MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,255
- 8,027
Katika vitu ambavyo Watanzania wanatekwa vichwa vyao ni pale ambapo Mtu mmoja kwa chama kile kile na mfumo uleule anasema naye anataka kuwaletea mabadiliko yalio bora! Mabadiliko bora ndani ya CCM? Huku anarudia kwa kusema nafanya yote kwa kufuata nyayo za watangulizi wangu! Jamani haya yatakua ni mabadiliko au MABORESHO? hebu tusishikwe akili tuamke tudai mabadiliko ya kweli yatakayobadilisha kila kitu hadi mfumo uliopo, hakuna atakayebadili mfumo ndani ya CCM tusidanganyane!kuwaambia watu kuwa mtapata maisha bora kwa kila mtanzania hayo yalikua maboresho, lakini hayakufanikiwa kwa maana hivi sasa hakuna maisha bora kwa kila mtanzania. Nadhani kwa wasomi watakua wamenielewa vyama.
Mabadiliko yanaambatana na kubadili/kufumua mfumo mzima wa kiutawala katika ngazi za taasisi zote nchini na kuweka mfumo mpya kabisa! Hili hutanguliwa na kutengeneza katiba itakayofumua mfumo wa zamani na kuweka mfumo mpya ulio tofauti kabisa! Huwezi kunadi Sera za mabadiliko huku kwapani umekumbatia kitabu cha ilani ya chama chako chenye Sera za MABORESHO.
Wananchi wanataka MABADILIKO na sio MABORESHO kwa sasa tafadhali.