Mabango ya Lema yaichanganya CCM

Mabango ya Lema yaichanganya CCM

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
[h=1][/h]

mabango.jpg
By Filbert Rweyemamu na Mussa Juma,
Arusha. Mabango ya mgombea ubunge Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema yamezua kizazaa baada ya CCM kutaka yaondolewe.

Mabango hayo yenye sura ya Lema yanayosomeka: “Nyie siyo Wapumbavu, Nyie siyo Malofa, Nyie
ni wana wa Mungu, sisi tunawapenda, Lema tena 2015,” yamebandikwa katika miti, kuta za nyumba na maduka na mengi yako katikati ya Jiji la Arusha.

Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha, Feruz Banno alidai jana kuwa mabango hayo yana lugha ya uchochezi, hivyo, wanaandika barua ya kumwomba msimamizi wa uchaguzi atoe amri yaondoshwe.

Akizungumzia sakata hilo, Lema alisema Rais mstaafu Benjamin Mkapa ndiye aliwaita Watanzania wanaotaka ukombozi kuwa malofa na wapumbavu.

“Mimi nikiwa mbunge wao na mgombea kwa mara nyingine, ninawapenda sana wananchi wangu, ujumbe huo una lengo la kuwatia moyo tu na siyo uchochezi,” alisema Lema.

Hata hivyo, msimamizi wa uchaguzi wa Arusha, Juma Idd alisema bado hajapokea barua hiyo ya malalamiko kutoka CCM.

“Kama wataileta tutatazama wanacholalamikia kama kina mantiki,” alisema Idd.

Wakati huohuo, Lema amemsihi Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa kurejea ofisini kuendelea na majukumu yake kwani muda aliopumzika unatosha.

Lema alitoa wito huo wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi jimboni Karatu uliofanyika katika Uwanja wa Mbowe.

“Nakuomba sana Dk Slaa urudi tufanye kazi, heshima ya Chadema iliyonayo sasa, wewe una mchango mkubwa na hakuna sehemu ya nchi hii ambayo hujafika ili kuhakikisha wananchi wanapata mabadiliko ya kweli, kama mapumziko yanatosha,” alisema Lema.

Alisema licha ya wito wa kumtaka Dk Slaa arejee ofisini kutolewa na watu kadhaa, bado kuna kundi dogo la watu lisilotaka kiongozi huyo arudi kwenye nafasi yake hiyo baada ya sintofahamu iliyotokea kutokana na ujio wa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na baadaye kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema.

Lema aliwaambia wakazi hao kuwa katika mchakato wa Lowassa kuhamia Chadema, Dk Slaa alishiriki kikamilifu tofauti na inavyozungumzwa na baadhi ya watu. “Nawaomba ninyi wananchi ambao Dk Slaa alikuwa mbunge wenu wa kwanza baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini, mumsihi arudi ofisini tuendeleze mapambano ya kuwakomboa Watanzania,” alisema Lema.

Mbunge wa Viti Maalumu aliyemaliza muda wake, Cecilia Paresso aliiponda kauli iliyotolewa na mgombea mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan kuwa watajenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Karatu hadi Mbulu.

Paresso alisema Serikali iliyopo madarakani imeshindwa kujenga barabara hiyo hata kwa kilometa mbili tu, zilizopo Mbulu Mjini kwa kipindi chote cha miaka mitano.



-chanzo: mwananchi

 
Mkapa ataijutia hii kauli yake. Kila sehemu inatumika kuzidisha hasira za wananchi kwa serikali ya CCM.
 
Nilikuwa namchukia sana LEMA, Pamoja na kumdharau ila nimegundua nia njema ya LEMA, sasa namuunga mkono! Kwa dhati tukomboe hili taifa letu kwanza! kutoka mikononi mwa washenzi wa CCM! Godbless J Lema pamoja sana kaka!

#LOWASSAHATUACHIKUKUPENDAKUWANAWE!!!!!
 
Mkapa ataijutia hii kauli yake. Kila sehemu inatumika kuzidisha hasira za wananchi kwa serikali ya CCM.

Wala asijute huu ni mpango wa Mungu ILI JAMBO litimie ni budi jambo litokee jambo lenyewe ndio hilo
 
wewe ni kibaraka wa lowasa, unajulikana na kila aliye kwenye line ya lowasa lazima umfagilie. na hata leo hii lowasa akihamia ACT lazima utawafagilia akina zitto mkumbo na wengineo. huna jipya in short.

Nilikuwa namchukia sana LEMA, Pamoja na kumdharau ila nimegundua nia njema ya LEMA, sasa namuunga mkono! Kwa dhati tukomboe hili taifa letu kwanza! kutoka mikononi mwa washenzi wa CCM! Godbless J Lema pamoja sana kaka!

#LOWASSAHATUACHIKUKUPENDAKUWANAWE!!!!!
 
Mabango yote ya kampeni yanapitia Tume ya Uchaguzi na kupata baraka zake kabla ya kuruhusiwa kutumika. Kama Tume hawajaona huo uchochezi huyu kada wa CCM (Msimamizi wa Uchaguzi) anataka kutuambia nini? Tume inatakiwa imchukulie hatua Mkapa kwanza kabla ya kuyajadili hayo mabango.
 
Lema ni mbunifu sana, kawashika pabaya sasa wamejikuta wakiwa frontline kumtangaza zaidi mpinzani wao.
 
Mabango yote ya kampeni yanapitia Tume ya Uchaguzi na kupata baraka zake kabla ya kuruhusiwa kutumika. Kama Tume hawajaona huo uchochezi huyu kada wa CCM (Msimamizi wa Uchaguzi) anataka kutuambia nini? Tume inatakiwa imchukulie hatua Mkapa kwanza kabla ya kuyajadili hayo mabango.

Na hapo ndiyo mchezo unaanza!
Kama CCM hawakuona tatizo katika kauli hizo alipozitoa Mkapa vipi Leo ziwe tatizo kisa tu zinatumika na Lema?
 
Back
Top Bottom