kwani dar sio mkoaKwanza kabisa nataka niwachane wale wote wanaotumia vitu kama maji, soda, biscuits e.t.c na kisha kutupa mabaki dirishani..
Imagine mtu anatupa kopo la soda zile "cans" katikati ya barabara. Hujui unaweza kusababisha ajali na kuondoa roho za binadamu wenzio?
Tustaarabike wa Tanzania.. Tusiwe wapuuzi kiasi hicho, huwa nashindwa kuvumilia nikikutana na watu wa aina hii yano roho huwa haitulii mpaka niwachane live..
Hata kama kwenye basi/daladala hakuna trash bin we tupa humo chini ndani ya gari watasafisha wenyewe maana ni wajibu wao ku supply hizo facilities
Tuache uchafuzi wa mazingira na kuhatarisha maisha ya wengine bila sababu maalum
Duh! bahati mbaya simu yangu ya kitochiTupiamo na tupicha wengine hatujawahi safiri tuone namna wanavyoyachafua mazingira tunayotaka kujenga viwanda........
Duh! bahati mbaya simu yangu ya kitochi
na sikuwa na kamera.Ila amini nisemalo nimeliona.
ila tabia hii kama haitaisha basi nikienda mapumziko
ya pasaka nitapiga picha.Asante kwa ushauri.
hebu wakujibu hili..wakikujibu nipigie mluzi nije kucheki jibukwani dar sio mkoa
Nadhani hii inategemea umbali wa safari.kuna safari za mbali makapu hayo yanajaaSisi huku lile dustbin linakuwamo mlemle na matakataka yake had mnafika nahisi hua wanatupa wakifika waendako sijawah kuona yakimwagwa njiani hata siku moja
Niwapongeze wanajf wote kwa kuingia mwaka mpya 2018. Pia niwape pole/hongera na kazi za kulijenga taifa.
Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu iliyonisukuma kuanzisha uzi huu. Katika safari zangu za mapumziko ya sikukuu za Christmas na mwaka mpya,nilisafiri katika mojawapo ya mabasi ya kwenda mikoani(kanda ya ziwa)
Nilishangazwa sana na wahudumu wa mabasi hayo. kumwaga takataka wanazozikusanya kwenye mabasi kutoka kwa wateja wao wanaosafiri mfano,mabox ya biscuit chupa za soda/maji n.k. wakisimama porini kwa lengo la watu kuchimba dawa wanamwaga taka taka hizo kwenye mapori na hivyo kupoteza maana ya kuweka vikapu hivyo kwenye mabasi ambapo lengo lilikuwa kuzuia abiria kutupa taka ovyo njiani.
Rai yangu kwa mamalaka husika ni kuweka udhibiti wa tabia hii, ili kuhakikisha mabasi yana mifuko ya kutunzia taka taka kwenye buti za magari yao mpaka mwisho wa safari au mpaka sehemu sahii yenye kuhusika na takataka hizo ili kuepuka uharibifu wa mazingira kwa kiasi kikubwa.
Karibu kama una wazo mbadala au la ziada ili kuhakikisha hali ya mazingira inatunzwa.
Safi sana,naona huu ni ushauri mzuri.Kuna sheria za halmashauri mabasi yoteKwanini wasifanye kama kwenye air transport, kila stand nchini iwe na kampuni ya usafi kwa magari yanayofika hapo na kuondoka, hii inaweza kurejesha nidhamu kwa maana kwamba bus ambalo halitafika na uchafu liwajibike kueleza uchafu umetupwa wapi kama si kwenye kituo husika
Ni mkoa ila sioni point yako kuuliza hilo swalikwani dar sio mkoa