Alichosema Mwanasheria mkuu wa serikali juu ya No reform no election sio sahihi.
Sababu mabadiliko ya sheria za uchaguzi yaliyofanyika 2024 hayajakidhi vigezo vya kuwa na tume huru ya uchaguzi.
Tume huru ya uchaguzi ni ka ile ya Kenya ambapo mwenyekiti wake hateuliwi na rais.
Uchaguzi hauwezi kuwa huru wakati wakurugenzi walioteuliwa na rais ndio wasimamizi na wasoma matokeo.
Kwa muktadha huu ni wazi kuwa tunahitaji mabadiliko ya katiba ili chaguzi ziwe huru.
Mmesahau alichowahi kusema kada wa CCM kule Mwanza?