa kuwa walisema ina vimelea vya uchochezi

CAEJAY (MDAU):

Ikionekana Chombo cha Habari fulani kinaripoti taarifa ambazo haziwafurahishi waliopo katika Utawala, kunatengenezwa Mazingira ya kuonekana hicho kilichoripotiwa sio sahihi

Kuna hii falsafa ya "No Reforms, No Election", inaonekana kuwa ni ya Kichama lakini kuna mambo ambayo ni ya Kitaifa, mambo kama hayo yalitakiwa kuwa katika Vyombo vya Habari ili kujadiliwa na kupatikana kwa Usawa

Baadhi ya Vyombo vya Habari navyo vimeingia katika ombwe la kusifia na kutukuza kutokana na Mazingira

Kinachofanyika kwa sasa katika Vyombo vya Habari ni kuua Uzalendo wa Watanzania, kwani kusema mambo kwa maslahi ya Taifa sio kulichukia Taifa lako

FREDYHERBET (Mdau):

Moja kati ya jambo ambalo linawatatiza au kuwaweka njia panda Wanahabari ni wanapoona urafiki kati ya Mmiliki wa Chombo chao na Mwanasisasa

Mwanahabari anapoona hivyo anaweza kupata hofu ya kuamini kuwa hawezi kuandika taarifa ya pande zote kwa kuwa anajua atamkasirisha bosi wake

Mizania ni ngumu kupatikana inapotokea Mwandishi au Waandishi wanahudumiwa Kiuchumi na mtoa taarifa kwenye kuripoti Habari fulani, inapokuwa hivyo usitegemee kuona Mizania
 
Karibu kwenye Mjadala wa Mizania katika Uandishi wa Habari. Je, waandishi wa habari wanawezaje kusimamia ukweli bila kupindishwa na shinikizo, upendeleo au ushawishi?
Tujadili pamoja, ni maeneo gani yanahitaji mizania zaidi? Uhuru wa habari unalindwaje katika mazingira ya sasa?
Jiunge nasi kuanzia saa 12 jioni hadi 2 usiku kupitia #Xspaces ya JamiiForums
Kujiunga bofya jamii.app/MizaniaSpaceJu
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi202

513510337_1060809299529058_7434884578552654518_n.jpg
 
usikose kujiunga nasi kwenye Mjadala wa Mizania kwenye uandishi wa habari, tutachambua maeneo muhimu yanayohitaji mizania, namna ya kukabiliana na shinikizo la moja kwa moja au na ulinzi wa uhuru wa habari

MENDE hata akiishi Ikulu, bado chakula chake huwa ni uchafu tu.

Asante kwa Mwaliko, tutajiunga kusikiliza.
 
Ilaumiwe Serikali ya ccm kwa kukiuka katiba na sheria za nchi kwa kuwakandamiza na hata kuwaua waandishi wa habari kama Daudi Mwangozi.
 
Katika mazingira yenye ushindani wa kisiasa, kijamii na kibiashara, waandishi wa habari wanakumbwa na changamoto kama shinikizo kutoka kwa wenye mamlaka, upendeleo wa vyombo au wahariri na ushawishi kutoka kwa wafadhili au wamiliki wa vyombo vya habari

Katika yote haya, ukweli na haki ya wananchi kupata taarifa sahihi vinapimwa kila siku. Je, ni taarifa zote zinahitaji mizania? Tunawezaje kuhakikisha kuwa habari haipindishwi kwa maslahi binafsi au ya taasisi fulani?

Kufahamu haya na mengine, usikose kujiunga nasi kwenye Mjadala wa Mizania kwenye uandishi wa habari, tutachambua maeneo muhimu yanayohitaji mizania, namna ya kukabiliana na shinikizo la moja kwa moja au na ulinzi wa uhuru wa habari

Kujiunga bofya https://jamii.app/MizaniaSpaceJune26th

Ni leo Alhamisi Juni 26, 2025 kuanzia Saa 12 jioni hadi 2 Usiku

========================================

MAONI YA WACHANGIAJI WALIOPO KWENYE MJADALA

PETER ELIAS (Mhariri Mwananchi):

Mizania bado ni changamoto katika tasnia ya Habari Nchini hasa katika Vyombo vya Habari vya Mtandaoni, ni mara chache unaweza kukuta kuna Mizania sawa.

