Mada Maugo jiuzulu ubondia! Fuata nyayo za Tyson!!!

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Nimeona habari tbc inasema Cheka kaibuka na ubingwa katika pambano la jana dhidi ya Mada Maugo. Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi hicho ni kipigo cha tatu mfululizo mada anakipata kutoka kwa Francis Cheka.

Mara mbili zilizopita Maugo alilalamika kwamba cheka alipendelewa na majaji na waamuzi lakini safari hii pambano limechezeshwa na marefa kutoka nje ya nchi na jopo la majaji pia limeundwa na watu kutoka nje ya nchi lakini bado mada maugo kadundwa japo sijajua kadundwa kwa pointi ngapi.

ushauri wangu kwa mada maugo atangaze rasmi kustaafu ngumi kwani ni dhahiri hamuwezi tena cheka. Asiyekubali kushindwa sio mshindani. Kama ataona kujiuzulu inakuwa ngumu basi atafute watu saizi yake ya kupamabana nao kwani Francis Cheka sio saizi yake hata kidogo.
 
kwa iyo kupigwa na bondia mmoja ndio kigezo cha mtu kustaafu ngumi< hoja yako ni finyu!
 
Toka fb. Mara baada ya pambano msafara wa cheka umepata ajari watu wawili wamevuta . Cheka anashikiliwa na polisi. Mwenye update pls
 
Maugo ni mzuri wa vita ya nje ya uwanja anajua kupiga domo kitu kinachochangia kuhamasisha watu kufuatilia mchezo.Kwa maana nyingine ni mzuri wa promo.Ila anatakiwa kujitahidi kuinua kiwango chake aweze kumatch majigambo anayotoa.Muhamad Ally alikuwa na sifa hiyo.

Isipokuwa nafikiri sio sahihi kupambanisha mabondia walewale mara nyingi hivyo.Sina hakika mapambano haya ya akina cheka na maugo yanaandaliwa kwa kufuata sheria zipi.Katika levo ya kimataifa hairuhusiwi maboxer walewale kurudiarudia mapambano kama wanavyotaka.
 
Kustaafu baada ya hiki kipigo? Hapana sikubaliani nawe! Maugo hawezi kustaafu sasa, mbona umri bado unamruhusu.

Wasiwasi wangu ni kwa cheka kila siku anapigana hapa bongo na maboxer kama akina maugo hiyo haimjengi inabidi atafutiwe mapambano ya huko duniani, oneday tusikie nae anaingia MGM. Huko ndo kuna mkwanja mrefu.Angalia akina Manny wanapigana mara ngapi na wanamkwanja kama chawa.
 
cheka anakula matofali jitu ngumi nzito ka nini? kama vp wamfanyie fitina we mtu gani unashinda wewe tu ka vp akapigane na warusi au wathailand
 
Naomba kujuzwa... Pambano lake na Karama Nyilawila (zamani) alishinda nani? Ingawa Karama ndiye aliyerusha taulo ukumbini kuwa bondia wake (Maugo) hawezi kuendelea na pambano la Cheka..

Je,matokeo hayo kuna anayeyakumbuka..
 
Back
Top Bottom