Mada: Kupigana vita pasipo na vita

Kitaja

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
2,836
1,382
Kama Mtanzania wa kawaida ninapenda kutoa maoni yangu katika vita iliyopamba moto hapa nchini dhidi ya dawa za kulevya. Kilichonisukuma kutoa maoni haya ni baada ya kuona mbinu ama njia zinazotumiwa na aliyejipa “ukamanda” wa vita hii, ama hazitaleta ushindi unao tarajiwa ama kuifanya vita yenyewe kupoteza mwelekeo.

Ndugu zangu Wakurya wana msemo wao maarufu wa “vita ni vita Mura” ( Kwa lafudhi ya Kikurya), ikiwa na maana kuwa vita yeyote uliyodhamiria kupigana, ni sharti uifanyie maandalizi ya kutosha na zana sahihi kwa vita hiyo, la sivyo vita hiyo itakutoa nishai.

Tunayo mifano mingi ya watu walioanzisha vita pasipokuwa na maadalizi ya kutosha na mipango thabiti wakiishia kushindwa vibaya vita hivyo. Mifano michache ni Nduli Idd Amin Dada wa Uganda, huyu alidhani kuwa angeweza kulishinda kirahisi jeshi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Amiri Jeshi Mkuu wakati huo, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kiburi cha Idd Amin kilitokana na kuungwa mkono na mataifa ya kiarabu hasa Libya, Saud Arabia na Palestina. Jamabo ambalo Amin hakujua ni kwamba, tayari alikuwa na vita kubwa ya ndani ya nchi yake japo vita hii ilikuwa ikipaganwa chini kwa chini bila kujua.

Hali hii ilisababisha anguko lake kirahisi na kukimbia nchi mnamo mwezi Aprili 1979 na kukimbilia nchini Libya na hatimaye nchini Saudi Arabia. Idd Amin Alipigana vita mahali pasipokuwa na vita. Huo ndio ukawa mwisho wa zama za utawala wa Idd Amin Dada.

Mfano mwingine ni mpigana vita mwingine aliyeitwa Adolf Hitler, aliyekuwa kiongozi wa chama cha Nazi nchini Ujerumani. Huyu aliamini kuwa dola ya Ujerumani ilikuwa na nguvu mno wakati huo na pasingekuwepo na taifa lolote la kuipinga.

Hivyo alidhani anaweza kuvamia taifa lolote pasipo kuingiliwa na mtu yeyote na kufanya anachotaka. Alifanya hivyo kwa kuivamia Poland Mwaka 1939 na baadae vita hii kusambaa sehemu kubwa ya Ulaya na Afrika ya Kaskazini mwaka 1941.

Hitler aliendeleza mapambano kwa kila nchi ambayo haikuwa upande wake kwa kuivamia Urusi, Uingereza na kisha Marekani. Lengo la Hitler lilikuwa ni kusambaratisha taifa la Urusi ambalo lilikuwa likiibuka kwa nguvu kubwa. Lakini cha ajambu alijipa kazi ya kushambulia kila taifa ambalo aidha halikumuunga mkono ama alidhani linashirikiana na adui wake Urusi.

Japo alijivunia ushirika wa baadhi ya nchi kama Italy, Hungary and Rumania akidharau nguvu ya mataifa kama Japan na Marekani. Matokeo yake, Mmarekani aliyekuwa akimdharanu ndiye aliyechangia kwa sehemu kubwa kwa Hitler kupoteza pambano na kuamua kujiua mwenyewe mwaka 1945. Hitler alikuwa akipigana vita mhali pasipo na vita, na hapo ndipo ikawa mwisho wa Hitler na kukoma kwa vita kuu ya pili ya dunia.

Mifano hii michache inayo ya kutufunza katika vita hii dhidi ya dawa za kulevya. Vita hii inapiganwa duniani kote na pengine hii ndiyo vita kuu ya tatu ya dunia. Mataifa mengi yameingia katika vita hii baada ya kushuhudia nguvu kazi kubwa ya mataifa hayo ikiteketekea huku kikundi cha watu wachache wakiukwaa ukwasi wa kupindukia kwa gharama ya watu wengine.

Ukubwa wa vita hii umesababisha mataifa mengi kuwa na mipango mikakati ama mipango kazi madhubuti ikihanikizwa na fungu kubwa la bajeti. Pamoja na juhudi zote hizo, vita inazidi kukolea na vijana wengi ambao ndio uwanja wa vita wanazidi kuteketea kwa dawa za kulevya.