Matukio kama yale ya kujibiwa kwa Askofu Gwajima yanaonesha kunakosekana kwa Mizania ya usawa, kwa kuwa kila upande unastahili kupata Haki sawa

Wakati huu wa kuelekea katika Uchaguzi kunakuwa na mashinikizo mengi, hasa kutoka kwa Wanasiasa ambao wanakuwa na nguvu ya Ushawishi, ni vema Wadau wa Habari wakawa makini kwa hili

Moja ya kitu au hali ambayo Vyombo vya Habari vinahitaji kusimamia au kuweka mkazo zaidi, ni suala la Wanasiasa wenye Ushawishi kutumia nguvu waliyonayo ndani ya Vyumba vya Habari kwa lengo la kunufaika wao au kwa maana ya kupata maslahi binafsi.

ELIAS MSUYA (MWANAHABARI):

Vyombo vya Habari vilirekodi mkutano wa Waandishi wa Habari na Askofu Josephat Gwajima, baadaye kukawa na shinikizo kwa Vyombo vya Habari vikitakiwa kuondoa taarifa hiyo.

Siku kadhaa baadaye kukawa na Watu mbalimbali wakiwemo Wanasiasa ambao walimjibu (Gwajima) lakini hakukuwa na shinikizo la kwamba hayo majibu nayo yasiwekwe hewani.

Kuelekea kwenye Uchaguzi ni vema Watu wote wanaohusika kwenye Vyama wakapewa Haki sawa, hii isiwe kwa Vyombo vya Habari Binafsi bali vyote.

ERGON (MDAU):

Vyombo vingi vya Habari vimekuwa vikiendesha shughuli zao vikiwa katika Mazingira ya hofu kutokana na uhalisia wa hali ilivyo

Vyombo vya Habari vimekuwa visemeo vya Wanasiasa na wanashindwa kuwa Wasemaji wa Jamii ya kawaida, ndio maana hata taarifa nyingi zinazotawala kwenye ‘Media’ utaona zinahusu nini ambacho Wanasiasa walikuwa wanakisema au wanatarajia kukisema

EDWARD CHAINA (MDAU):

Kuelekea Uchaguzi Mkuu ni kama tayari baadhi ya Vyombo vya Habari vimeshachagua upande, na hilo linaonekana wazi kutokana na kile ambacho wanakifanya

Inapotokea Chombo au Vyombo vya Habari vinapochagua upande, inamaanisha Wananchi hawatapata taarifa kwa Usawa.

Juzi nilikuwa nasikiliza chombo kimoja cha Habari, kuna mwandishi mmoja alikuwa akimlazimisha mwenzake kukubaliana na Serikali kwa kile ambacho wanakijadili, hiyo inaweza kuchangia ushabiki na kukosekana kwa Maadili ya Mizania katika Chombo husika.

KENNETH SIMBAYA (Mkurugenzi Mtendaji UTPC):

Mizania inasaidia kuongeza thamani ya Mwanahabari na Chombo cha Habari ikiwa kutakuwa na usawa na itazingatiwa.

Ukiniuliza mimi, sidhani kama Waandishi wa Habari hawaelewi Mizania kwenye Uandishi wa Habari, swali linakuja, kama wanajua kwanini hawalizingatii hilo?

Tukijibu hilo swali kwanini inakuwa hivyo, Wanahabari tutapata majibu kwanini kuna umuhimu wa kuwa na Mizania.

Kuna hoja ya maslahi ya Wanahabari nayo inachangia suala la Mizania katika Taaluma, wapo ambao hawajalipwa kwa Miaka kadhaa, wanategemea ‘sosi’ ndio awape

Hapo tayari inatengeneza ushawishi kwa yule aliyeandika, hawezi kuandika tofauti na kile ambacho aliyetoa hela hatakipenda.