Tanzania hatujabaki nyuma, tumeingia kwenye vita hii pasipo kusita kwa kuunda kitengo maalum cha kupambana na dawa za kulevya. Juhudi zinaonekana kwani ripoti za “mateka” wa hii vita tunazidi kuzipata katika vyombo vya habari.

Pamoja na hilo, bado vita ni ngumu, vijana wengi wanateketea na hizi dawa, wengi wamekuwa “mazezeta”, wengi wamefariki dunia na wengine kuishia kuwa vichaa.Mifano ya waathirika ni mingi, hao wasanii ni sehemu ndogo sana ya jamii iliyoathirika na janga hili la dawa za kulevya.

Huenda kwa kuliona hili, mkuu wetu wa mkoa wa Dar es salaam, ndugu Paul Makonda kaamua kuibuka na kujiweka mstari wa mbele katika vita hivi. Nachukua fursa hii kumpongeza kwa hatua hii, kwani kwa nafasi yake ya ukuu wa Mkoa wa Dar es salaam, jiji ambalo ni kitovu cha usafirishaji na utumiaji wa dawa hizi, anayo sehemu muhimu sana katika vita hii.

Tatizo kubwa la ndugu yetu Makonda ni kuichukua vita hii kama ni ya kwake mwenyewe. Busara inatuelekeza kuwa, yeye kama Mkuu wa Mkoa alipaswa kuunda tume ya wataalam wa masuala ya uchunguzi akihusisha vyombo vya ulinzi na usalama. Tume hii ingekuwa na jukumu la kuchunguza ni nani wanahusika na wanahusika namna gani na wako wapi na pengine washirika wao ni kina nani na wako wapi.

Kisha Tume ingependekeza hatua madhubuti za kuchukua kwa kila mhusika. Jambo hili lingefanyika kimya kimya. na,lakini matokeo yangekuja kujidhihirisha kupitia kukamatwa kwa wahusika ( mateka) sambamba na ushahidi wa kuwatia hatiani.

Staili ya sasa ya kutajataja tu majina bila ushahidi wa moja kwa moja kwa watuhumiwa unatupotezea muda katika vita hii. Na hili linaweza kusababisha vita hii ikapoteza maana kwa kukosa umakini. Kama ilivyotokea kwa Hitler kupoteza vita, sababu kubwa ilikuwa kutosikiliza ushauri wa “makamanda” wake. Hitler aliamini kuwa ana uwezo wa juu mno wa kivita kuwazidi majenerali wake.

Hili ndilo mkuu wetu wa mkoa anafanya, kwa nini asitumie wataalam alionao katika vita hii? Wengi mtaniambia mbona yuko bega kwa bega na kamanda Siro? Tuwe wakweli, ingekuwa Siro ndiye anyeoongoza vita hii, pengine tungeanza kupata “mateka” halisi wa vita na sio kundi la wasanii wanaotuhumiwa kutumia dawa hizi.

Hata hao waliotajwa sasa hivi bado haisemwi uhusika wao ni wa namna gani kwa ushahidi upi, bado ni kupapasa papasa tu,ni kupigana vita pasipo na vita.

Wito: Hii vita ni yetu sote, sharti vita hii ipiganwe kitaifa kwa mikakati na nyenzo thabiti kwa kutumia jopo la vyombo vetu vyote vya ulinzi na usalama tukitangulizwa na viongozi wa kitaifa. Mh.Makonda upende kupokea ushauri, vita hii ni ngumu, peke yako hutaweza.

Wasalaam,

Kitaja wa JF.
 
Hizi akili za kukataa ushauri na kujifanya mnajua kila kitu ndizo zitakazo tukwamisha. Matokeo ya juhudi zenu yatakuwa hovyo, watakao hoji mtawaona maadui.
Tatizo ni hawa vijana wanaotegemea kula yao kutokana na kupost utumbo humu
 
:(
 

Attachments

  • ym taifa kwanza.png
    ym taifa kwanza.png
    400.7 KB · Views: 17
Jana Mheshimiwa Rais alisema msionee watu katika hii vita.Je alimaanisha watu kama hawa? au pale wabunge walipopitisha azimio la kumhoji Makonda?
 
Back
Top Bottom