Unapopata stori ambayo inakuwa ya upande mmoja na ukaitumia, uwezo wako wewe Mwandishi unakuwa unafifishwa

Jamii ikielewa kuwa Chombo chako cha Habari kina mwelekeo fulani inakuwa inashusha thamani ya Biashara yako

Unaporipoti taarifa ya upande mmoja, unawanyima Haki wale wanaotaka kusikia upande wa pili unasema nini

MAXENCE MELO (Mwananchi):

Suala la Mizania bado ni changamoto katika sekta ya Habari, hilo lipo wazi

Unaweza kuzungumzia Habari za Serikali katika Chombo chako na Watu wakakuona bado wewe uliyeandika au kuripoti ni Mtu wa maana na mwenye thamani kubwa, inategemea na Wewe umeitengeneza vipi taarifa yako
Fisiemu wameamua kubaka media mazima, yaani hata hawajifichi... utasikia muda si mrefu kabla waandishibhawajapost inabidi Bodi ya Ithibati waione, waipitishe ndio waruhusiwe kupost! Sasa ndio nini hivyo? 😒😒
 
Mizania ya uandishi wa habari hapa kwetu bado inahitaji maboresho ya dhati. Kuna juhudi, lakini bado habari nyingi zina bias.

Ni nadra kuona deep analysis ya sera au ahadi za wagombea.

Mfano hivi karibuni kuna watangazaji wa media kubwa wali-brand mpaka magari yao ya kifahari rangi za CCM huko Dodoma, unadhani wanaweza kufanya hivyo kwa vyama vingine?

Waandishi wengi hawajawezeshwa vya kutosha kuchambua mambo kwa undani, na worse enough, mitandao imetapakaa fake news ambazo zina-confuse watu badala ya kuwaweka sawa.
 
Vyombo vya Habari vimekuwa visemeo vya Wanasiasa na wanashindwa kuwa Wasemaji wa Jamii ya kawaida, ndio maana hata taarifa nyingi zinazotawala kwenye ‘Media’ utaona zinahusu nini ambacho Wanasiasa walikuwa wanakisema au wanatarajia kukisema
Sahihi kabisa...

Vyombo vya habari kwa sasa zimegeuka 'mouth piece ' za wanasiasa hasa wenye madaraka.
 
Nadhani swala la mizania limekua ni la kufikirika kwenye tasnia ya habari hasa pale ambapo vyombo vya habari vinafanya biashara, katika uchaguzi wao ni kama peak time. Kama msimu wa Utalii unavyokuaga. Sasa wao wanaona huu ni muda wa kupiga hela zaidi. Lakini pia mizania inakua ya kufikirika kwa sababu Sheria zinazotungwa na Serikali zinasimamiwa na Taasisi hizo hizo za serikali at their advantage.
Pia sheria hizo na kanuni ziko vague kiasi kwamba zinaacha uwazi kwa wale law enforcers kutafsiri sheria na kuitumia vile wanavyotaka. Sasa kwa namna hii mizania inakua ngumu kuwepo kwanza kwa sababu ya financial interests za vyombo vya habari lakini pia Sheria zinaztotungwa na kusimamiwa kwa interest ya serikali.
 
Karibu kwenye Mjadala wa Mizania katika Uandishi wa Habari. Je, waandishi wa habari wanawezaje kusimamia ukweli bila kupindishwa na shinikizo, upendeleo au ushawishi?
Tujadili pamoja, ni maeneo gani yanahitaji mizania zaidi? Uhuru wa habari unalindwaje katika mazingira ya sasa?
Jiunge nasi kuanzia saa 12 jioni hadi 2 usiku kupitia #Xspaces ya JamiiForums
Kujiunga bofya jamii.app/MizaniaSpaceJu
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi202

View attachment 3384744
Miongoni mwa sababu ya kukosekana mizani katika uandishi wa habari Shinikizo kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya habari ambapo wamiliki wa baadhi ya vyombo vya habari wanaweza kutumia ushawishi wao kuathiri mwelekeo wa uandishi ili kulinda maslahi yao binafsi au ya kisiasa.

Lakini maslai madogo kwa waandishi wa habari ambapo waandishi wengi hapa Tanzania awana mishaara na kama wanaolipwa pina wanapokea kiduchu mno hali ambayo inapelekea kutumika zaidi na watu, au wanasiasa kwa sababu watalipwa posho fulani ambayo itamsaidia kwa siku hiyo kupata hata kula so lazima tu habari yake ataandika kwa kuegemea upande mmoja na kusifia tu hata kama kuna sehemu ya kukosoa
 
Back
Top Bottom